Saturday, October 8, 2016

KIMBUNGA MATTHEW CHAUA WATU 800


Umoja wa mataifa umeonya kuwa huenda ikachukua siku kadhaa kwa athari kamili ya kimbunga Matthew kujulikana nchini Haiti wakati idadi ya waliokufa imeongezeka hadi 800.
Idadi hiyo imezidi mara mbili wakati maafisa wa uokozi wanafika katika maenoe ya kusini ambaye imekuwa vigumu kuyafikia kutokana na mvua kali.
Carlos Veloso wa Shirika la chakula duniani anasema miji iliyoathirika zaidi yanayweza kufikiwa kwa njia ya anga au majini pekee.
Vifo vingi Haiti vimetokea kusini magharibi mwa pwani ya eneo hilo, lililoathirika pakubwa na kimbunga hicho wiki iliyopita.
Kimbunga Matthew kimetua pwai mwa jimbo la Florida Marekani lakini kimepungua kasi na kuwa cha kiwango cha pili kikiwa na upepo wenye kasi ya kilomia 177 kwa saa.
Kimbunga cha kiwango cha tano ndicho kikali zaidi katika mizani ya Saffir-Simpson ya uzito wa vimbunga.
Image copyrightERSImage
Jitihada za kutafuta manusura zinaendelea kufutia kimbunga hicho kilicho kibaya kuwahi kushuhudiwa katika visiwa vya Caribbean katika muda wa muongo mmoja.
Shirika la ulinzi wa raia Haiti Ijumaa limesema idadi ya waliofariki imeongezeka mara mbili zaidi kutoka watu 400 hadi watu 800.
Maafisa wa uokozi wanasema wanatarajia kupata waathiriwa zaidi wanapokaribia maeneo ya mashinani.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la watoto katika mji wa Port-Au-Prince, Cornelia Walther, ameiambia BBC kwamba, kupatikana maji safi ni muhimu zaidi kwa sasa.

TRUMP AOMBA MSAMAHA KWA KUWATUKANA WANAWAKE.



                                  MGOMBEA KITI CHA URAIS MAREKANI DONALD TRUMP
Mgombea urais wa chama cha Republican Marekani, Donald Trump, ameomba msamaha kwa matamshi machafu aliyotoa kuhusu wanawake katika kanda ya video iliyozuka ya miaka 11 iliopita.
Katika kanda hiyo, Trump anasikika akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake sehemu zao za siri na kujaribi kushiriki ngono nao, anasema: 'unaweza kufanya chochote unapokuwa nyota'.
Maafisa wakuu wa chama cha Republican wameshutumu vikali matamshi yake akiwemo spika wa bunge, Paul Ryan, aliyesema amechafuzwa roho na matamshi hayo.
Mhariri wa BBC wa eneo la Amerika kaskazini anasema hiki ni kiwango cha mzozo katika azma ya Trump kuwania urais wa Marekani
Katika kanda iliyorekodiwa Trump aliomba radhi kwa kuonekana akisoma , na ameahidi kuwa mwanamume bora zaidi lakini amemshutumu Bill Clinton kwa kuwanyanyasa wanawake kingono.
Amemshutumu Hillary Clinton pia kwa kuwakandamiza na kuwaibisha waathiriwa wa unyanyasaji uliotekelezwa na mumewe.

VALENCIA AWATOROKA MAPOLISI.

enner_valencia-496713
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ecuador anayeichezea klabu ya Everton ya England kwa mkopo akitokea West Ham United Enner Valencia amerudi kwenye headlines baada ya kuwakwepa mapolisi waliokuwa wanasubiri mechi imalizike wa mkamate.
Valencia alifanikiwa kufanya hivyo  dakika ya 82 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 dhidi ya Chile mchezo ambao ulimalizika kwa Ecuadorkuondoka na ushindi wa goli 3-0, Valencia mwenye umri wa miaka 26 anakabiliwa na kesi ya kutakiwa kulipa dola 17000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 30 kama gharama za matunzo ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka mitano aliyezaa na mke wake wa zamani
Maafisa wa mahakama ambao wamejaribu kutaka kumkata Valencia kwa zaidi ya mara moja, safari hii aliwakimbia kwa staili ya kujifanya ameumia dakika ya 82 na kutolewa nje akiwa kawekewa mashine ya Oxygen na kukimbizwa katika ambulace na kuondolewa uwanjani haraka na mapolisi kushindwa kumtia nguvuni.

SERIKALI YAPINGA KUKODISHWA KWA YANGA.

                                                                  YUSUF MANJI.

Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imesema kuwa mkataba wa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kukodishwa klabu hiyo ni batili. Tamko hilo limetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja baada ya juzi kusambaa kwa taarifa ya mkataba wa Yanga katika mitandao ya kijamii.

Suala la Yanga kukodishwa timu lilianza mchakato tangu Manji aitishe mkutano mkuu wa dharura miezi miwili iliyopita, akiomba ridhaa ya wanachama wa klabu hiyo kumkodisha timu na nembo kwa miaka 10, ombi ambalo lilipitishwa na kurudishwa katika bodi ya wadhamini kwa ajili ya kufanyiwa kazi na juzi kupitishwa kwa makubaliano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiganja alisema wanaunga mkono suala la mabadiliko, lakini lazima yafuate sheria na taratibu zilizowekwa ili kukamilisha mabadiliko yoyote.

“Mimi sipingi klabu zetu kufanya mabadiliko isipokuwa najaribu kukumbusha zifuate utaratibu wa kisheria, kwa sababu unapobadilisha jina au kufanya marekebisho yoyote ni lazima vikasajiliwe na kutambulika,”alisema.

Kiganja alisema hata Bodi ya Yanga iliyohusika kuruhusu timu hiyo kukodishwa haitambuliki kwa Msajili, kwa vile wajumbe wake wengi ni wale waliochaguliwa kwa mpito. Alisema bodi ya wadhamini iliyoundwa Julai 5, 1973 ni wawili tu wanaotambulika waliopo hadi sasa ambao ni Jabir Katundu na Juma Mwambelo.

Lakini, Mwembelo amekuwa ahusishwi tena katika mambo yanayoendelea ya timu hiyo. Bodi ya mpito, ambayo Kiganja alisema hawakusajiliwa wala kupitishwa kwenye mkutano mkuu kutokana na taratibu ni George Mkuchika, Fatuma Karume, Francis Kifukwe, Amri Ramadhan, Juma Kambi na Abeid Mohamed.

Katibu huyo alifafanua taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili timu ikodishwe kuwa ni kutumia vikao, ambapo cha kwanza ikiwa ni Kamati ya Utendaji ya Klabu itakayochambua hoja na kukubaliana au kutokukubaliana kisha kupeleka katika kikao cha ngazi za juu.

Pia, alisema baadaye hoja inapelekwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wote uwe wa dharura au kawaida ili kujadiliana hoja husika, kisha baada ya kukubaliana au kutokukubaliana inapelekwa kwa Baraza la wadhamini lenye uwezo wa kuingia kwenye maamuzi makubwa, na mwisho inapelekwa kwa msajili.

“Kwa mujibu wa sheria ya BMT ya mwaka 1967 kifungu namba 11 (1) kinaeleza chama chochote kinachofanya mabadiliko ya jina, anuani, madhumuni au kifungu chochote cha Katiba yake kitatakiwa kipate idhini ya msajili,”alisema.

Alisema kifungu namba 11 (3) msajili anaweza kuyakataa maombi ya kubadili kifungu chochote cha katiba kama ataona kuwa mabadiliko yanaweza kuhatarisha usalama na kuvuruga amani, au kama kuna malengo ya kuwanufaisha wachache au kama hayazingatii sera za michezo na sheria za BMT.
Alisema baada ya hatua hizo kukamilika, inabidi kufanya marekebisho ya Katiba ambayo yatapitia kwenye taratibu za klabu, na ndipo klabu husika itakuwa imepata baraka za serikali.


Katibu huyo aliweka wazi kuwa amezungumza hayo kwa kuwa yeye ni kiongozi na mlezi wa vyama vya michezo nchini na kwamba, maelezo yake hayalengi kuwakatisha tamaa wale walionesha nia ya kuwekeza kwenye michezo bali kuwambushana mambo ya msingi kwa manufaa

MWANAMKE ALIYEMNYOFOA ULIMI KIJANA AFIKISHWA MAHAKAMANI.


Mwanamke anayedaiwa kumng'ata ulimi kijana Saidi Mnyambi (26) siku 28 zilizopita, kwa kile kilichodaiwa kutaka kufanya naye mapenzi kwa nguvu, hatimaye amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Singida.

Mwanamke huyo, Mwajabu Jumanne (36) mkazi wa eneo la Mandewa nje kidogo ya mji huu amefikishwa mbele ya Hakimu Flora Ndale akishitakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa kunyofoa theluthi moja ya ulimi wa kijana Mnyambi wakati wakipeana denda.

Wakili wa Serikali, Michael Ng'hoboko alidai mbele ya hakimu Ndale kuwa Septemba 12 mwaka huu majira ya saa 2.45 usiku katika eneo la Mandewa Manispaa ya Singida, kwa makusudi, mama huyo alimng'ata ulimi Mnyambi na kumsababishia jeraha na maumivu makali.

Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa mshitakiwa Mwajabu alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 cha Kanuni ya adhabu Sura ya 16 Sheria za nchi kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshitakiwa alikana kosa na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 itakapotajwa tena.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana ya watu wawili waliotoa ahadi ya Sh milioni moja kila mmoja