Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika WhatsApp, lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshatumwa na kupokewa.
Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu zenye mfumo endeshi wa iOS.
Katika hilo kutakuwa na program katika eneo la ‘Settings’, ambapo utatakiwa kue-‘Edit’ kisha ‘Revoke’ mchakato utakaowezesha kufuta ujumbe huo kwa wakati mara tu unapogundua umekosea.
Hata hivyo, kikubwa ni kuwa utaweza kufanya hivyo kama tu uliomfikia bado hajausoma, ikimaanisha iwapo ameshausoma hutaweza kuufuta.
Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.