Msanii Diamond Platinumz ndiye mshindi wa tuzo ya msanii bora wa tuzo za Afrimawards upande wa wanaume katika eneo la Afrika Mashariki.
Diamond alijipatia tuzo tatu katika tamasha hiyo iliofanyika mjini Lagos nchini Nigeria huku nyota wa Afrika waliohudhuria wakiwaenzi Manu Dibango, King Sunny Ade na marehemu Papa Wemba.
Msanii wa Uganda Cindy Sanyu naye alijishindia tuzo la mwanamuziki bora wa kike Afrika Mashariki huku Mwanamuziki Wizkid wa Nigeria akijishindia tuzo la msanii bora wa mwaka Afrika.
Tuzo ya Kolabo bora zaidi iliwaendea Eddy Kenzo na Niniola kutoka Nigeria.
Facebook Diamond aliandika hivi:
''Ningependa niwashukuru na niwajuze kuwa kipenzi chenu jana nimeshinda tuzo tatu...nyimbo bora ya Afrika- #Utanipenda ,msanii bora wa muziki wa Afro Pop na Msanii bora wa Afrika mashariki''.
Ifuatayo ni orodha ya wasanii walioshinda tuzo za Afrimma:
1. Msanii bora wa kiume Afrika mashariki - Diamond Platnumz (Tanzania)
2. Msanii bora wa kike Afrika mashariki - Cindy Sanyu (Uganda)
3. Mwanamuziki bora wa Kiume Afrika Kusini - Black Coffee (Afrika Kusini)
4. Mwanamuziki bora wa Kike Afrika Kusini - Sally Boss Madam (Namibia)
5. Mwanamuziki bora wa kiume Afrika ya Kati - Wax Dey (Cameroon)
6. Mwanamuziki bora wa kike Afrika ya Kati - Bruna Tatiana (Angola)
7.Mwanamuziki bora wa kiume Afrika Kaskazini - DJ Van (Morocco)
8. Mwanamuziki bora wa kike Afrika Kaskazini - Zina Daoudia (Morocco)
9. Mwanamuziki bora wa kiume Afrika Magharibi - Flavour (Nigeria)
10. Mwanamuziki bora wa kike Afrika Magharibi - Olamide (Nigeria)
11. Mwanamuziki wa Kike mwenye ushawishi mkubwa - Naomi Achu (Cameroon)
12. Msanii bora wa bendi ya /Dou/GroupBand Afrika- Flavour (Nigeria)
13. Msanii anayeinukia vizuri zaidi - Amine Aub (Morocco)
14. Msanii anayependwa na mashabiki kote Afrika - Phyno (Nigeria)
15. Mtunzi wa Mwaka - Unique (Uganda)
16. Tuzo maalum ya utambulizi - King Sunny Ade (Nigeria)
17. Msanii bora /Duo/Group African Hiphop- Stanley Enow (Cameroon)
18. Msanii bora wa muziki wa rege na Dancehall - Patoranking (Nigeria)
19. Msanii bora wa muziki wa Utamaduni Afrika - Zeynab (Benin)
20. Msanii bora wa African Electro -Such (Zimbabwe)
21. Msanii bora wa Afrika katika RnB - Henok na Mehari Brothers (Ethiopia)
22. Msanii bora wa Afrika Muziki wa Rock -M'vula (Angola)
23. Msanii bora muziki wa muziki wa Jazz Afrika - Jimmy Dludlu (South Africa)
24. Kundi bora la muziki Afrika -VVIP (Ghana)
25. Kolabo bora Afrika - Mbilo Mbilo by Eddy Kenzo (Uganda) ft Niniola (Nigeria)
26. Video ya mwaka - Dogo Yaro by VVIP (Ghana)
27. Mwanamuziki Chipukizi wa Mwaka - Falz (Nigeria)
28. Albamu ya mwaka - Ahmed Soultan (Morocco)
29. Wimbo wa mwaka - Utanipenda Diamond Platnumz (Tanzania)
30. Msanii bora wa mwaka -Wizkid (Nigeria)