Mwanzilishi wa bendi ya Boy band, Lou Pearlman amefariki akiwa na umri wa miaka 62.
Pearlman pia ni mwanzilishi wa bendi ya backstreet boys maarufu iliyosajili mauzo mengi pamoja na ile ya Nsync.
Alifungwa kwa takribani miaka 25 mwaka 2008 kwa kuhusika na udanganyifu wa mpango wa ponzi uliogharimu dola 300.
Mwimbaji wa Nsync Lance Bass alituma ujumbe katika twitter alisema kuwa Pearlman hakuwa mfanyabiashara mzuri lakini hasingekuwa hapo alipo bila ushawishi wake.
Sababu ya kifo chake bado haijulikani.
Tuesday, August 23, 2016
MWANZILISHI WA BENDI ZA BACKSTREET BOYS NA NSYNC AFARIKI.
KIONGOZI WA BOKO HARAM AJERUHIWA NA JESHI LA NIGERIA.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Abubakar Shekau, amejeruhiwa vibaya kwenye shambulio la angani lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo.
Makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa.
Taarifa kutoka katika jeshi la angani la Nigeria, limesema shambulio hilo lilitekelezwa ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa jeshi, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.
Kiongozi wao, anayefahamika kama Abubakar Shekau anaaminika kujeruhiwa vibaya begani, jeshi limesema kupitia taarifa iliyotolewa na naibu mkuu wa mawasiliano Kanali Sani Kukasheka Usman.
Kundi la Boko Haram hivi karibuni limekabiliwa na mzozo wa viongozi.
Kundi la Islamic State lilitangaza kuwa Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa kundi la Boko Haram.
Lakini muda mfupi badae, Shekau alisema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo na akamshutumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.