J Lo (47) na Casper (29) walianza mahusiano yao oktoba 2011, ilisemekana kama waliachana mwaka 2014 ila wachunguzi walisema hawakugombana na walikuwa wakiishi nyumba moja.
Wiki kadhaa zilizopita walikuwa vizuri tu hadi J Lo akampaisha aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Marc Antony katika tamasha lake huko Las Vegas.
Hicho ndo kinasemekana ndio chanzo cha J Lo na Casper kuvunja mahusiano yao na kila mtu kuendelea na shughuri zake kama apo awali.
Friday, August 26, 2016
J LO NA CASPER SMART WAVUNJA MAHUSIANO YAO.
JARIDA LA FORBES LIMEMTAJA THE ROCK KAMA MSANII WA KWANZA DUNIANI ANAYELIPWA KIASI KIKUBWA CHA PESA.
Muigizaji maarufu wa Marekani na Canada, Dwayne Douglas Johnson maarufu kama "The Rock" ametajwa katika jarida la Forbes kama ni msanii namba moja duniani anayelipwa pesa kubwa kiasi cha dola za kimarekani $64.5 milioni kwa mwaka.
Hayo mamilioni yametokana na kulipwa kwenye movie alizocheza kama Central Intelligence na Fast 8 na pia movie ambayo bado haijatoka inayoitwa Baywatch.
Juhudi alizoonyesha kwenye movie ya Fast and furious na movie yake ya San Andreas ya mwaka 2015 zimezaa matunda hayo.
MUOGELEAJI WA MAREKANI RYAN LOTCHE ASHITAKIWA.
Polisi nchini Brazil wamemshtaki muogeleaji wa olmpiki wa Marekani Ryan Lotche kwa kutoa madai ya uongo kuwa yeye na wenzake watatu waliibiwa kwa kushikiwa bunduki wakati wa michuano ya Rio, kitu ambacho ni upotoshaji.
Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela.
Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lotche atatakiwa kujibu mashtaka hayo. Idara ya Marekani imesema inatambua ombi hilo.
Lotche ameondoka Brazil kabla hajaojiwa na polisi. Ameomba msamaha kwa kusema uongo juu ya kuibiwa. Lotche amepoteza wadhamini wake wakubwa wanne kufuatia tukio hilo na hivyo kuweka hatarini kazi yake ya uogeleaji.
SAMATTA ASAIDIA KLABU YAKE KUFUZU MASHINDANO YA EUROPA LEAGUE.
Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.
Hii ni baada ya klabu yake KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.
Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa jana jioni.
Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.
Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.
Samatta pia alioneshwa kadi ya njano dakika ya 69.
Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadae leo ijumaa mwendo wa saa tisa za Afrika Mashariki.
WANASAYANSI WAGUNDUA SAYARI INAYOFANANA NA DUNIA.
Wanasayansi wamegundua sayari ambao inakaribiana sana na dunia kwa mazingira na ukubwa wake ambayo inazunguka nyota ijulikanayo kama Proxima Centauri iliyo na mfumo unaokaribia zaidi mfumo wetu wa jua.
Sayari hiyo ambayo kwa sasa imepewa jina la Proxima b inazunguka nyota hiyo katika eneo ambalo kuna uwezo mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.
Proxima inapatikana umbali wa kilomita tirioni 40 na inaweza kumchukua mtu akitumia teknologia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu, maelfu ya miaka kufika huko juu.
Licha ya kwamba ni mbali sana kugunduliwa kwa sayari hiyo, huenda kukasisimua hisia na mawazo ya binadamu na wanasayansi kuhusu kuwepo kwa viumbe katika sayari nyingine au uwezekano wa wakati mmoja watu kuishi kwenye sayari nyingine.
"Kusema ukweli kufika huko kwa sasa hiyo ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja mtu anaweza kutuma chombo huko.