Monday, November 7, 2016

JEDWARI LA MSIMAMO WA LIGI YA EPL 2016/17.

MSIMAMO WA LIGI KUU.
NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Liverpool111626
2Chelsea111725
3Man City111524
4Arsenal111324
5Tottenham11921
6Man Utd11318
7Everton11218
8Watford11-415
9Burnley11-414
10Southampton11013
11West Brom11-313
12Stoke11-513
13Bournemouth11-312
14Leicester11-512
15Middlesbrough11-211
16Crystal Palace11-311
17West Ham11-911
18Hull11-1410
19Swansea11-115
20Sunderland11-125

TP MAZEMBE YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA.

Tp mazembe
Timu ya TP Mazembe ya Congo imetwaa ubingwa wa kombe la shirikisho barani Africa, baada ya kuichapa Mo Bejaia ya Algeria kwa 4-1 katika mchezo wa fainali ya pili.
Mabao mawili ya kiungo Rainford Kalaba na mengine ya Merveille Bope na Jonathan Bolingi yametosha kuipa TP Mazembe Ubingwa.
Sofiane Khadir aliifungia timu ya Algeria bao la kufutia machozi na kufanya matokeo ya jumla yawe 5-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Blida.
Mazembe sasa watamenyana na washindi wa Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kati ya Februari 17 na 19 mwakani kuwania taji la Super Cup ya CAF.

UCHAGUZI MKUU NCHINI MAREKANI NI KESHO, JE NANI ATASHINDA?

Clinton na Trump
CLINTON (Kushoto) NA TRUMP (Kulia).
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika hapo kesho kuchagua atakayemrithi Rais Barack Obama. Je, hali ikoje sasa na nani ana nafasi nzuri ya kushinda?
Mwandishi wa BBC wa Amerika Kaskazini Anthony Zurcher anachambua:
Leo Jumatatu ni siku nyingine ambayo wimbi la uungwaji mkono linatarajiwa kubadilika, hasa baada ya FBI kutangaza kwamba hawajapata ushahidi dhidi ya Bi Hillary Clinton baada ya kuchunguza barua pepe zilizopatikana hivi majuzi.
Bi Clinton anaendelea kuongoza dhidi ya mgombea wa Republican Donald Trump kwenye kura ya maoni ya kitaifa ya Washington Post/ABC, uongozi wake ukiwa alama tano. Kwenye kura ya maoni ya IBD/TPP, Bw Trump anaongoza kwa alama moja.
Hivyo, ni vigumu kubaini hali halisi kutoka kwa kura za maoni.
Aidha, kura zote za maoni ambazo zimefanywa kufikia sasa hazikuzingatia habari za karibuni zaidi za FBI kumuondolewa Bi Clinton makosa.
Lakini kunaweza kukatokea jambo la kuwashangaza watu?
Ukitazama kura za maoni katika majimbo muhimu, kunaonekana kuwa na udhaifu kidogo kwenye ngome ya Clinton.
Hii inaweza kuwa ndiyo sababu Bw Trump anatumia muda mwingi sana kwenye kampeni majimbo ya Michigan, Wisconsin na New Hampshire.
New Hampshire, ni moja ya majimbo ambayo yameonekana kuunga mkono chama cha Democratic kwa dhati miezi ya karibuni, lakini sasa jimbo hilo linaonekana kushindaniwa sana. Si ajabu kwamba Bi Clinton na Rais Barack Obama wamepanga mikutano ya dakika za mwisho kuimarisha uungwaji mkono.
Na katika jimbo la Michigan, ambapo Obama alishinda kwa kuwa mbele alama 10 mwaka 2012, mambo hayaonekani kuwa salama sana kwa Democratic.
Lakini kuna habari njema kwa Bi Clinton kutoka Ohio, ambapo utafiti wa maoni uliofanywa na kampuni ya kuaminika unamuonesha akiwa mbele kwa alama moja (hata hivyo, alama hiyo moja bado imo eneo la makosa yanayoweza kutokea kwenye utafiti).
Ikizingatiwa kwamba upigaji kura za mapema unaonyesha watu wengi weusi, ambao ni wengi kiasi eneo hilo, hawajajitokeza sana, Bi Clinton amefika huko siku za karibuni kufanya kampeni.
Alihudhuria tamasha ya muziki ya rapa Jay-Z na nyota wa muziki wa pop Beyonce siku ya Ijumaa kisha akahudhuria hafla ya pamoja na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James Jumapili.
Ushindi wa Clinton Ohio unaweza kuimarisha sana nafasi yake kushinda, kwa hivyo ishara za matumaini - baada ya kura kadha za maoni awali kuonyesha alikuwa nyuma ya Trump - ni habari njema.
Bi Clinton atafurahia hali jimbo la Nevada, ambapo kumekuwepo na foleni ndefu za wapiga kura wa mapema, ishara kwamba watu wa asili ya Hispania (Latino/Mexico) wamejitokeza kwa wingi.
Kwa jumla, ana nafasi nzuri ya kushinda ukimlinganisha na mpinzani wake lakini lolote linaweza kutokea.
Kwa mujibu wa:
  • New York Times Upshot: Clinton ana uwezekano wa 84% kushinda
  • FiveThirtyEight: Clinton ana uwezekano wa 65% kushinda
  • HuffPost: Clinton ana uwezekano wa 98% kushinda

SIMBA CHALII, YANGA WANACHEKA.

WACHEZAJI WA YANGA WAKISHANGILIA.
Simba jana ilionja joto ya kufungwa kwenye Ligi Kuu bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa African Lyon katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Wakati Simba ikionja joto hiyo, mtani wake wa jadi, Yanga ilichanua kwa ushindi wa bao 1-0 ugenini uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Prisons huku Azam ikikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, iliichukua dakika ya 90 Lyon kupata ushindi huo dhidi ya vinara wa ligi, Simba kwa bao lililofungwa na Abdullah Msuhi aliyeunganisha pasi ya Raizan Hafidh kabla ya kuujaza mpira wavuni. Simba ilikuwa ikishambulia muda wote wa mchezo huo huku Lyon iliyocheza mchezo wa kujihami zaidi ikishambulia kwa kushtukiza.
Katika dakika ya 38, Lyon walifanya mashambulizi kupitia kwa mchezaji wake Miraji Selemani, lakini mpira wake wa adhabu aliopiga uligonga mwamba na kutoka nje. Janvier Bukungu nusura aipatie Simba bao katika dakika ya 48 lakini shuti lake lilipaa juu.
Laudit Mavugo nusura afunge katika dakika ya 60 lakini akiwa kwenye nafasi nzuri mpira wake unawahiwa na mabeki wa Lyon na kuuondosha eneo la hatari. Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi zake 35.
Kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya, shujaa wa mabingwa watetezi Yanga, alikuwa Simon Msuva aliyefunga bao la mkwaju wa penalti katika dakika ya 74. Mwamuzi wa mchezo huo alitoa penalti hiyo baada ya mchezaji wa Yanga, Obrey Chirwa kuchezewa vibaya katika eneo la hatari.
Awali, Prisons ilipata penalti kipa wa Yanga, Beno Kakolanya akaokoa mkwaju huo na hivyo kuiacha timu ikiwa salama. Yanga sasa imeendelea kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 30, tofauti ya pointi tano dhidi ya vinara Simba.
Mshindi wa pili wa msimu uliopita, Azam bado imeendelea kupata matokeo ya homa za vipindi baada ya jana kuchapwa na Mbao Fc mabao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Matokeo hayo yanaifanya Azam ibaki na pointi 22 huku Mbao ikifikisha pointi 16.


Mbao iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 30 likifungwa na Venance Ludovick aliyeunganisha pande la Boniphace Maganga kabla ya kuujaza mpira wavuni. Dakika ya 50 Maganga aliifungia Mbao bao la pili na dakika ya 67 Francesco Sekumbawira aliifungia Azam bao la kufutia machozi.

MAKONDA KUJENGA VITUO 20 VYA POLISI JIJINI DAR.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA.
Mkoa wa Dar es Salaam unatarajia kujenga vituo vikubwa vya Polisi 20 ili kuimarisha ulinzi, pamoja na kuondoa changamoto ya ubovu wa vituo kwa vilivyopo, ambayo imegeuka kero kwa askari na wananchi wa mkoa huo wanaovitumia.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda wakati alipofanya ziara katika vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika mkoa huo.
Makonda alisema vituo vyote vinatarajia kutumia Sh bilioni 10 hadi kukamilika na kila kimoja kitakuwa na uwezo wa kuwa na askari 100.
“Najua serikali haikuwa na bajeti hii na hatuwezi kusubiri bajeti huku wananchi na askari wetu wakiteseka, mkoa huu una wadau wengi wenye uwezo na wanapenda kuona hali ya ulinzi ikiwa shwari, hivyo naamini tutajenga na tutafanikiwa,” alisema Makonda.
Alisema uwepo wa vituo hivyo utasaidia kuondoa changamoto ya wizi wa silaha zilizokuwa zikuibwa na majambazi waliokuwa wakivamia vituo na kuwaua askari.
“Tunategemea kila wilaya itakuwa na vituo vinne vya kisasa vitakavyokuwa na sehemu nzuri kwa ajili ya kuhifadhi silaha, askari wetu hawatakutana tena na changamoto ya kuuawa na kuibiwa silaha,” aliongeza.
Aidha, Makonda alitoa mwito kwa wananchi kushirikiana kuwafichua wezi wanaotumia pikipiki, majambazi na wauza dawa za kulevya ili wachukuliwe hatua za kisheria na Dar es Salaam ibaki kuwa safi.
“Hatuwezi kuwaachia polisi wenyewe lazima na sisi wananchi tushiriki kutoa taarifa Polisi, naamini kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu na mkoa utakuwa shwari hata ukisahau simu mahali na ukarudi ukaikuta,” alisema.

LORI NA NOAH USO KWA USO NA KUUA WATU 18.

MULIRO JUMANNE.
Watu 18 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika kijiji cha Nsalala Mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo iliyohusisha gari ndogo aina ya Toyota Noah na lori la mizigo ilitokea juzi saa 1:30 usiku baada ya dereva wa Toyota Noah iliyokuwa ikitoka Nzega kwenda Tinde mkoani Tabora, Seif Mohamed (32), kujaribu kuyapita magari mengine na kugonga uso kwa uso na lori lililokuwa likiendeshwa na Aloyce Kavishe, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne alisema polisi inawashikilia madereva wote wawili kwa mahojiano na hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya upelelezi kukamilika.

TANZIA: SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA HUKO UJERUMANI AKIWA KWENYE MATIBABU.

Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.

Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo.

‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu,alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima.

Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.

Sitta alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo Mashariki.

Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.

Alikuwa miongoni mwa wanachama zaidi ya 42 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.
Magufuli atuma salamu

Rais John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge, Job Ndugai kufuatia kifo cha Sitta alikokuwa akipatiwa matibabu.

Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sitta kilichotokea katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.

“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.

“Kupitia kwako Mheshimiwa Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

Dk Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.

“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni”

WASHINDI WA TUZO ZA MTV EMA.


Tuzo za MTV Europe Awards 2016 ‘MTV EMA’ zimefanyika usiku wa kuamkia leo November 7 2016, washindi wa tuzo hizo ni;
BEST SONG
Adele – “Hello”
Justin Bieber – “Sorry” — WINNER
Lukas Graham – “7 Years”
Mike Posner – “I Took A Pill In Ibiza (Seeb Remix)”
Rihanna ft. Drake – “Work”
BEST VIDEO
Beyoncé – “Formation”
Coldplay – “Up&Up”
Kanye West – “Famous”
Tame Impala – “The Less I Know the Better”
The Weeknd ft. Daft Punk – “Starboy” — WINNER
BEST FEMALE
Adele
Beyoncé
Lady Gaga — WINNER
Rihanna
Sia
BEST MALE
Calvin Harris
Drake
Justin Bieber
Shawn Mendes — WINNER
The Weeknd
BEST LIVE
Adele
Beyoncé
Coldplay
Green Day
Twenty One Pilots — WINNER
BEST NEW
Bebe Rexha
DNCE
Lukas Graham
The Chainsmokers
Zara Larsson — WINNER
BEST POP
Ariana Grande
Fifth Harmony  — WINNER
Justin Bieber
Rihanna
Selena Gomez
Shawn Mendes
BEST ROCK
Coldplay — WINNER
Green Day
Metallica
Muse
Red Hot Chili Peppers
BEST ALTERNATIVE
Kings of Leon
Radiohead
Tame Impala
The 1975
Twenty One Pilots — WINNER
BEST HIP HOP
Drake — WINNER
Future
G-Eazy
Kanye West
Wiz Khalifa
BEST ELECTRONIC
Afrojack
Calvin Harris
David Guetta
Major Lazer
Martin Garrix — WINNER
BEST PUSH
Alessia Cara
Anne-Marie
Bebe Rexha
Blossoms
Charlie Puth
DNCE — WINNER
Dua Lipa
Elle King
Halsey
Jack Garratt
Jonas Blue
Lukas Graham
BIGGEST FANS
Ariana Grande
Beyoncé
Justin Bieber — WINNER
Lady Gaga
Shawn Mendes
BEST WORLD STAGE
Duran Duran – Piazza Del Duomo, Milan (2015)
Ellie Goulding – Piazza Del Duomo, Milan (2015)
Jess Glynne – Isle of MTV, Malta (2016)
Martin Garrix – Isle of MTV, Malta (2015) — WINNER
One Republic – MTV Evolution, Philippines (2016)
Tinie Tempah  – MTV Crashes, Plymouth (2015)
Tomorrowland – Belgium (2016)
Wiz Khalifa – Isle of MTV, Malta (2016)
WORLDWIDE ACT WINNERS
Troye Sivan – Australia
Shawn Mendes – Canada
Maluma – Columbia
GOT7 – Korea
Wizkid  – Nigeria
Zara Larsson – Sweden
Ariana Grande – U.S.