Watu takribani 21 wafariki baada ya kutokea tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter katikati mwa Italia.
Watu wengine wengi wamefukiwa chini ya vifusi.
Wengi wamefariki katika kijiji cha Pescara del Tronto ambacho kimeharibiwa vibaya na inahofiwa kwamba idadi ya waliofariki inaweza ikaongezeka.
Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36)GMT, 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia katika kina cha 10km (maili 6) chini ya ardhi.
Taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi imesema USGS.
Mitetemeko ilisikika miji ya mbali kama vile Roma, Venice, Bologna na Naples. Mjini Roma baadhi ya majumba yalitikisika sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la Repubblica.
Mji wa Amatrice nao pia uliharibiwa vibaya. Watu wanne wanahofiwa kufariki katika mji jirani wa Accumoli.
Eneo hilo ambalo linapatikana katikati ya mikoa ya Umbria, Lazio na Marche ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia karibu na Perugia.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia za ulinzi wa nchi hiyo.
Meya wa mji wa Amatrice Sergio Perozzi ameambia kituo cha redio cha serikali cha RAI kwamba mji huo umeharibiwa vibaya.
Barabara za kuingia na kutoka mjini hazipitiki, nusu ya mji imeharibiwa, watu wamefukiwa chini ya vifusi. Kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja moja ambalo huenda likapolomoka.
Wednesday, August 24, 2016
TETEMEKO LA ARDHI ITALIA LASABABISHA VIFO VYA WATU 21.
UTAFITI: WANASAYANSI WAMEGUNDUA HILI KUHUSU MANUKATO.
Wanasayansi wamebaini kuwa kemikali zinazotengeneza manukato, zinaweza kuhama kutoka kwenye nguo ya mtu mmoja hadi mwingine, hata kama wamegusana kidogo.
Harufu ya manukato inaweza kubaki kwenye nguo kwa siku kadhaa, licha ya kwamba huisha baada ya mda.
Jopo la wanasayansi hao linasema huu ni ushahidi wa msingi wa utafiti, lakini wanasema kwamba manukato yana uwezekano mkubwa wa kutumiwa kupata ushahidi wa mharifu.
Katika taarifa yao waliyoiandika katika jarida la kisayansi na haki, watafiti hao wanasema walifanyia uchambuzi harufu za manukato zinazoweza kufaa katika visa ambako kumekuwa na mgusano wa karibu wa kimwili kama vile kesi za uharifu wa kingono.
Mkuu wa utafiti huo Simona Gherghel kutoka University Collage London, anasema "tulihisi kuna uwezekano mkubwa wa kutumiwa kwa manukato kwa sababu watu wengi ni watumiaji" tunafahamu 90% ya wanawake na 60% ya wanaume wanatumia manukato kila siku.
Wakati tunafahamu kuwa kazi kubwa katika Sayansi ya kutafuta ushahidi ulio hamishwa, hadi sasa haujawahi kufanyika utafiti kuhusu kuhamishwa manukato kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
UTAFITI
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE.
Rais Magufuli amemteua Modestus Kipilimba kuwa mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa Taifa (TISS) na Robert Msalika kuwa naibu wake.
Aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa idara hiyo George Madafa ameteuliwa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa badae.
Modestus Kipilimba ataapishwa leo jioni Ikulu.
Uteuzi bado unaendelea.
FIESTA YASABABISHA MUIMBAJI WA MZIKI WA KISINGELI MANIFONGO KUGOMBANA NA MKEWE.
Weekend iliyopita kulikuwa na tamasha kubwa la Fiesta lililofanyika jijini mwanza siku ya Jumamosi katika viwanja vya CCM Kirumba.
Mwanamziki mashuhuri wa nyimbo za visingeli Manifongo alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza katika tamasha hilo.
Balaa lilikuja pale Manifongo alipokuwa anatumbuiza nyimbo aliyoshirikishwa na msanii Shilole wimbo unaokwenda kwa jina la Mtoto mdogomdogo.
Manifongo alionekana kujiachia na kimshikilia Shilole. Ndipo mke wake alipata wasiwasi kutokana na show hiyo.
Manifongo alikuwa anakiambia kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, kuwa kwa sasa wameelewana kwa sababu ilibidi amueleweshe mke wake kuwa alikuwa kazini na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.
Vilevile Manifongo alitambulisha nyimbo yake mpya inayoitwa Tumtafute Kibaka.
BRUCE LEE ACHAGULIWA KUWA DIWANI AFRIKA KUSINI.
Baada ya Vasco da Gama kuwa spika wa baraza la mji wa Johannesburg nchini Afrika kusini, sasa Bruce Lee amechukua wadhifa katika baraza la Tshwane mjini humo.
Kwa wale waliokosa somo la historia, Vasco da Gama alikuwa baharia maarufu ambaye amerikodiwa kuwa mtu wa kwanza kusafiri makini kutoka Ulaya hadi India kupitia Cape of good hope.
Na muda mfupi badae orodha ya majina ya madiwani ilitolewa huko Tshwane nchini humo humo yalionesha Bruce Lee akiwa katika wadhifa wa maendeleo ya kiuchumi katika baraza hilo.
Bruce Lee ni mcheza filamu kutoka nchini Marekani.
RAYVANN WA WCB ASHINDWA KUJIZUIA NA KUANGUSHA KILIO CHA FURAHA.
Mwanamziki anayetokea katika lebo ya WCB Rayvan azawadiwa zawadi ya gari aina ya Rav4 katika siku yake ya kuzaliwa.
Raymond alikuwa anatimiza miaka kadhaa siku ya jumatatu na usiku wake kukawa na sherehe ndogo ya kumpongeza iliyofanyika nyumbani kwa Diamond Platnumz pande za Madale.
Lakini kundi la WCB walimfanyia surprise kubwa Raymond kwa kumzawadia gari aina ya Rav4, ndipo Raymond alishindwa kujizuia na kulia machozi ya furaha.
Raymond ni msanii chipukizi anayefanya vizuri katika tasnia ya bongo flava. Kwa sasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Natafuta kiki.
UZINDUZI WA TUZO ZA MTV MAMA 2016.
Tuzo za MTV Mama zitafanyika Octoba 22 kwenye mji mkuu wa Afrika kusini, Johannesburg.
Uzinduzi wa tuzo hizo umefanyika jumanne hii jijini humo mbele ya waandishi wa habari. Tuzo mbili zilizopita zilifanyika jijini Durban nchini humo.
Tuzo hizo zitatolewa katika ukumbi wa Ticket Pro Dome. Tarehe ya hafla ya kutajwa vipengele na washiriki wa tuzo za mwaka huu itatangazwa siku za usoni.
UTAFITI: JE WAJUA KUOSHA MDOMO NI DAWA YA KISONONO.
Kuosha mdomo kunasaidia kupunguza maambukizi ya kisonono, watafiti wanaamini.
Utafiti wa hivi majuzi umeonyesha kwamba binadamu wanaweza kubeba magonjwa ya zinaa katika koo zao kwa muda wa wiki moja au hata miezi bila ya kupata dalili zozote.
Na wanaweza kusambaza kwa wengine kupitia ngono isiyo salama ya mdomoni.
Wachunguzi wanajaribu kuona iwapo kuosha mdomo Mara kwa Mara kunaweza kusaidia kuzuia polepole na wataalamu wanasema kuwa ni wazo ambalo linafaa kutumiwa.