RIDHIWANI KIKWETE. |
Monday, November 21, 2016
RIDHIWANI:URAFIKI KATI YA BABA ANGU (KIKWETE) NA LOWASA BADO UPO.
Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ridhiwan Kikwete amesema urafiki kati ya baba yake na aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa bado upo na wanawasiliana kwenye simu mara kwa mara.
RAPPER CHEMICAL AKILI KUWA YEYE NI BIKRA.
Rapa wa Kike kiwango Bongo, Claudia ‘Chemical’ Lubao, amesema anashangaa kuona watu hawamuamini anaposema yeye hajawahi ‘Kuvunja amri ya sita’ tangu azaliwe.
Akiongea kupitia kipindi cha Kubamba cha Times Fm jana, Chemical amedai yeye anataka kuutunza ‘Usichana’ wake mpaka pale atakapoona inafaa. “Sijawahi kufanya Mapenzi hata siku moja, nmeachana na Mpenzi wangu kwa sababu hataki kusubiri nipo single sasa hivi. ” Sijui watu kwanini hawaamini wanahisi ni kitu ambacho hakiwezekani aisee”
WASHINDI WA TUZO ZA AMERICAN MUSIC AWARDS (AMAs).
ARTIST OF THE YEAR
Adele
Beyonce
Justin beiber
Drake
Selena GomezAriana Grande -- WINNER
Rihanna
Twenty one pilots
Carrie UnderwoodThe Weekend
NEW ARTIST OF THE YEAR UN-LEASHED BY T-MOBILE
Allesia Cara
The Chainsmokers
DNCE
Shawn mendes
ZAYN -- WINNER
COLLABORATION OF THE YEAR
The Chainsmokers Featuring Daya, “Don’t Let Me Down”
Drake Featuring Wizkid & Kyla, “One Dance”
Fifth Harmony Featuring Ty Dolla $ign, “Work From Home” -- WINNER
Rihanna Featuring Drake, “Work”
Meghan Trainor Featuring John Legend, “Like I’m Gonna Lose You”
TOUR OF THE YEAR
Beyoncé -- WINNER
Madonna
Bruce Springsteen & the E Street Band
VIDEO OF THE YEAR
Justin Bieber “Sorry” -- WINNER
Desiigner “Panda”
Rihanna Featuring Drake “Work”
FAVORITE MALE ARTIST – POP/ROCK
Justin Bieber -- WINNER
Drake
The Weeknd
FAVORITE FEMALE ARTIST – POP/ROCK
Adele
Selena Gomez -- WINNER
Rihanna
FAVORITE DUO OR GROUP – POP/ROCK
The Chainsmokers
DNCE
Twenty One Pilots -- WINNER
FAVORITE ALBUM – POP/ROCK
Adele, 25
Justin Bieber, Purpose -- WINNER
Drake, Views
FAVORITE SONG- POP/ROCK
Adele, “Hello”
Justin Bieber, “Love Yourself” -- WINNER
Drake Featuring Wizkid & Kyla, “One Dance”
FAVORITE MALE ARTIST – COUNTRY
Luke Bryan
Thomas Rhett
Blake Shelton -- WINNER
FAVORITE FEMALE ARTIST – COUNTRY
Kelsea Ballerini
Cam
Carrie Underwood -- WINNER
FAVORITE DUO or GROUP – COUNTRY
Florida Georgia Line -- WINNER
Old Dominion
Zac Brown Band
FAVORITE ALBUM - COUNTRY
Luke Bryan, Kill the Lights
Chris Stapleton, Traveller
Carrie Underwood, Storyteller -- WINNER
FAVORITE SONG - COUNTRY
Florida Georgia Line, “H.O.L.Y.”
Tim McGraw, “Humble And Kind” -- WINNER
Thomas Rhett, “Die A Happy Man”
Old Dominion
Zac Brown Band
FAVORITE ALBUM - COUNTRY
Luke Bryan, Kill the Lights
Chris Stapleton, Traveller
Carrie Underwood, Storyteller -- WINNER
FAVORITE SONG - COUNTRY
Florida Georgia Line, “H.O.L.Y.”
Tim McGraw, “Humble And Kind” -- WINNER
Thomas Rhett, “Die A Happy Man”
FAVORITE ARTIST – RAP/HIP-HOP
Drake -- WINNER
Fetty Wap
Future
FAVORITE ALBUM – RAP/HIP-HOP
Drake, Views -- WINNER
Drake & Future, What A Time To Be Alive
Fetty Wap, Fetty Wap
FAVORITE SONG – RAP/HIP-HOP
Desiigner, “Panda”
Drake, “Hotline Bling” -- WINNER
Fetty Wap, “679”
Drake -- WINNER
Fetty Wap
Future
FAVORITE ALBUM – RAP/HIP-HOP
Drake, Views -- WINNER
Drake & Future, What A Time To Be Alive
Fetty Wap, Fetty Wap
FAVORITE SONG – RAP/HIP-HOP
Desiigner, “Panda”
Drake, “Hotline Bling” -- WINNER
Fetty Wap, “679”
FAVORITE MALE ARTIST – SOUL/R&B
Chris Brown -- WINNER
Bryson Tiller
The Weeknd
FAVORITE FEMALE ARTIST – SOUL/R&B
Beyoncé
Janet Jackson
Rihanna -- WINNER
FAVORITE ALBUM – SOUL/R&B
Beyoncé, Lemonade
Rihanna, Anti -- WINNER
Bryson Tiller, T R A P S O U L
Chris Brown -- WINNER
Bryson Tiller
The Weeknd
FAVORITE FEMALE ARTIST – SOUL/R&B
Beyoncé
Janet Jackson
Rihanna -- WINNER
FAVORITE ALBUM – SOUL/R&B
Beyoncé, Lemonade
Rihanna, Anti -- WINNER
Bryson Tiller, T R A P S O U L
FAVORITE SONG – SOUL/R&B
Drake Featuring Wizkid & Kyla, “One Dance”
Rihanna Featuring Drake, “Work” -- WINNER
Bryson Tiller, “Don’t”
FAVORITE ARTIST - ALTERNATIVE ROCK
Coldplay
Twenty One Pilots -- WINNER
X Ambassadors
FAVORITE ARTIST - ADULT CONTEMPORARY
Adele -- WINNER
Rachel Platten
Meghan Trainor
Drake Featuring Wizkid & Kyla, “One Dance”
Rihanna Featuring Drake, “Work” -- WINNER
Bryson Tiller, “Don’t”
FAVORITE ARTIST - ALTERNATIVE ROCK
Coldplay
Twenty One Pilots -- WINNER
X Ambassadors
FAVORITE ARTIST - ADULT CONTEMPORARY
Adele -- WINNER
Rachel Platten
Meghan Trainor
FAVORITE ARTIST - LATIN
J Balvin
Enrique Iglesias -- WINNER
Nicky Jam
FAVORITE ARTIST - CONTEMPORARY INSPIRATIONAL
Lauren Daigle
Hillsong UNITED -- WINNER
Chris Tomlin
FAVORITE ARTIST - ELECTRONIC DANCE MUSIC (EDM)
The Chainsmokers -- WINNER
Calvin Harris
Major Lazer
TOP SOUNDTRACK
Purple Rain -- WINNER
Star Wars: The Force Awakens
Suicide Squad: The Album
J Balvin
Enrique Iglesias -- WINNER
Nicky Jam
FAVORITE ARTIST - CONTEMPORARY INSPIRATIONAL
Lauren Daigle
Hillsong UNITED -- WINNER
Chris Tomlin
FAVORITE ARTIST - ELECTRONIC DANCE MUSIC (EDM)
The Chainsmokers -- WINNER
Calvin Harris
Major Lazer
TOP SOUNDTRACK
Purple Rain -- WINNER
Star Wars: The Force Awakens
Suicide Squad: The Album
HAT-TRICK YA RONALDO YAILAZA ATLETICO MADRID.
CRISTIANO RONALDO. |
Nyota Cristiano Ronaldo amerudi kwa kasi akifumania nyavu kwa kishindo, baada ya kufunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha Real Madrid kuilaza Atletico Madrid kwa 3-0 katika uwanja wa Vicente Calderon kuamkia leo.
Kwa mantiki hiyo, Madrid imejiimarisha kileleni kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya mahasimu wao Barcelona, ambayo awali ililazimishwa sare ya bila kufungana na Malaga.
Zikiwa zimecheza michezo sawa, Real Madrid inaongoza baada ya kujikusanyia pointi 30, ikifuatiwa na Barcelona yenye alama 26 huku Atletico Madrid ikisalia na pointi 24.
Ronaldo alianza kutikisa nyavu katika dakika ya 23 baada ya kupiga mkwaju wa adhabu na kuwababatiza mabeki wa Atletico. Alizidi kuwapa furaha mashabiki wa Madrid baada ya kufunga kwa njia ya penalti dakika ya 71 kabla ya kukamilisha hat-trick katika dakika ya 77, baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na winga mwenye mbio, Gareth Bale.
WALALA NA MAITI CHUMBA KIMOJA.
MKUU WA WILAYA YA GEITA, HERMAN KAPUFI. |
Kituo cha Afya Katoro kilichopo Wilaya ya Geita mkoani hapa kinakabiliwa na uhaba wa majengo la kulazimu kulaza wagonjwa na maiti kwenye wodi moja.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Peter Janga alisema mgonjwa anapofariki hulazimika kumuacha kitandani hadi ndugu zake wafike kuchukua mwili na kama hana ndugu, huagiza gari kutoka hospitali ya mkoa kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa huko.
“Tunalazimika kuwachanganya kwa sababu hatuna chumba kingine cha kuwalaza, tunachokifanya kama mgonjwa akifariki tunaweka godoro chini na kuulaza mwili hapo,” alisema Dk Janga.
Alisema mbali na ukosefu wa jengo la kuhifadhia maiti na wodi, wanakabiliwa na uhaba wa vitanda.
“Tatizo hilo linatulazimisha kuwalaza wagonjwa wawili wawili kwenye kitanda kimoja.
MBEYA CITY YAWAPA ONYO YANGA.
Uongozi wa klabu ya Mbeya City umetoa onyo kwa Yanga kuhusu kuwasajili wachezaji wake Raphael Daud na Kenny Ally ambao bado inawahitaji.
Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Habari wa timu hiyo, Dismas Ten alisema wanazionya timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, hasa Yanga kuhusu kuwasajili wachezaji wake, ambao hawajamaliza mikataba yao.
“Sisi hakuna mchezaji ambaye kamaliza mkataba, wote ni mali yetu, hivyo tunashangaa kuhusu kiungo wetu Raphael Daud na nahodha Kenny Ally kuhusishwa na kujiunga na Yanga, kiukweli hizo taarifa hatuzijui ila kama Yanga wanawataka hao wachezaji walete barua rasmi,” alisema Ten.
Ten alisema kuwa endapo timu yoyote itawasajili wachezaji hao bila ya uongozi kujua, sheria zitachukua mkondo wake, lakini pia hawawezi kumzuia mchezaji kuondoka ila wanachotaka taratibu zifuatwe.
Kiungo Daud amefunga mabao manne kwenye mzunguko wa kwanza na yupo kwenye kiwango kizuri na nahodha Ally naye ni mchezaji muhimu katika nafasi ya kiungo mkabaji. Pia Ten alisema usajili wao wa wachezaji watakaoachwa na watakaosajiliwa kwenye dirisha dogo, utatolewa rasmi Novemba 30.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Novemba 15, ambapo timu zinazoshiriki Ligi Kuu ziko katika mawindo ya wachezaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza Desemba 17.
Wakati huo huo, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche amesema kwamba hajazungumza na Simba wala Yanga kuhusu mpango wa usajili.
Mchezaji huyo wa Al Suwaiq ya Oman, alikaririwa na mtandao mmoja wa kijamii akisema kuwa hajawahi kufanya mawasiliano na klabu hizo na hiyo ndio kawaida yao kuzusha mambo. Lakini Kipre Tchetche amewataka Simba na Yanga waache porojo kwenye vyombo vya habari na kama kweli wanamtaka wawasiliane naye.
MPAKA VIATU RANGI WA NIGERIA ANAYEJULIKANA SANA KULIKO WATU MAARUFU.
Idris, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 21, amekuwa akipaka viatu rangi kwa muda wa miaka mitatu sasa.
Huwa anazunguka mitaa ya mji wa Abuja akiwatafuta wateja ambao wangependa viatu vyao kushonwa au kupakwa rangi.
Idris hana kisomo lakini hajutii hilo. Anasema kuwa hupata karibu dola 5 kwa siku na kuongeza kuwa kipato chake cha mwezi mzima ni cha juu kuwaliko cha wafanyakazi wengine wa umma, ambao mishahara yao ni kati ya dola 125 na 190.
Ndoto ya Idris ni kumiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza rangi ya viatu, lakini kwa sasa ameamua kuwa mpaka viatu rangi kwenye mitaa ya mji wa Abuja.
WATU 100 WAMEFARIKI NA WENGINE KUPATA MAJERAHA KATIKA AJALI YA TRENI INDIA.
Idadi ya watu waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India, imeongezeka na kupita watu 100 na kuwajeruhi mamia ya wengine.
Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.
Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.
Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)