Thursday, September 1, 2016

TANZANIA YAWEKA HISTORIA KWA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA.

Dr. Nurjan Jiwaj mtaalamu wa sayansi ya anga nchini Tanzania na mmoja wa waratibu wa tukio.

Wageni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya, pamoja na mwanasayansi wa anga wapo katika mji wa Rujewa mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa Tanzania, kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua kwa kiwango cha asilimia 97 kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya anga.


Tukio kama hilo hutokea baada ya miaka mingi, ambapo tukio la mwisho lilikuwa mwaka 1977.