Monday, August 15, 2016

WEMA SEPETU AZUA UTATA INSTAGRAM



Masaa machache yaliyopita, msanii wa filamu Wema Abraham Sepetu aleta gumzo kwenye mtandao wa Instagram baada ya ku-post picha ya mastaa mbalimbali wakiwemo Jamal wa kwenye movie ya empire, Alikiba, Cyril Kamikaze, Diamond platnumz, Trey songz, Korede bello na wengine kama picha inavyoonesha hapo juu.

Mashabiki wamjia juu baada ya kutokumuweka anayesemekana ni mpenzi wake Idris Sultan.

Wengine wadai kuwa Wema na Idris wamegombana so Wema kapanick na kuamua kuwa-post hao mastaa na kuweka caption ya #MCM.

Mpaka sasa Wema hajaeleza sababu ya yeye kutomuweka Idris kwenye hiyo picha. Bado tunaendelea kutafuta undani wa hiyo habari.

Usiache kupitia burudaninaangie.blogspot.com kwa updates zote


MASANJA HATIMAYE AFUNGA NDOA.

Mchekeshaji maarufu wa kundi la Ze comedy show Masanja mkandamizaji afunga ndoa jumapili ya jana tarehe 14 August. Wiki kadhaa zilizopita Masanja alimvalisha Pete mke wake huyo na hatimaye jana afunga pingu za maisha.

Wasanii wengi wakihudhuria hiyo sherehe wakiwemo Ze comedy, Lulu Michael, Dr. Cheni, Mbasha na viongozi mbalimbali.


NAY WA MITEGO AMALIZANA NA BASATA.

Kama utakuwa unakumbuka 27, 7, 2016 Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) lilitoa tamko la kumfungia msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutojihusisha na kazi ya sanaa kwa muda usiojulikana

Sasa leo August 15, 2016 baraza hilo limetoa tamko rasmi la kumfungulia msanii huyo kufanya kazi ya muziki huku akiwa kwenye uangalizi maalum sehemu ya kuhakikisha anaendesha shughuli za sanaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na kuzingatia maadlili katika kazi zake.

Kwa mujibu wa Katibu mkuu wa BASATA Godfrey L. Mngereza aliyaongea haya>>>>Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 27/7/2016 Baraza lilimfungia Msanii Nay wa Mitego  kwa kipindi kisichojulikana na kumtaka kutekeleza maagizo yafuatayo:

1.Kuhakikisha amesajiliwa na kuwa na kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa

2.Kulipa faini ya Shilingi milioni moja (1,000,000/-)

3.Kuomba radhi watanzania kupitia mkutano wa waandishi wa habari na kwenye akaunti  zake za mitandao ya kijamii

4.Kuufanyia marekebisho wimbo wa ‘Pale Kati’ ili ubebe maudhui yenye maadili

Msanii huyo ametekeleza adhabu zote zilizotajwa hapo juu, hata hivyo pamoja na kuleta marekebisho mara mbili ya wimbo wa ‘Pale Kati’ Baraza bado halijaridhishwa na marekesho hayo hivyo linaendelea kuufungia wimbo huo hadi hapo litakapojiridhisha umekidhi vigezo vya kimaadili‘- Godfrey Mngereza

BASATA  limetoa agizo kwa msanii huyo kuendelea kuufanyia marekebisho wimbo wake huo kama bado atakuwa anauhitaji.

Source millardayo.com


DIRECTOR HANSCANA ATANGAZA KUACHANA NA WANENE ENTERTAINMENT





Director maarufu hapa nchini Hascana, ametangaza rasmi kuachana na Wanene na kuanza maisha yake mapya. Hanscana alisema hajagombana na uongozi wa wanene entertainment bali ameamua kuondoka ili aanzishe maisha yake mwenyewe, kwasababu amekuwa sasa (23).

Director huyo ameondoka na crew yake nzima ya videos department tangu tarehe 4 mwezi huu wa nane, kwasababu ya kutofautiana kimalengo kati ya Hanscana brand na wanene entertainment. Hanscana alisema ametumia juhudi kubwa sana kuipigania hiyo kampuni kama yake from zero to hero, mpaka kufikia kuwa moja ya kampuni kubwa ya videos hapa Afrika Mashariki.

Hascana alisema kuwa anahitaji kuwa na kampuni yake mwenyewe na hakuna ubaya kati yake na wanene entertainment.

  "Kitu ambacho nilikipigania mwenyewe     siwezi kukiongelea vibaya, hata kwa bahati mbaya".

Hanscana alimaliza kwa kusema, ameamua kuweka wazi jambo hilo kwasababu amekuwa alipigiwa simu sana na waandishi, bloggers.