Saturday, August 13, 2016

SHAH RUKH KHAN AOMBWA MSAMAHA BAADA YA KUZUIWA BILA KOSA LOLOTE AIRPORT NCHINI MAREKANI

                         

Muigizaji maarufu duniani Shah Rukh Khan siku ya ijumaa alipost kwenye akaunti yake ya twitter kuwa alipata kizuizi katika uwanja wa ndege wa Marekani. Balozi wa Marekani nchini India Richard Verma ameomba msamaha kwa kitendo hicho na kusema mamlaka inafanya kila iwezalo kuzuia tukio kama hilo kutokea tena.

Mwaka 2012 pia alikamatwa na kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa white Plains karibu na jiji la New York kwa dakika 90 na mwaka 2009 pia alizuiwa katika uwanja wa ndege wa New York kwa masaa mawili.
"ninaelewa kikamilifu jinsi hali ya usalama wa Marekani na dunia ulivyo, lakini kukamatwa kwenye idara ya uhamiaji ya Marekani kila wakati inaudhi".

MZEE YUSUPH KUACHA MZIKI NA KUMRUDIA MUNGU.

                                   

Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph "Mfalme wa taarabu" amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita. Taarifa zilienea kwenye mitandao ya kijamii siku mbili zilizopita kuwa nguli huyo ameachana na mziki huo.

Mzee Yusuph alikubali kuhusiana na taarifa hizo kuwa ni za kweli na akusema "nashangaa hizi taarifa zinasemwa leo, ni suala la muda mrefu takribani miezi miwili iliyopita na kwa sababu nimeamua kurudi kwa Allah".

Alisema familia yake imekubaliana na maamuzi yake, kwa sasa ataanza kuimba kaswida zenye mafundisho ya dini. Alipoulizwa kwanini alichukua uamuzi mkubwa kiasi hicho, alijibu kifupi,
"ndiyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini"
Ijumaa hii Mzee Yusuph alikuwa katika Swalat Jumaa ndani ya masjid Taqwa Ilala Bungoni, alipopata fursa ya kuongea na waumini alishindwa kuvumilia na kuanza kulia.
Pia alisema kuwa aataitisha mkutano rasmi kuelezea swala hilo.


HISTORIA FUPI YA MZEE YUSUPH.
Mwimbaji na Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, amezaliwa Zanzibar mwaka 1977 na amemaliza darasa la 10 katika Shule ya Haile Selasie.

Alianza mziki baada ya kumaliza darasa la kumi na  alikuwa anafanya mziki na maigizo, huku anaendelea na shule na ikafika pahali akachukuliwa na bendi ya melody.

Mzee Yusuph ameshinda tuzo nyingi katika tasnia ya mziki wa taarabu zikiwemo Kilimanjaro Music Awards 2014-2015.

VERA SIDIKA AFUNGUKA.

                                     VERA SIDIKA

Mrembo machachali kutoka Kenya Vera Sidika afunguka na kuelezea kuhusu malumbano yake na Huddah Monroe mrembo kutoka huko huko Kenya. Vera alifunguka na kusema kuwa hana tatizo na mtu yoyote, bali watu ndio wenye matatizo na mimi. Marafiki zangu walikuwa wakinambia kuwa Huddah ananitukana sana kwenye mitandao ya kijamii. Vera aliendelea na kusema nime-ignore bifu nyingi na Huddah lakini bado ananitafuta.

HUDDAH MONROE

Maneno aliyokuwa anayasema wiki zilizopita kwenye Snap chat yaliniuma sana kwasababu alinisingizia kuwa nina ukimwi wakati mimi niko safi, ndio maana nikaamua kwenda kupima ili nimthibitishie kuwa sina ukimwi mimi. Na Huddah alishawahi kuwa rafiki yangu kipindi cha nyuma tena tulikuwa karibu sana. Vera pia alikubali kuwa akipatanishwa na Huddah atakubali kwasababu yeye hana tatizo na mtu yoyote na hapendi mabifu yasiyo na maana.

VERA ATAJA SABABU ZINAZOMFANYA KUMKUBALI DIAMOND.
Mrembo huyo wa Kenya alijibu swali la msanii yupi hapa bongo anamsikiliza sana kati ya Diamond na Alikiba. Vera alisema anamsikiliza sana Diamond, na kuzitaja sababu za kumkubali kwamba;
  • Style yake ni tofauti pia ni nzuri, naona kuwa anajikakamua kwa kutoa hit after hit bila kutulia.
  • Lakini pia si mziki peke yake, ila ameweza kuwasaidia vijana kwa kuwapatia nafasi ya ku-explore talent zao kama sasa hivi wako artist ambao wako chini yake.
Vera aliongeza na kusema pia Diamond ni baba mzuri anayetimiza majukumu yake.

DIAMOND AZIDI KUNG'ARA.

                                  

Mwanamziki Diamond Platnumz anayetamba kwa sasa na wimbo wa kidogo aliowashirikisha mapacha wawili Psquare kuingia kwenye playlist ya kituo cha redio cha BBC Radio 1xtra, kitu ambacho hakuna msanii wa bongo aliyefika huko.

Ijumaa hii, August 12 kituo hicho kilitoa playlist za wiki nzima, kidogo ikiwemo ya Diamond. Kidogo itakuwa kwenye playlist ya nyimbo zitakazokuwa zinachezwa wiki nzima kwenye 1xtra.
Ni wasanii wachache sana waliowahi kufika huko barani Afrika. Miongoni mwao ni Wizkid, AKA, D'banj huku hakuna msanii kutoka Tanzania aliyewahi kufika huko zaidi ya Diamond kuvunja rekodi na kufika huko.

USAILI WA MAISHA PLUS AFRIKA MASHARIKI SASA.


Muongozaji wa Maisha Plus, Masoud Kipanya atangaza rasmi kuwa usaili umeanza, tena mwaka huu utahusisha nchi za Afrika Mashariki na sio Tanzania peke yake kama ilivyozoeleka. Usahili umeanza na unaendelea Rwanda-Kimihurura Kigali.
Ratiba ya usaili Afrika Mashariki ipo hivi;
  • Burundi- Hotel Club du lac Tanganyika, Bujumbura
  • Kenya- Royal Court hotel, Mombasa
  • Uganda- Monot bar & lounge (Bugolobi), Kampala
  • Zanzibar- Ngome kongwe