Tuesday, October 18, 2016

RAIS MAGUFULI AMETENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI LEO.

October 17 2016 iliripotiwa taarifa iliyomhusu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo ambapo ilisema kuwa Mkurugenzi huyo amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Mororgoro kwa mashtaka sita, likiwamo la kutishia kuua.
Sasa leo October 18 2016 taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kwamba Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga Emmanuel Mkumbo. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Mkumbo utafanywa baadaye.
Hata hivyo taarifa hiyo ya Ikulu haijaeleza sababu ya utenguzi huo.

MAMBO SABA USIYOWEZA KUFANYA NCHINI ETHIOPIA.

1. Mitandao ya kijamii
Wanaharakati wametumia simu zao kusambaza taarifa kuhusu maandamano yao
Hakuna ruhusa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, kuwasiliana na serikali inayowaita "vikosi vya nje". Jaribio lolote la kuwasiliana na "makundi ya kigaidi na makundi yanayopinga amani yanayotajwa kuwa ya kigaidi" ni marufuku.
Waandamanaji wametuma ujumbe na video walizo rekodi kwa simu zao katika mitandao ya kijamii na mitandao inayoendeshwa na raia wa Ethiopia walio katika nchi za nje.
Serikali imezishutumu Eritrea na Misri kwa kuchochea maandamano hayo.
2. Vyombo vya habari
Huwezi kutazama vituo vya Esat na OMN vya televisheni, vilivyo na makao yake nje ya nchi. Serikali imezitaja kumilikiwa na 'makundi ya kigaidi'.
3. Maandamano
Kumeshuhudiwa maandamano katika miezi ya hivi karibuni
Huwezi kupanga mandamano shuleni au katika chuo kikuu unakosoma, na hakuna ruhusa ya kuwa mfuasi wa kampeni ya kisiasa ambayo huenda 'ikazusha ghasia, chuki, na ukosefu wa imani miongoni mwa raia'.
4. Ishara
Mwanariadha Feyisa Lilesa alikunja mikono hewani katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu - ishara ya maandamano ya Oromo inayotambulika kote duniani
Huwezi kuonyesha ishara ya kisiasa, kama kukunja mikono juu ya kichwa au kuwasilisha ujumbe wa kisiasa kwa umma 'bila ya ruhusa'.
Ishara hiyo ya kukunja mikono imetumika pakubwa katika maandamano ya Oromo na pia katika mashindano ya Olimpiki Rio de Janeiro mnamo Agosti.
5. Marufuku ya kutotoka nje
Viwanda vimelengwa katika maandamano Ethiopia
Huwezi kutembelea kiwanda, shamba au taasisi ya serikali kati ya saa kumi na mbili jioni hadi kumi na mbili alfajiri. Ukikiuka marufuku ya kutotoka nje, 'vikosi vya sheria vimeagizwa kuchukua hatua zipasazo'.
6. Wanadiplomasia
Gari la kidiplomasia
Kama wewe ni mwanadiplomasia hauruhusiwi kusafiri zaidi ya kilomita 40 kutoka mji mkuu Addis Ababa, bila ya ruhusa. Serikali inasema ni kwa usalama wako.
Kwa jumla hakujatolewa tamko lolote kidiplomasia kuhusu hali ya tahadhari ilioidhinishwa.
7. Bunduki
Kama unamiliki bunduki, huwezi kuibeba kufikia kilomita 25 za barabara kuu za mji mkuu Addis Ababa, na kufikia kilomita 50 za mipaka ya nchi hata kama una kibali cha umiliki.

JUX AELEZA SABABU ZA DIAMOND KUTOMPOST.

'Kiukweli niongee ukweli ni kwamba sijawahi kumtumia cover ya wimbo wangu wala yeye hajawahi kunitumia cover ya wimbo wake mimi uwa nina list ya watu kadhaa kwenye simu yangu kuna baadhi ya wasanii ambao nipo nao karibu ninawatumia kwahiyo Diamond sijawahi kumtumia na kulalamika kwamba apost kazi zangu’ Aliongea Jux.
‘Mara ngapi umeona post moja inajirudi zaidi ya mara 10 au  mara 20 yaani sio vitu ambavyo fulani ajakupost  basi ndio ukasirike naomba kusema sijawahi kufanya hivyo na kwa upande wangu mtu anapostahili kupostiwa basi nitampost kwani huyo mtu anahitaji kupewa pongezi kafanya kitu fulani’ Alimaliza kwa kusema hayo.
source: millardayo.com

MTANGAZAJI ALIYEMHOJI TRUMP AFUTWA KAZI.

Billy Bush
Shirika la utangazaji la NBC nchini Marekani limemfuta kazi mtangazaji Billy Bush ambaye amekuwa akiendesha kipindi cha Today.
Mgombea urais wa chama cha Republican alikuwa anahojiwa na Bw Bush miaka kumi iliyopita alipotoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake.
Ukanda wa mahojiano hayo yaliyofanyika mwaka 2005 ulifichuliwa majuzi na gazeti la Washington Post.
Baada ya kufichuliwa kwa ukanda huo, viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican walijitenga na Bw Trump ambayo yamezua utata.
Kwenye video hiyo, Bw Bush anasikika akicheka baada ya matamshi ya Bw Trump.
Billy Bush, 45, ambaye ni mpwa wa rais wa zamani George H W Bush, alikuwa awali amesimamishwa kazi baada ya kufichuliwa kwa video hiyo.
Amekuwa mtangazaji wa kipindi cha Today kwa miezi miwili pekee.
"Ingawa alikuwa mgeni tu katika waandaaji wa kipindi cha Today, amekuwa na NBC kwa muda mrefu. Tunamtakia kila la heri," shirika la NBC limesema kupitia taarifa.
Mke wa Donald Trump, Melania, amemshutumu Bw Bush akisema alimchochea mumewe kusema mambo mabaya kuwahusu wanawake.
Bw Bush mwenyewe aliomba radhi tarehe 7 Oktoba akisema binafsi pia aliaibishwa na tabia yake alipokuwa akifanya mahojiano hayo.

MWIMBAJI WA BENDI YA AKUDO IMPACT KUFANYA KOLABO NA DAVIDO.

Image result for tarsis masela
Mwimbaji wa bendi kutoka Akudo Impact,  Taasisi Masela ambae kwasasa yupo katika maandalizi ya kutoa single zake ikiwemo matarajio ya kuwepo kwa collabo yake na msanii wa Nigeria Davido.
Kuhusu collabo yangu na Davido ndiyo ipo tulikutana congo wakati nilipoenda kusheherekea miaka 30 yangu na bahati nzuri Davido nilishawahi kusafiri  nae kwenye ndege moja basi tukabadilisha mawasiliano yeye alikuwa akielekea London mimi naelekea Dubai
Kwahiyo basi mazungumzo yetu yalikuwa na marefu sana nikazungumza nae kuhusu collabo yangu na yeye akanimbia kwa kipindi hiki yuko busy sana tukapanga kuanzia mwakani itabidi niende Nigeria kukamilisha collabo hiyo’

YOUNG KILLER AKANA TUHUMA ZA KUMPIGIA MAGOTI MONAGANGSTAR.

Kama utakuwa unakumbuka wiki zilizopita kumekuwa na headlines zikisema kwamba msanii wa Hip Hop, Young Killer alimpigia magoti  Monaganstar huku akimtaka wamalize tofauti zake.
''Hilo suala la mimi kwenda kumuomba msamaha sio la kweli ilikuwa ni ishu nyingine tu na nilikwenda kumuona kuhusu na kile kilichokuwa kinaandikwa katika mitandao mbalimbali’'.
Sio kuhusiana na kazi ni masuala binafsi, tofauti yangu na Mona nadhani ni mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi ndio yalipelekea kuwa hivyo nilikuwa kwake ndani ya miaka miwili na ni mfumo ambao tulikubaliana wote wawili’

MUME WA MARY J BRIGE ATAKWA ALIPWE BAADA YA TALAKA.

Mary J. Blige's  husband Martin 'Kendu' Issacs is demanding $130,000 in monthly spousal support so that he can continue to live the 'lavish' life he enjoyed before she filed for divorce

Mume wa Mary J. Blige, anataka awe analipwa $130,000 (zaidi ya shilingi milioni 286) kila mwezi ili zimsaidie kuendelea kuishi maisha ya kifahari aliyokuwa akiyafurahia kabla ya MJB hajaomba talaka.

Martin 'Kendu' Issacs, 49, anaamini kuwa mwanamuziki huyo wa R&B anapaswa kumsaidia kulipia gharama za mazoezi, mpishi binafsi na posho ya $1,000 kwaajili ya kununua nguo mpya.

Blige, 45, aliomba talaka kwa Issacs July, akisema ni kutokana na tofauti zisizosuluhishika baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miama 13. Pia alimtimua kama meneja wake na kumwacha bila chanzo cha kuingiza pesa.

Katika malalamiko yake kortini, Isaacs anadai alikuwa akiingiza $46,204 kila mwezi alipokuwa ameajiriwa na mkewe na kuingiza jumla ya $554,465 mwaka jana kama meneja wake.

Blige alimpa Issacs $35,000 mwezi August na $50,000 September kama fedha za kujikimu (spousal support) pamoja na $25,000 kulipa wanasheria.

Kwenye nyaraka zake, Issacs anadai ameshazitumbua fedha hizo kwakuwa bado hajapata mahali pa kuishi na kwamba akaunti yake ya benki -$13,104.

Isaacs anataka pia apewe $5,000 ambazo huwalipa wazazi wake kila mwezi na $71,000 za kodi anazodaiwa! "Issacs also pays nearly $5,000 a month in support for two children from a past relationship, $2,500 on auto expenses and transportation, $5,708 in maintenance and repair on his properties and another $5,732 on groceries.
He has also asked for help in paying the $21,677 he gives in charitable donations and the $10,000 he spends on entertainment, gifts and vacations," wameandika Mail Online.

MAKAMBA AMWAGA ZAWADI KILOMBERO KWA UTUNZAJI MAZINGIRA.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Mh January Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya Saruji kwa kijiji cha Katurukila, tarafa ya Mang'ula, wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ikiwa na kutambua mchango wao mkubwa katika utunzaji wa mazingira hasa eneo la Msitu wa Magombera pamoja na kuwapa wananchi motisha zaidi ya kuendelea na utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Waziri Makamba aliye katika ziara mahsusi ya kutembelea, kutambua na kushughulikia changamoto zilizopo kwenye mazingira amepokea taarifa fupi ya hali ya msitu wa Magombera kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilombero Bwana Dennis Londo pamoja na kuzungumza na wananchi pamoja na viongozi wa kijiji cha Katurukula ambao ni watunzaji wakubwa wa msitu huo kwa kushirikiana na taasisi husika za serikali.

10 WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI LINDI.


Watu 10 wamekufa na wengine 44 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Kampuni ya Barcelona lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Newala mkoani Mtwara jana.

Ajali hiyo ni ya jana saa 5 asubuhi katika kijiji cha Miteja wilayani Kilwa mkoani Lindi, umbali wa kilometa 30 kutoka mkoa wa Pwani na miongoni mwa waliopoteza maisha wamo watoto wadogo watatu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga akizungumza jana, alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva ambaye bado wameshindwa kumhoji kwa kuwa ni miongoni mwa majeruhi na mpaka jana jioni alikuwa amepoteza fahamu. “Ni kweli ajali imetokea asubuhi saa tano leo (jana), dereva alikuwa katika mwendo kasi, basi likapasuka tairi la mbele, likapinduka. Majeruhi wapo 44 na waliokufa ni 10, wanawake sita na mwanamume mmoja, mtoto wa kike mmoja na wakiume wawili,” alisema Kamanda Mzinga.

Kamanda Mzinga alilitaja basi hilo kuwa ni lenye namba za usajili T110 CUU Youtong, mali ya Kampuni ya Barcelona.

ATCL YATOA OFA KWA ABIRIA WA MWANZA.



Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ofa ya mwezi moja kwa abiria wanaosafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kulipa nauli ya Sh 160,000 kwa safari moja.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Ofisa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Lily Fungamtama wakati akizungumza na Idara ya Habari (MAELEZO).
Fungamtama alisema ndege za kampuni hiyo, zimeanza kutoa huduma kuanzia Jumamosi iliyopita, kama ilivyobainisha kupitia vyombo vya habari.
Safari hizo zilianza kwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuelekea nchini Comoro, na hapa nchini inatoa safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Kigoma.
Alisema kwa kuanzia walianza na mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wa ndani ya ndege, na hatimaye walianza safari za biashara ya kusafirisha abiria Oktoba 15, mwaka huu kama ilivyopangwa.
Aliongeza kuwa ATCL imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja wake ofa ya kubeba kilo 20 za mizigo na kilo saba za mzigo wa mkononi bure pamoja na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani ya mwezi.
Alikanusha taarifa potofu kuwa zimekwama kuanza safari zilizopangwa. Alisema habari hizo sio za kweli, kwani hivi sasa wameshaanza huduma katika mikoa hiyo mitatu.
ATCL kwa sasa ina ndege tatu, zikiwemo mbili aina ya Bombadier Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, na Dash8-Q300 yenye uwezo wa kubeba abiria 50.

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WATU KUAGA MWILI WA MASABURI.



Rais John Magufuli jana aliongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika kuaga mwili wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Massaburi aliyefariki Alhamisi iliyopita kwa ugonjwa wa ini.
Dk Magufuli aliwaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk Massaburi (56) kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam, na alipopewa nafasi ya kuzungumza, alisisitiza familia za marehemu kuishi kwa kushikamana.
“Nawaombeni familia mkashikamane, shetani hujitokeza wakati wa msiba, watoto mumtangulize Mungu, baba aliwapenda wote na hakuwabagua, watoto mkishikamana na mama zenu pia watashikamana. Naomba mtoto mkubwa ukawe nguzo ya familia ili pawe na umoja na Mungu atawasimamia,” alisema Dk Magufuli ambaye alisema anachofahamu marehemu ameacha wake wanne hadi watano na watoto zaidi ya 20.
Akisoma wasifu, kaka wa marehemu, Machabe Massaburi alisema Didas alizaliwa mwaka 1960 Serengeti mkoani Mara akiwa mtoto wa 10 katika familia ya John Massaburi.
Alisema Dk Massaburi amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Kivukoni na Meya wa Jiji la Dar es Salaam kuanzia 2010 hadi 2015 na pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na hadi mauti yanamfika alikuwa Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Chuo chake cha ugavi IPS kilichopo Chanika.
Alisema marehemu ameacha wajane, watoto, wajukuu kadhaa na kwamba alifunga ndoa na Janeth Massaburi ambaye ni Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu.
Dk Magufuli alisema alimfahamu Dk Massaburi kama mpiganaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mengi aliyafanya wakati akiwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na akaongeza kuwa historia yake haiwezi kufutika katika siasa za Tanzania.
Tukio hilo la kuaga lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kutoa heshima za mwisho akiwemo Rais mstaafu Jakaya Kikwete na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Viongozi wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Makamu wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Mohamed Gharib Bilal, Mama Salma Kikwete, viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, mawaziri mbalimbali, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Dk Charles Tizeba alisema wamepoteza rafiki, ndugu na mtu waliyemtegemea zaidi katika uendeshaji wa jumuiya hiyo.
Alitoa mwito kwa familia kuwa kifo hicho, kisiwe chanzo cha ugomvi na mifarakano na kwamba waimarishe umoja.
Msemaji wa Familia, Otieno Igogo alisema kifo hicho ni pigo kubwa na kimekuja katika wakati mgumu kwa kuwa Dk Massaburi amefariki dunia wiki moja na kaka yake, na hakuweza kulifahamu hilo kwa kuwa alikuwa taabani.
Alisema aliacha wosia wa maneno kuwa pindi akifariki, azikwe katika mji wake ulioko Chanika, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, na kwamba zisifuatwe mila za kabila la Wajaluo kuwa hawazikwi ugenini.
Baada ya kuaga mwili wa marehemu, ulipelekwa katika mji wake eneo la Chanika kwa ajili ya maziko kama alivyowausia mwanasiasa huyo.

WALIOIBA MAKONTENA BANDARINI WAJISALIMISHA.



Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema tayari baadhi ya watu waliotorosha makontena bandarini bila kukaguliwa, wameitikia agizo lake la kuwataka kujisalimisha na kufanyika ukaguzi ili kujiridhisha bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo.
Mwishoni mwa wiki, Mwijage alitoa siku nne kwa wafanyabiashara ambao wanadaiwa kutorosha makontena 100 bandarini, wajisalimishe Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili yakaguliwe. Ili kutekeleza agizo hilo waziri huyo aliweka dawati la dharura kutoa huduma hiyo katika siku za mapumziko.
Alisema wafanyabiashara ambao wangekaidi agizo hilo, wangechukuliwa hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kulipa faini ya asilimia 15. Ukaguzi huo ulitakiwa kufanywa na TBS kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC). Lengo la ukaguzi huo ni kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini na ubora wake.
Alisema kuna wafanyabiashara wanaleta makontena yana nguo, ambazo zina kiwango cha chini na wengine hawalipi kodi, wengine wanaleta vilainishi vya magari wakati hapa nchini, pia kuna kiwanda cha kuzalisha vilainishi hivyo, hivyo kuruhusu makontena kupita bila kukaguliwa ni kuua viwanda vya ndani.
Aidha, alisema anaipenda sana kazi yake ya uwaziri, ndio maana analazimika kufanya kazi za chini, ambazo zingefanywa na ofisa wa kawaida wa Shirika la Viwango (TBS).
Akizungumza jana wakati wa kuzindua Sensa ya Uzalishaji Viwandani ya Mwaka 2013, Mwijage alisema ili asiondolewe kwenye wadhifa huo na aliyemteua (Rais John Magufuli), ni lazima afanye kazi hata ya kukagua makontena kwani anafanya hivyo kwa lengo la kulinda viwanda vya ndani.
“Aliyenipa kazi hii tajiri namba moja, ameniagiza nifanye hivyo, ndio maana naenda hadi mitaani kukagua makontena kazi ambayo ingefanywa na ofisa wa kawaida wa TBS,” alisema Mwijage na kutamba kwamba kazi yake hiyo imezaa matunda.
Alisema licha ya kuwepo baadhi ya watu kumkebehi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu hatua yake ya kwenda mitaani kukagua makontena, alisema hatishiki kwani yeye kazi yake ya kwanza kuifanya ilikuwa ni ya ukaguzi na hivyo anaifahamu vyema kazi hiyo.
“Nawaambia hivi nitaendelea kwenda kukagua makontena, niacheni nifanye kazi yangu, acheni kuniandika kwenye mitandao,” alisema Mwijage.
Aliongeza “Nilianza kazi nikiwa navaa khaki wakati nafanya kazi hiyo ya ukaguzi, licha ya kuwa leo hii mimi ni waziri, ndio maana niliwaambia wafanyakazi wa TBS wasiwe na haraka ya kupanda vyeo, nani angejua mvaa kaki angepanda hadi kuwa waziri.”
Alisema kuna bidhaa zinatoka nje zikiwa hafifu na hazina ubora, zinaingizwa nchini na kubandikwa lebo ya bandia.
“Kwa mfano kuna tomato zinatoka nje hazina ubora, lakini wanaweka lebo ya bandia, sasa tusipokagua kontena hizi zinaonekana ni bidhaa za maana kuliko tomato za nyanya za Morogoro ambazo zina ubora wa asili.
“Natoa mwito kwa Watanzania kununua bidhaa zinazozalishwa nchini kwani zina ubora kuliko bidhaa zinazotoka nje. Tunataka waje na ukaguzi ufanyike kwa usahihi ili kujua ubora wao, na sisi tutaendelea kunadi tomato yetu ya hapa nchini na matokeo tukutane huko sokoni,” alisema.
Alisisitiza kuwa yeye pamoja na wizara yake wataendelea kufuatilia kila kontena linaloingizwa nchini ili kujua ubora wa bidhaa pamoja na ulipaji wa kodi.
Alisema hana nia mbaya na wafanyabiashara ila anachowataka ni kutaka wafanye biashara katika uwanja sawa wa kibiashara.
Pia alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha kwamba hawaleti nchini bidhaa, ambazo zinatengenezwa na viwanda ambavyo vimeajiri watu wengi nchini.
Alisema kuruhusu kuleta bidhaa hizo nchini ni kuua viwanda vya ndani na matokeo yake ndio kunazalishwa vijana wahalifu, kama wale wa kundi la Panya Road.

LIVERPOOL 0 - 0 MANCHESTER UNITED

Mchezo wa kusisimua wa ligi kuu ya soka England umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Katika mchezo huo kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu huku kipindi cha pili Liverpool ikishambulia zaidi lango la United.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa hakukasirika lakini pia hakufurahishwa na kiwango cha uchezaji wa timu yake.
Klopp pia ameisifu safu ya ulinzi ya Man U na kusema ilikuwa vigumu kushinda kutokana na ulinzi ulivyokuwa imara.
Philippe Coutinho akiachia mkwaju mbele ya wachezaji wa Man u
Kwa upande wake meneja wa Man U Jose Mourinho amesema licha ya kutopata matokeo aliyoyataka lakini ameridhishwa na matokeo hayo.
Amesema si matokeo mabaya kwani waliweza kumzuia hasimu wao wa jadi kuondoka na alama tatu nyumbani kwake.
Katika mchezo huo Ander Herrera aliibuka kuwa mchezaji bora huku akiwa mchezaji aliyegusa mpira mara nyingi kuliko mchezaji yoyote , aligusa mpira mara tisini

MKE WA DONALD TRUMP AMTETEA MUMEWE.

Melania Trump
Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump, Melania, amesema wanawake wanaomtuhumu mumewe kwa kuwadhalilisha kingono ni wanasema uongo, na kusisitiza kwamba Bw Trump ni "mwanamume mstaarabu".
Amesema hata hivyo kwamba matamshi ambayo Bw Donald Trump aliyatoa kwenye kanda ya video ya mwaka 2005 kuhusu wanawake hayakubalini, ingawa amesema hayaonyeshi mwanamume ambaye yeye amemfahamu.
Mgombea huyo wa chama cha Republican ana makosa ya kushiriki "mazungumzo ya wavulana faraghani" lakini alichochewa na mtangazaji wa runinga Billy Bush, Bi Trump amesema.
Kanda hiyo ya ivdoe iliwafanya viongozi wengi wakuu wa chama cha Republican kuacha kumuunga mkono.
Kwenye video hiyo, Bw Trump anaonekana akimwambua Bw Bush, ambaye alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Access Hollywood cha NBC, kwamba anaweza kujilazimisha kimapenzi kwa wanawake kwa sababu yeye ni nyota.
Tangu kutolewa kwa kanda hiyo, wanawake kadha wamejitokeza na kudai Bw Trump alidhalilisha kimapenzi, madai ambayo mgombea huyo amekanusha.
"Najua yeye huwaheshimu wanawake lakini anajitetea kwa sababu yanayosemwa ni uongo," Bi Trump amesema kwenye mahojiano na CNN.
"Namwamini mume wangu," amesema.
"Mume wangu ni mkarimu na mwanamume mstaarabu. Hawezi kufanya hayo."
Amedai kashta hiyo "imepangwa na kuandaliwa ili kumzuia kushinda" na kundi la kampeni la mpinzani wake Hillary Clinton na wanahabari.
"Kwa maelezo waliyopata (wanahabari) hawafanyi uchunguzi zaidi kuhusu wanawake hawa? Hawana maelezo ya kweli," ameongeza.
Akiongea kwa mara ya kwanza tangu madai hayo kutokea, Bi Trump amesema mumewe hajawahi kuwadhalilisha wanawake.
Utathmini wa kura za maoni kufikia 17 Oktoba, 2016.
Anasema mara kwa mara wanawake walimwendea mumewe mbele yake wakitaka awape namba yake ya simu kwa njia isiyofaa.
Akiongea kuhusu kanda hiyo ya mwaka 2005 ya Access Hollywood ambay ilitolewa kwa wanahabari siku 10 zilizopita, amesema: "Nilimwambia mume wangu, wajua, lugha uliyoitumia haikufaa. Haikubaliki."
"Na nilishangaa kwa sababu huyo si mwanamume ninayemfahamu."
Bi Trump anaamini Billy Bush, ambaye alifutwa kazi na NBC kuhusu kanda hiyo, ndiye wa kulaumiwa.
Bw Trump, alisema, "alihadaiwa, na kupotoshwa na mtangazaji huyo aseme mambo mabaya".
Zimesalia wiki tatu kabla ya uchaguzi na kura za maoni zinaonesha Bw Trump yuko nyuma mpinzani wake wa Democratic Hillary Clinton katika majimbo muhimu yanayoshindaniwa.