Monday, January 16, 2017

FIFTH HARMONY KUTUMBUIZA KWA MARA YA KWANZA BILA CAMILA CABELLO.

Fifth Harmony, Instagram
FIFTH HARMONY.
Kundi la Fifth Harmony wapo tayari kuwaonyesha mashabiki kuwa wanaweza hata bila ya Camila Cabello ambaye alijitoa mwishoni mwa mwaka jana kwenye kundi hilo.

Kundi hilo litatumbuiza siku ya Jumamosi kwenye 2017 PEOPLE'S CHOICE AWARDS bila ya Camila.

PRIYANKA CHOPRA APATA MAJERAHA WAKATI WA KU-SHOOT SERIES YA QUANTICO.

PRIYANKA CHOPRA.

Priyanka Chopra tweeted, "Thank you for all of your warm thoughts and well wishes. I will be ok, and am looking forward to getting back to work as soon as I can. Much ♥."

Mcheza filamu Priyanka Chopra aliyepata umaarufu kwenye series ya QUANTICO amepata ajari wakati yupo kambini ana-shoot series hiyo.

Alipata majeraha hayo siku ya Alhamisi usiku na kulazwa hospitali. Lakini kwa sasa Priyanka ameruhusiwa kutokana na hali yake kuwa shwari na kuendelea vizuri.

MWANAMIEREKA JIMMY SNUKA AFARIKI DUNIA.

Jimmy Snuka
MAREHEMU, JIMMY SNUKA.
Mwanamiereka wa WWE,Jimmy Snuka maarufu kama 'Superfly' amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Wakili wake amesema mwanamiereka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida, akiwa pamoja na familia yake.
Mzaliwa huyo wa Fiji alikuwa wakati mwingi hospitalini kwa shida tofauti ikiwemo ugonjwa wa kiakili wa Dementia, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika
Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata 'mwanzilishi wa kitengo cha high flying' katika ukumbi wamiereka.
Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa miereka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, 'Nakupenda babangu' na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.
Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.
Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.
Mashtaka hayo waliwasilishwa mahakamani mwaka 2015.
Alikana madai hayo ya mauaji.
Nyota wa miereka wamekuwa wakituma risala za rambirambi kwa Snuka kwenye mitandao ya kijamii.