Wednesday, October 26, 2016
WATOTO WAKISHUKA NA KUPANDA MILIMA NCHINI CHINA, KWENDA SHULE.
Katika milima ya jimbo la Sichuan kusini magharibi mwa China, kundi la watoto ambalo lilikuwa likishuka mita 800 kwenye mlima ili kufika shule huku wakitumia njia za asili ambazo ni ngazi za miti ambayo ni hatari sasa wanajengewa ngazi za chuma.
Ngazi hiyo ya chuma inayojengwa na wanakijiji itakuwa na mabomba 1,500 ya chuma na inatarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu, ujenzi wa ngazi hizo zenye gharama ya dola za marekani 150,000 ambazo ni karibu Tsh za kitanzania milioni 327, ilianza kujengwa na wanakijiji mwezi August mwaka huu.
Ngazi hiyo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi pia inatarajiwa itakuwa yenye usalama zaidi kwa hata wanakijiji wa kijiji hicho ambao watakuwa wanaitumia kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoishi. Siku za nyuma wanakijiji walikuwa wakitumia miti ya mizabibu ambayo ilikuwa mibovu.
JUSTIN TIMBERLAKE MATATANI KWA KUJIPIGA SELF KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA.
Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Justin Timberlake nusura ajipate taabani baada yake kupakia picha yake ya kujipiga kwenye mtandao wa Instagram.
Alikuwa amejipiga picha hiyo akipiga kura yake katika mji wa Memphis, Tennessee.
Yeye ni miongoni mwa mamilioni ya wapiga kura ambao wamekuwa wakipiga kura zao mapema.
Nyota huyo wa pop, ambaye pia ni mwigizaji, hakuwa anakumbuka kwamba jimbo la Tennessee lilipiga marufuku upigaji wa picha katika vitu vya kupigia kura mwaka jana.
Afisi ya mwanasheria mkuu wa eneo la Shelby ilikuwa awali imesema "imefahamishwa kuhusu uwezekano wa uvunjaji wa sheria za uchaguzi" na kwamba kisa hicho kilikuwa kinachunguzwa.
Lakini baadaye, mwanasheria huyo Amy Weirich alisema taarifa hiyo ya awali "haikuwa sahihi" na lilitolewa kwa umma bila yeye kufahamu.
"Niko nje ya mji kwa sasa nikihudhuria kongamano. Hakuna yeyote katika afisi yetu anayechunguza kisa hiki kwa sasa. Hatutatumia rasilimali zetu adimu kufuatilia suala hili," alisema Bi Weirich.
Timberlake ana wafuasi 37 milioni kwenye Instagram.
Iwapo angefunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria za uchaguzi, angehukumiwa kufungwa jela siku 30 au kupigwa faini $50 (£41), au apewe adhabu zote mbili.
Adam Ghassemi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Tennessee, amesema watu wanafaa kutumia simu zao kujisaidia katika kupiga kura pekee.
Ni kinyume cha sheria kupiga picha katika chumba cha kupigia kura katika majimbo 18 nchini Marekani kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Hata hivyo, katika majimbo 20 inakubaliwa.
Jumatatu, jaji mmoja wa mahakama ya dola aliunga mkono msimamo wa mwanamume mmoja kutoka Michigan kwamba sheria inayowazuia watu kupiga picha kura zao ambazo tayari wamezijaza na kuzisambaza picha hizo mitandaoni ni ukiukaji wa haki ya kikatiba ya kujieleza.
Jumatatu, wapiga kura wengine wawili jimbo la Colorado waliwasilisha kesi kortini kupinga sheria inayozuia watu kuonyesha karatasi za kura ambazo wamezijaza kwa watu wengine. Wanasema marufuku hiyo inakiuka katiba.
MAALIM SEIF: MARUFUKU KUHUTUBIA MISIKITINI.
Mgogoro wa kisiasa baina ya chama cha wananchi CUF na serikali ya Zanzibar unaendelea kufukuta licha ya jitihada zinazoendelea za kutatua mgogoro huo.
Hali hiyo imejitokeza baada ya katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kupigwa marufuku kuzungumza misikitini hatua ambayo imepingwa na baadhi ya vyama vya upinzani nchini Tanzania.
ALIYEKUWA BEKI WA BRAZIL CARLOS ALBERTO AFARIKI DUNIA.
Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72.
Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali.
Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.
Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)