Sunday, September 4, 2016

MAMA TERESA ATAWAZWA NA PAPA FRANCIS KUWA MTAKATIFU.

Maelfu ya watu wameshuhudia ibada ya kutawazwa kuwa mtakatifu, ambapo Papa Francis amemtangaza mtawa Mama Teresa kuwa Mtakatifu.

Raia huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka 1997 alianzisha shirika la hisani la kimisionari ili kuwasaidia walala hoi katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.

Atajulikana kuwa Mtakatifu Teresa wa Calcutta.

Waandishi wanasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis kuhusu kanisa linalojulikana kwa kuwasaidia watu maskini.

Lakini wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu wagonjwa, na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu maskini wa kabila la Hindu huko India kuwa wakristo.


WACHEZAJI 25 WANAOCHEZA EPL KUTOKA AFRIKA.

Ligi ya Uingereza imetoa orodha rasmi ya wachezaji 25 wa msimu wa mwaka 2016/17.

Kila klabu katika ligi hiyo kuna mchezaji wa kiafrika.

Timu ya Senegal ndio yenye idadi kubwa ya wachezaji wake katika ligi hiyo ikiwa na wanane;

Cheikhou Kouyate (Westham United)

Diafra Sakho (Westham United)

Pape Souare (Crystal Palace)

Idrissa Gana (Everton)

Oumar Niasse (Everton)

Sadio Mane (Liverpool)

Mame Biram Diouf (Stoke City)

Papi Djilobodji (Sunderland)

Ikifuatiwa na Ivory Coast yenye wachezaji Sita, Nigeria ikiwa na wachezaji watano, Algeria wachezaji wanne huku Ghana ikiwa na watatu.


DARAJA LINALOELEA LA ZHANGJIAJIE LIMEFUNGWA.

Daraja la vioo lililojengwa juu huko China lililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 zilizopita limefungwa.

Maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo ijumaa ambapo tarehe ya kufunguliwa itatangazwa.

Lakini kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daraja hilo linaloelea, limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake.

Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea  na daraja halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.


VIJANA 7,170 WALIOPITIA JKT WAAJIRIWA.

Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Ally Mwinyi.

Vijana 7,170 waliojiunga kwa kujitolea katika jeshi la kujenga Taifa (JKT) wameajiriwa katika  vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa.

Waziri wa ulinzi na JKT, Dk. Hussein Ally Mwinyi amesema kuanzia mwaka huo JKT huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi na kuwajengea uzalendo.

Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na TBC, Dk. Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri toka uraiani bali vijana  waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa wakiajiriwa kwa mwaka.

Alisema pia kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kampuni binafsi za ulinzi.


MJANE AUAWA KWA KUNYOFOLEWA VIUNGO.

Mjane mwenye umri wa miaka 46, Veronica Dala ameuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na mapanga mwilini. Aidha mjane huyo amenyofolewa baadhi ya viungo vya mwili wake.

Tukio hilo limetokea asubuhi ya Septemba mosi mwaka huu katika kijiji cha Ilagaja kata ya Mangoye wilayani Nzega Mkoa wa Tabora baada ya wahalifu hao kuvamia nyumba ya mjane huyo kisha kuanza kumshambulia kwa mapanga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti majirani na ndugu wa mjane huyo walisema walipata taarifa ya kuwa ameuawa na watu wasiojulikana asubuhi ya tukio hilo.

Luhaga Jilala ambaye ni ndugu wa mjane huyo, alisema taarifa hizo alizipata asubuhi kuwa ndugu yake ameuawa. Hata hivyo chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Juma Seleli alisema tukio hilo ni la pili kutokea miaka kadhaa iliyopita alivamiwa na waharifu na kumjeruhi vibaya.

Alisema kijiji hicho kimejipanga kuhakikisha wanafanya doria za mara kwa mara ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi wa kijiji na wananchi wake.

Diwani wa kata hiyo, Henerico Kanoga alisema atahakikisha wananchi wanafanya uchunguzi kwa kupiga kura za maoni ili kuwapata watu wanaoshiriki kufanya uharifu huo wa kikatili.

Mwenyekiti wa ulinzi na usalama, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla alisema serikali ya Wilaya imepanga mipango ya mkakati wa kuhakikisha wananchi wanatoa ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza mauaji.

Alisema Wilaya ina mpango wa kuanza kupiga kura za maoni kwa wananchi ili kubaini wote wanaoshirikiana na waharifu hao na kuongeza kuwa mwananchi atakayetoa taarifa dhidi ya waharifu hao, siri zote zitatunzwa ili kulinda usalama wake.

Polisi mkoani Tabora imekiri mauaji hayo na kuahidi kufanya msako mkali kwa ajili ya kuwakamata na inawashikiria watu wawili kwa ajiri ya mahojiano.


MOVIE 10 KALI ZITAKAZOTOKA MWEZI HUU SEPTEMBA.

Kwa wapenzi wa kuangalia filamu, nakusogezea filamu kali zitakazotoka mwezi huu.