Kampuni ya Mbowe Hotels Limited (MHL) imebakiza siku ya leo tu, kuwa tayari imelipa deni la shilingi Bilioni 1.3 ya kodi ambayo inadaiwa na shirika la nyumba la Taifa (NHC) ili kujinasua katika hatari ya kuondolewa katika jengo la shirika hilo lililopo katika makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Ghadhi Makunganya jijini Dar es salaam.
Jengo hilo ni maarufu kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za starehe na burudani kutokana na kuwepo kwa Club maarufu ya Billcanas.
Hatua hiyo inatokana na notisi mbili zilizotolewa; Moja na shirika la nyumba la Taifa Juni 24, mwaka huu ikitishia kuvunja makubaliano ya mkataba wa ukodishaji wa jengo hilo na kufuatia na notisi ya kampuni ya udalali ya mahakama ya fosters, ambazo zote zinakamilisha muda wake leo.
Kampuni hiyo inamilikiwa na mwenyekiti wa taifa wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Mbowe alinukuliwa na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki akilihusisha deni hilo na masuala ya kisiasa, kwa madai kuwa suala hilo linakuzwa na kupotoshwa ili kumnyamazisha katika harakati za kisiasa, bila kukiri uwepo wa shauri baina ya pande hizo mbili juu ya deni hilo.
Mkurugenzi mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu, alithibitisha kuwepo kwa mpango wa kuiondoa kwa nguvu kampuni ya Mbowe katika jengo hilo.
"Ni kweli kuwa tumempa mpangaji wetu huyo Mbowe notisi ya kumuondoa. Kampuni ya Hoteli za Mbowe ni miongoni mwa wateja wetu watatu ambao ni wadaiwa sugu wa kodi ya pango kwa wateja binafsi nchini" alisema.
Mchechu alisema suala hilo ni la kibiashara na halina mahusiano na masuala ya siasa, kama ilivyodaiwa na Mbowe hivi karibuni alipoongea na vyombo vya habari.
"NHC haina uhusiano na masuala ya kisiasa wala kujihusisha nayo, hatuna uhusiano wowote na masuala ya umoja wa kupambana na udikteta (UKUTA), namuomba Mbowe atambue kuwa hili ni suala la kibiashara na si vinginevyo" alisema Mchechu.
Hatua ya NHC ya kuandika notisi ya kuvunja mkataba, ilitokana na kampuni ya Mbowe kushindwa kujibu na kusaini hati mpya ya makubaliano ya namna ya ukodishaji wa jengo hilo uliowasilishwa kwa kampuni hiyo January 18, 2015.
Monday, August 29, 2016
KAMPUNI YA MBOWE IMEBAKIZA SIKU MOJA KULIPA BIL.1.3/-NHC.
LIST YA WALIOCHUKUA TUZO ZA MTV VIDEO MUSIC AWARDS.
Tuzo za MTV VMAs zilifanyika jana huko Marekani na wafuatao ni wasanii waliochukua tuzo hizo huku mwanadada Beyonce akiongoza kwa kuchukua tuzo 8;
VIDEO OF THE YEAR - Formation (Beyonce).
BEST MALE VIDEO - This is what you came for (Calvin Harris ft Rihanna).
BEST FEMALE VIDEO - Hold up (Beyonce).
BEST POP VIDEO - Formation (Beyonce).
BEST HIP HOP VIDEO - Hotline bring (Drake).
BEST ROCK VIDEO - Heathens (Twenty one pilots).
BEST ELECTRONIC VIDEO - How deep is your love (Calvin Harris & Discipline).
BEST COLLABORATION VIDEO - Work from home (Fifth harmony ft Ty Dolla $ign).
BEST NEW ARTIST - D.N.C.E
BEST BREAKTHROUGH LONGFORM VIDEO - Lemonade (Beyonce).
BEST DIRECTION - Formation (Beyonce).
BEST VISUAL EFFECTS - Up & up (Cold play).
BEST ART DIRECTION - Black star (David Bowie).
BEST EDITING - Formation (Beyonce).
BEST CINEMATOGRAPHY - Formation (Beyonce).
BEST CHOREOGRAPHY - Formation (Beyonce).
SONG OF SUMMER - All in my head (flex) (Fifth harmony).
YANGA YANG'ARA TENA.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu bara, yanga jana kuanza vizuri kampeni zao kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Afrikan Lyon katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Yanga imeanza kutetea taji lake baada ya kutupwa nje ya michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa na TP mazembe ya Congo DR mabao 3-1 katika mechi ya mwisho ya makundi.
Ikicheza soka safi Yanga ilichukua dakika 19 kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Deus Kaseke baada ya kuunganisha pasi safi ya Simon Msuva.
Afrikan Lyon ambayo ni mechi ya kwanza ilitoka sare 1-1 na mechi ya Azam, jana ilizidiwa karibu kila idara na kuonekana kuchoka hasa katika kipindi cha pili.
Msuva aliiandikia Yanga bao la pili katika dakika ya 59 akiunganisha pasi ya Haruna Niyonzima kabla ya kumpiga chenga kipa wa Lyon na kuujaza mpira wavuni.
Pamoja na kuelemewa huko, Lyon walijitahidi kufanya mashambulizi ambapo katika dakika ya 76 Tito Okello alishindwa kumalizia krosi akiwa amebaki peke yake na kipa.
Yanga iliendeleza mashambulizi na dakika ya 90 Amisi Tambwe alikosa bao baada ya mpira wa kichwa aliopiga kugonga mwamba na mpira kurudi uwanjani.
Zikiwa zimebaki sekunde chache mpira kumalizika, Juma Mahadhi aliyeingia uwanjani kuchukua nafasi ya Msuva aliandika bao la tatu kwa Yanga baaa ya kazi nzuri ya Niyonzima.
Yanga itacheza mechi ya pili keshokutwa ambapo itaminyana na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo wa Taifa.
Kutoka kwenye uwanja wa CCM kirumba Mwanza, Alexander Sanga anaripoti kuwa wenyeji Toto Africans wameshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya city.
Wageni Mbeya City waliandika bao hilo katika dakika ya tano lililofungwa na Haruna Shamte kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja golini.