Friday, November 18, 2016

JIWE LA KALE LENYE AMRI KUMI ZA MUNGU LAUZWA.

Jiwe hili la amri kumi za Mungu liligunduliwa mwaka 1913
Jiwe la kale zaidi lenye amri kumi za Mungu limeuzwa kwenye mnada nchini Marekani kwa dola 850,000.
Jiwe hilo ambalo lina urefu wa sentimita 60 limeandikwa kwa lugha ya kiyahudi
Liliuzwa katika soko la mnada huko Los Angeles, kwa masharti kuwa litawekwa kwa umma kuliona.
Jiwe hilo liligunduliwa mwaka 1913, wakati wa ujenzi wa reli karibu na mji wa Yavneh ulio nchini Israel.
Wauzaji wanasema kuwa jiwe hilo ni la kutoka miaka ya 300 na 500 AD.
Amri ambayo haionekani kwenye jiwe hilo ua "Usitumia jina la Mungu kwa njia isiyostahili" sasa pameandikwa kwa kutoa wito kwa waumini wa Samaria wakitakiwa kujengwa kwa hekalu katika mlima Gerizim, eneo takatifu juu ya mji wa Nablus, ambayo ndio sasa Ukingo wa Magharibi.
Jamii ya Samaria ina historia ndefu eneo la Mashariki ya Kati, licha watu hao kutoweka hadi chini ya watu 1000 miaka ya hivi karibuni.

VIBAKA WAMVAMIA NA KUMPORA BABY MADAHA.

baby-madaha
BABY MADAHA.
Mwigizaji wa filamu za bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, amejikuta akishikwa na butwaa baada ya kuporwa pochi yake na vibaka wawili waliokuwa katika pikipiki eneo la Makonde, Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Mwigizaji huyo alipatwa na mkasa huo usiku wa juzi, wakati akielekea kununua chipsi karibu na kituo cha daladala cha Makonde. Ghafla pikipiki iliyokuwa na vibaka wawili waliopakizana ilipita kwa kasi karibu yake na kumpora simu mbili aina ya Samsung na mkoba uliokuwa na vipodozi, fedha na hati ya kusafiria.
“Yaani hata sikuamini nilipokutana na mkasa ule, nilikuwa nikitokea Uwanja wa Ndege nikielekea kwangu Makonde, lakini nikiwa kituo cha daladala Makonde nilihisi njaa, nikaelekea kwenye banda linalouza Chipsi, ndipo nielekee nyumbani, lakini kabla sijafika katika banda wakaja watu wawili wakiwa wamepakizana katika pikipiki iliyokuja kwa kasi wakanipora mkoba wangu na kukimbia kwa kasi.
“Katika pochi yangu kulikuwa na simu mbili aina ya Samsung, dola 100 ambazo ni zaidi ya laki mbili, vipodozi na hati yangu ya kusafiria, lakini kwa bahati nzuri nilishika sura za wale vibaka na baada ya kutoa taarifa polisi ulifanyika msako mkali wakakamatwa wengi na nilipoitwa nilifanikiwa kuwatambua walionipora,’’ alieleza Baby Madaha.
Alisema baada ya utambuzi huo ulifanyika ukaguza katika nyumba wanazoishi vibaka na baadhi ya vitu, ikiwemo simu moja, vipodozi na dola 100 zikapatikana, upelelezi unaendelea kusaka vitu vilivyobaki, ikiwemo hati ya kusafiria, watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi.
Kwa sasa Baby Madaha na wasanii wenzake wawili, Isabella Mpanda na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wapo mbioni kuzindua wimbo wao mpya wa ‘Mario’ kupitia kundi lao la Scorpion Girl.

MWANAFUNZI WA UDOM KORTINI KWA UGAIDI.



Wakati mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akifikishwa mahakamani kwa mashitaka ya ugaidi mkoani Dodoma, wadau wanaotetea haki za wanawake na watoto wamelaani kitendo cha wanawake wanne na watoto kukamatwa wakijihusisha na mafunzo ya ugaidi na kuiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Mkoani Dodoma, mtu anayehusishwa na vitendo vya ugaidi, Azan Abubakary amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini na kusomewa mashtaka yake.
Akiwa amevalia fulana ya rangi ya bluu na kijani na suruali nyeusi na viatu vya matairi (maarufu kama katambuga), alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mwajuma Lukindo.
Mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa makosa ya kufadhili ugaidi chini ya kifungu cha 13 cha sheria ya makosa ya kuzuia ugaidi namba 21 ya mwaka 2002. Ilidaiwa kuwa Mei 15, 2016 alimtumia fedha Mohamed Ibrahim kwa njia ya M-Pesa kiasi cha Sh 265,000 katika namba +254 708104109 kwa ajili ya kufanyia ugaidi nchini.
Aidha Julai 22, 2016 Abubakary alionekana eneo la Dodoma akituma fedha kwa njia ya M-Pesa kwa Mohamed Ibrahim Sh 148,000 kwa ajili ya kufanya vitendo vya ugaidi. Hakimu Lukindo alisema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma katika taarifa yake kwa vyombo vya habari imesema kwamba mtuhumiwa huyo aliyefikishwa mahakamani ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha Afya na yupo mwaka wa pili.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, mtuhumiwa alikamatwa Nzega mkoa wa Tabora baada ya kugundulika kuwa anajihusisha na mtandao wa ugaidi wa kundi la ‘Al Shabaab’ kutoka Somalia.
Kamanda alisema mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa za Intelijensia ya Polisi katika masuala ya ugaidi. Katika tukio lingine, polisi wanafanya uchunguzi wa kifo cha mashaka kilichotokea Novemba 15, mwaka huu saa 12 jioni katika Hoteli ya Kitemba katikati ya mji wa Dodoma.
Katika tukio hilo, Ofisa mstaafu wa Magereza aliyefahamika kwa jina la DCP – Luvugo Chiza, mwenye miaka 62, mkazi wa Kigoma aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma, alishuka Dodoma na kulala katika hoteli hiyo kwa ajili ya kushughulikia viwanja vyake CDA.
Ofisa huyo alikutwa amefariki dunia huku akitokwa na damu puani, pia katika chumba chake yalikutwa mabaki ya vyakula, chips, nyama ya kuku, nyama ya nguruwe, chupa ya maji na kinywaji aina ya Savana.

MWANAUME MWENYE HIV ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAWAKE 104 MALAWI.

Eric Aniva alikiri kufanya mapenzi na wanawake pamoja na wasichana 104
ERIC ANIVA.
Uamuzi wa kesi ya mwanamme mmoja nchini Malawi unatarajiwa kutolewa wiki hii, baada ya kuiambia BBC kuwa alifanya mapenzi na wasichana kama sehemu ya mila.
Eric Aniva alikamatwa mwezi Julai kufuatia amri ya rais, baada ya kukiri kuwa alifanya mapenzi yasiyo na kinga na wasichana walio na umri wa hadi miaka 12, na kuwa kimya juu ya hali yake ya kuugua ugonjwa wa ukimwi.
Aniva anasema kuwa alipewa vibarua na familia za wasichana hao kushiriki mapenzi nao, kwa tamaduni ambayo jamii inaamini kuwa huwezesha wasicha kuingia utu uzima.
"Tunaamini kuwa ikiwa mjane au mwanamme aliyefiwa hawezi kusafishwa kwa njia ya mapenzi, huenda kisa kibaya kikafuatia kama kifo kwa majane au mwanamme aliyefiwa au kwa ukoo mzima," alisema mhudumu mmja wa jamii.
Wakati rais wa Malawi Peter Mutharia aliamrisha mwanamme huyo akamatwe, alitaka Aniva ashtakiwe kwa kuwabaka wasichana wadodgo, lakini hata hivyo hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.
Kwa hivyo sasa Aniva ameshtakiwa kwa kushiriki utamaduni wenye kuumiza, chini ya kipengee cha chato cha sheria ya usawa wa kijinsia nchini Malawi ambapo alifanya mapenzi na wajane.
Katika kesi hii wanawake wawili wamejitokeza ili kutoa ushahidi dhdi ya Aniva, licha ya mmoja kusema kuwa alifanya mapenzi naye kabla ya mila hiyo kupigwa marufuku huku mwingine naye akisema kuwa alifanikiwa kukimbia kabla ya kitendo cha ngono kufanyika.
Hadi miaka michache iliyopita, mila hii ilikuwa maarufu katika wilaya yote kwa mjane kufanya mapenzi na mwanamme mara tatu kwa siku kwa usiku tatu au nne.
Eric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti
Mwanamme huyo anaweza kuwa ndugu wa mmewe, lakini wakati mwingine mtu kutoka nje hutafutwa kama Aniva kuweza kushiriki kitendo hicho.
Ikiwa aliyefiwa ni mwanamme, mwanamke hutafutwa kuweza kufanya mapenzi naye.
Kinachowatisha watu nchini Malawi kuhusu Aniva, ambaye alidai kufanya mapenzi na wanawake 104 pamoja na wasicha, wakati wa mahojiano na BBC ni kuwa hukuachana na tabia hiyo licha ya kugundua kuwa alikuwa na virusi vya HIV
"HIV inaua. Itakuwaje mtu mwenye virusi kufanya kile alichokifanya? Nafikiri yeye ni shetani. Ningekuwa hakimu ningempa hukumu ya kifo na kifungo cha maisha," alisema mhubiri Paul Mzimu.

DZEKO APEWA KADI NYEKUNDU KWA KUMVUA MWENZAKE SURUALI.

Edin Dzeko
EDIN DZEKO.
Mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko alipewa kadi nyekundu na kulazimika kutoka uwanjani baada ya kukasirika na kumvua suruali mchezaji mwenzake.
Mchezaji huyo alikuwa akishiriki katika mechi dhidi ya Ugiriki wakati alipoangushwa wakati Bosnia ilipokuwa inaongoza katika mechi ya kutafuta kufuzu kwa kombe la dunia.
Mechi hiyo ilikuwa ikiendelea vyema baada ya mpira wa adhabu wa Miralem Pjanic kugonga chuma cha goli,kumgusa mlinda lango la kuingia wavuni.
Lakini ilisitishwa dakika tano baada ya bao hilo huku baadhi ya mashabiki wa Bosnia wakiwasha moto na kurusha miale ya moto pamoja na viti vilivyovunjika huku baadhi ya mashibii wa Ugiriki wakiimba nyimbo dhidi ya Bosinia.
Ni wakati huo ambapo makabiliano kati ya nahodha Dzeko na Kyriakos Papadopoulos zikiwa zimesalia dakika 10 za mechi yalimtia hasira Dzeko ambaye alimvua suruali mwenzake kwa hasira hatua iliosababisha apewe kadi nyekundu.
Hatua hiyo ilizua hali ya mshikemshike miongoni mwa wchezaji wa timu zote mbili.
Papadopuolos naye hakubali na akajihusisha katika katika mvutano uliomlazimu kupata kadi nyekundu huku Dzeko akipewa kadi ya njano ya pili na kutolewa uwanjani damu ikionekana kumtoka katika sikio lake moja.
Baadaye Ugiriki ilisawazisha na kuinyima Bosnia ushindi huo kupitia Orestis Karnezis

AZAM FC YASAJILI WACHEZAJI WAWILI.

Azam Fc
Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC,imeingia mkataba na washambuliaji nyota kutoka Ghana, Samuel Afful na Yahaya Mohammed.
Zoezi la kuingiana mikataba limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul Mohamed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez pamoja na wakala anayewasimamia wachezaji hao, Kingsley Atakorah, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Adom Wonders Academy ya nchini Ghana.
Wakati Afful, 20, akisaini mkataba wa miaka mitatu, Mohammed naye amesaini kandarasi ya miaka miwili tayari kabisa kuanza kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Afful ambaye mpaka sasa yumo katika vikosi vya timu za vijana za Ghana chini ya umri wa miaka 20 na 23, anajiunga Azam FC akitokea timu ya Sekondi Hasaacan ya Ghana, ambayo aliifungia mabao tisa msimu uliopita.
Moja ya rekodi yake ni kuifungia bao muhimu timu ya Taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) mwaka jana dhidi ya Zambia kwenye ushindi wa mabao 2-1, lililoipa nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini New Zealand, baada ya kutinga nusu fainali ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana (U-20) zilizofanyika Senegal mwaka jana.
Mohammed, 28, ambaye ni mshambuliaji mzoefu anayetokea Aduana Stars, alikuwa ni mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana msimu uliopita akifunga mabao 15, pungufu ya mabao mawili na kinara Latif Blessing (Liberty Proffessional) aliyetupia 17.

TUZO YA FORBES YA MTU MASHUHURI 2016 KABISA AFRIKA YAENDA AFRIKA KUSINI.

Thuli Madonsela akihutubu Johannesburg
THULI MANDONSELA
Aliyekuwa mlinzi wa maslahi ya umma nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela ametawazwa kuwa mtu mashuhuri zaidi wa Forbes wa mwaka 2016.
Bi Madonsela aliwashinda marais watatu wa Afrika, raia mwenzake wa Afrika Kusini na watu wan chi ya Rwanda katika kushinda tuzo hiyo.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake Ameenah Gurib wa Mauritania walikuwa wameteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Mwingine ni mfanyabiashara wa Afrika Kusini Michiel le Roux ambaye ni mwanzilishi wa benki ya Capitec.
Bi Madonsela, aliyetangazwa mshindi kwenye hafla iliyoandaliwa Nairobi Alhamisi jioni, amejulikana kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi alipokuwa anahudumu kama mlinzi wa maslahi ya umma Afrika Kusini. Alihudumu kuanzia mwaka 2009 hadi 14 Oktoba mwaka huu, muhula wa miaka sita.
Kipindi hicho, alimchunguza rais, akawachunguza wakuu wa polisi, maafisa wakuu serikalini na hata wanasiasa wa upinzani.
Uchunguzi wake ulipelekea kusimamishwa kazi kwa mkuu wa polisi Bheki Cele mwaka 2011.
Aliwahi kumchunguza pia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters Julius Malema ambaye mwishoni mwa kipindi chake, alimuunga mkono alipofanya uchunguzi kuhusu uhusiano wa Rais Jacob Zuma na familia tajiri ya Gupta.
Alimchunguza pia Rais Zuma kuhusu ukarabati uliofanyiwa makao yake Nkandla.
Bi Madonsela ni mama wa watoto wawili.
Alikuwa wakili na kiongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa harakati za kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Huu ni mwaka wa sita kwa tuzo hiyo ya Forbes kwa mtu mashuhuri zaidi Afrika kutoleewa.

Washindi wa awali ni:

  • 2011 - Sanusi Lamido Sanusi, aliyekuwa wakati huo Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria.
  • 2012 - James Mwangi, CEO wa Benki ya Equity, Kenya
  • 2013 - Akinwumi Adesina, aliyekuwa wakati huo Waziri wa Kilimo Nigeria.
  • 2014 - Aliko Dangote, mwenyekiti wa CEO wa kampuni ya Dangote Group, Nigeria.
  • 2015 - Mohammed Dewji, CEO wa kampuni ya MeTL Group, Tanzania

MWILI WA MSICHANA ANAYETARAJIA KUFUFULIWA KUHIFADHIWA.

Mchoro wa jinsi miili huenda ikahifadhiwa siku za usoni
Msichana ambaye alitaka mwili wake ugandishwe na kuhifadhiwa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai wakati mmoja siku za usoni, alipata ushindi wa kihistoria saa chache baada ya kufariki dunia.
Msichana huyo alitaka mwili wake uhifadhiwe kwenye friji maalum baada ya kufa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai, na hata ikiwezekana aponywe, baadaye. Mamake alimuunga mkono lakini babake alikuwa anapinga wazo hilo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 14 alikuwa anaugua aina nadra sana ya saratani.
Jaji katika mahakama ya Uingereza aliamuru kuwa mama yake ndiye angekuwa na usemi wa mwisho kuhusu mwili wake.
Mwili wa msichana huyo, aliyefariki mwezi Oktoba, sasa umesafirishwa kwa ndege hadi Marekani kuhifadhiwa.
Msichana huyo alikuwa anaishi London na alitumia mtandao wa intaneti kusoma zaidi kuhusu teknolojia ya kuhifadhi miili ya cryonics miezi ya mwisho ya uhai wake.

Matumaini siku za usoni.

Cryonics ni teknolojia inayotumia kuuhifadhi mwili kwa kuugandisha kwa matumaini kwamba huenda ikawezekana kuufufua au kupata tiba siku za usoni.
Msichana huyo alimwandikia jaji na kumwambia kwamba alitaka "kuishi muda mrefu" na hakutana "kuzikwa ardhini".
Freezing heart valves for preservation
Aliandika: "Nafikiri kuhifadhiwa kwa teknolojia ya cryonic kutanipatia fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni baada ya miaka mia moja."
Jaji Justice Peter Jackson, alimtembelea msichana huyo hospitalini na anasema aliguswa sana na ujasiri ambao msichana huyo alikuwa nao katika kukabiliana na maradhi aliyokuwa anaugua.
Kwenye uamuzi wake, alisema, uamuzi huo haukuwa kuhusu usahihi au kutofaa kwa cyronics bali mzozo kati ya wazazi wa msichana huyo kuhusu hatima ya mwili wa binti yao.

Mwili kugandishwa.

Cryonic ni shughuli ambayo imekuwa na utata mwingi na hakuna ajuaye iwapo inawezekana kufufua miili iliyogandishwa kufikia sasa.
Kuna vifaa Marekani na Urusi ambapo miili inaweza kuhifadhiwa kwenye madini ya naitorjeni kwenye baridi kali (chini ya nyozijoto -130C) - lakini huduma hiyo haipo Uingereza.
Gharama ya kugandisha mwili kwa muda usiojulikana inakadiriwa kuwa takriban £37,000.

Barua ya msichana kwa jaji.

"Nimetakiwa kueleza ni kwa nini nataka jambo hili lisilo la kawaida lifanyike.
"Nina miaka 14 pekee na sitaki kufariki dunia lakini najua nitafariki dunia.
"Nafikiri kuhifadhiwa kwa njia hii ya cyronic kutanipa fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni miaka mia moja ijayo.
"Sitaki kuzikwa ardhini.
"Ninataka kuishi na niishi muda mrefu na nafikiri siku za usoni huenda kukapatikana tiba ya saratani ninayougua na kuniamsha.
"Ninataka kupata fursa hii.
"Hayo ndiyo mapenzi yangu.
Wazazi wa msichana huyo walitalakiana na msichana huyo hakuwa amekutana na babake kwa miaka sita kabla yake kuanza kuugua.
Mamake aliunga mkono mapenzi yake ya kutaka mwili wake uhifadhiwe kwa kugandishwa lakini babake alikuwa anapinga.
Babake alisema: "Hata kama itawezekana afufuliwe na atibiwe tuseme miaka 200 ijayo, huenda hatapata jamaa yeyote anayemjua na huenda asikumbuke mambo mengi. Atakuwa katika hali ya masikitiko ikizingatiwa kwamba ana miaka 14 na atakuwa Marekani."
Ingawa baadaye alibadili msimamo wake na kusema anaheshimu uamuzi wa bintiye, alitaka kuuona mwili wa bintiye baada ya kifo chake, jambo ambalo msichana huyo alikuwa amekataa.
Jaji alisema ombi la msichana huyo lilikuwa la kipekee kuwahi kuwasilishwa England na Wales, na labda kwingineko.