SALLAM SK. |
Friday, January 20, 2017
TAMASHA KUBWA LA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA.
Meneja wa Diamond Platnumz, fundi mitambo Sallam SK ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.
“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” alisema
QUEEN DARLEEN: SIJAWAHI KUTONGOZWA.
QUEEN DARLEEN. |
Queen alisema''kusema ukweli mimi sijawahi kutongozwa na mwanaume, kwa asilimia kubwa mimi ndio huwa nawtongoza wanaume.
SHAMSA FORD: WASANII WENGI HAWAOLEWI KWA SABABU WANATAKA WANAUME WENYE HELA.
SHAMSA FORD. |
Shamsa Ford alisema baada ya ndoa heshima kwa mumewe anayefahamika kwa jina la Chiddy Mapenzi iliongezeka na akaanza kumuogopa, kwa sababu kabla hajaolewa alikuwa anamchukulia poa tu.
Pia Shamsa alisema kuwa wasanii wengi wa kike wa bongo hawaolewi kwa sababu wanataka mwanaume ambaye amekamilika kwa kila kitu, wakati mwanaume anatengenezwa na mwanamke mwenyewe.
Shamsa alimaliza kwa kuwataja wasanii wa bongo movie anaowakubali ni Gabo na Rihama.
WASANII WATAKAO TUMBUIZA KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA TRUMP SIKU YA LEO.
JACKIE EVANCHO. |
SAM NA DAVE. |
RADIO CITY ROCKETTES. |
Radio City Rockettes pia watatumbuiza katika dansi hizo rasmi, ingawa hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya wanachama wa bendi hiyo.
Wengine watakaotumbuiza katika dansi hizo ni Tim Rushlow na bendi yake ya Big Band, Silhouettes, Pelican212, The Piano Guys, Circus 1903, Cache Olson, Lexi Walker na Erin Boheme.
PIA KUTAKUWA NA DANSI ZA WANAOMPINGA TRUMP. Kutakuwa na dansi mbadala - ambazo zinaitwa Dansi za Amani - ambazo zimeandaliwa na wanaharakati watetezi wa uhuru. Miongoni mwa watakaotumbuiza huko ni dadake Beyonce, Solange Knowles.
SOLANGE KNOWLES. |
KANYE WEST NI RAFIKI TU WA TRUMP LAKINI HATOTUMBUIZA KATIKA KUAPISHWA KWA RAIS HUYO.
TRUMP NA KANYE WEST. Kanye West hatatumbuiza wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump, waandalizi wa sherehe hiyo wamesema. Kumekuwa na uvumi kwamba tangu nyota huyo wa muziki alipowaambia watu kwamba angempigia Bw Trump kura iwapo angeshiriki uchaguzi, na kisha wakakutana Trump Tower, basi angekuwa mmoja wa wasanii ambao wangetumbuiza Ijumaa. Lakini Tom Barrack, mwenyekiti wa kamati andalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa rais, alisema kwamba sherehe hiyo si "ukumbi ufaao" kwa West. Alisema mwanamuziki huyo wa mtindo wa rap ni "jamaa mzuri" lakini "hatujamuomba atumbuize." Bw Barrack alisema: "Yeye hujichukulia kama rafiki wa rais mteule, lakini huu sio ukumbi wake. "Ukumbi ambao tunao, upande wa watumbuizaji, umejaa, uko sawa, utakuwa kimsingi wa nyimbo za kitamaduni za Marekani, na Kanye ni jamaa mzuri lakini hatujamuomba atumbuize. Tunaendelea na ajenda yetu." |
Subscribe to:
Posts (Atom)