Saturday, November 5, 2016

HITIMISHO LA BURUDANI FIESTA JIJINI DAR.

Image result for TIGO FIESTA

Lile tamasha la Fiesta lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wakazi wa Dar es salaam limewadia. Ni siku ya leo tarehe 5 Nov, Jumamosi 2016, litafanyika katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa kumi na mbili jioni.

KIINGILIO:
18,000/= Ukilipa kwa TigoPesa
20,000/= Ukilipa kawaida
25,000/= Ukilipa cash mlangoni

tigo-fiesta

WASANII WATAKAO KUWEPO:
TEKNO, YEMI ALADE, JOSE CHAMELEON huku wakisindikizwa na wasanii wa ndani;

  • Vanessa
  • Belle9
  • Benpol
  • Darasa
  • Weusi
  • Juma nature
  • Jux
  • Chege
  • Tunda man
  • Shilole
  • Manfongo
  • Barnaba
  • Alikiba
  • Raymond
  • Hamadai
  • Maua sama
  • Mr. Blue
  • Nandy
  • Young D
  • Baraka da prince
  • Billnass
  • Christian Bella
  • Dogo janja
  • Fid Q
  • Jay Moe
  • Stamina
  • Sholo mwamba
  • Msami
  • Roma
  • Lord Eyes


MBILIKIMO WASHIRIKI MITINDO.

wakipita-jukwaani
MBILIKIMO KATIKA MASHINDANO.
Wanawake wafupi warembo wameweza kuvunja mtazamo wa miaka mingi kuwa urembo na au uanamitindo ni kwa warefu, wenye miguu mirefu na wembamba pekee.
Ni kupitia maonesho ya mitindo ya mavazi yanayopigiwa chapuo na taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo la Onesho la Kimataifa la Mitindo la Mbilikimo.
Taasisi hiyo, inayoitwa Onesho la Taifa la Mitindo la Mbilikimo ilianzishwa mwaka mwaka 2014 mjini New York Marekani baada ya kuona changamoto zinazowakabili mbilikimo.
Tayari imechochea kufanyika kwa mashindano ya mitindo ya mavazi kwa mbilikimo katika miji ya New York, Paris, Berlin na hivi karibuni mjini Tokyo Japan.
Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali hulenga kuinua uelewa na mwamko kuhusu umbilikimo.
Huwashirikisha katika maonesho hayo kufuatia changamoto zinazowakabili kupata mavazi yanayowafiti.
Kubwa zaidi kuliko yote maonesho haya huendesha kampeni za kubadili mtazamo wa jamii kuhusu tasnia nzima ya urembo kwa ujumla wake na vigezo vya aina ya washiriki.
Hivi karibuni mjini Tokyo, Japan wanawake mbilikimo sita waliweza kushiriki onesho la kimataifa la mitindo kwa mbilikimo.
Picha zikionesha warembo hao wakipingana na dhana kuwa urembo ni kwa ajili ya warefu pekee wakiwa wamependeza na mavazi yao wakati wakitembea kwa miondoko ya kipaka huko Ebisu, zilivutia hadhila. Ni onesho la mavazi lililofana mno.
Hivyo, waliweza kuonesha kwamba wanamitindo wanaweza kutokana na maumbo na saizi yoyote ile kuliko inavyofikiriwa sasa.
Kwa kawaida wanamitindo wanafahamika  kuchaguliwa wakiwa na vigezo vya urefu si chini ya mita 1.30.
Na washiriki hawa ‘twiga’ kutoka duniani kote husafirishwa katika madaraja ya juu ya ndege na kuwekwa katika hoteli za kifahari kwa kushiriki maonesho hayo.
Hali kama hizo zinazowafanya wahusudiwe huwafanya wanawake wengine kuhesabiwa hawana sifa na au si warembo.
Kitendo hicho huwaathiri wengine kisaikolojia au hujikuta wakiingia katika mkumbo wa kujitengeneza miili yao kwa kupandikiza plastiki, kitu ambacho kinafahamika ni hatari kwa afya.
Shoo hii ya Japan inafanyika kwa mwaka wa tatu ikiwa tayari imefanyika katika miji ya Paris na New York kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Katika onesho la mwaka jana mjini Paris, ambalo liliandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya serikali kusaidia kuhamasisha viwango mbadala vya urembo katika tasnia hiyo inayopendelea warefu na wembamba.
Lilifanyika baada ya waandaaji kuishutumu vikali tasnia ya urembo nchini humo kwa kubagua wanawake wengine.
Wanawake mbilikimo 15 wenye urefu wa futi nne walishiriki kwa mavazi tofauti tofauti ya kisasa yaliyobuniwa na wabunifu maarufu mjini humo.

CLINTON AMTUHUMU TRUMP KUMTUMIA WAHUNI KUMZOMEA.

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton
HILLARY CLINTON.
Mgombea urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton, jana uzalendo ulimshinda na kuwakemea waandamanaji waliokuwa wakimzomea katika mkutano wake wa kampeni, huku akimtuhumu hasimu wake, Donald Trump kuwatuma.
Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyosomeka ‘Bill Clinton ni mbakaji’ katika jimbo la Florida, walimpa usumbufu mkubwa mgombea huyo wakati akihutubia kutokana na kelele na maneno waliyokuwa wanayatoa.
Akiwa kwenye mkutano huo wa hadhara, Clinton alionyesha waziwazi kukerwa na kitendo cha waandamanaji hao na kumshutumu Trump kufadhili vitendo visivyo vya kiungwana katika kampeni.
“Nimechoshwa na vitendo vya giza na uchokozi vinavyotoa picha mbaya ambavyo vinafanywa na wafuasi wanaomuunga mkono Donald Trump,” alisema Clinton kwa sauti yenye hasira.

MAGUFULI: YANGA NA SIMBA MWIKO KUTUMIA UWANJA WA TAIFA.

Rais John Magufuli akiwa na msanii nguli wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto, Ikulu, Dar es Salaam baada ya Rais kuzungumza na wahariri na waandishi wa habari jana. (Picha na Mroki Mroki).
RAIS MAGUFULI AKIWA NA MRISHO MPOTO, JANA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amepigilia msumari wa mwisho kwa timu za Simba na Yanga na kuzitaka zifute ndoto za kutumia Uwanja wa Taifa.
Rais Magufuli alisema jana Ikulu Dar es Salaam, katika mkutano wake na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari na kudai kuwa anapenda kwenda uwanjani kuangalia mpira, lakini anashindwa kufanya hivyo kutokana na fujo ambazo zimekuwa zikizuka kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
“Natamani kwenda Ndondo Cup kuangalia kuliko kwenda kuangalia timu ambazo wanashindana Uwanja wa Taifa, wakishindwa wanang’oa viti,”alisema Rais Magufuli na kuongeza: “Nimefurahi uamuzi wa Waziri (Nape) kufungia uwanja, ni lazima kujenga nidhamu, uwanja umejengwa kwa gharama kubwa, huwezi kung’oa viti, Ndondo ni bora kuliko hizo timu kubwa,”alisema.
Kauli ya Magufuli imekuja ikiwa ni siku za kadhaa baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuzifungia kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana timu za Simba na Yanga kutokana na mashabiki wa timu hizo kung’oa viti katika mechi ya Ligi iliyofanyika Oktoba mosi na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Hata hivyo, vurugu kubwa ziliibuka kabla na baada ya mchezo huo ambao kabla ya mchezo mashine za tiketi za elektroniki zilishindwa kufanya kazi na kusababisha mlundikano kwenye mageti upande wa lango la Yanga na mashabiki kukosa uvumilivu na kuvunja mageti hayo.
Vurugu nyingine kubwa ilizuka dakika ya 26 ya mchezo baada ya mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe kuifungia timu yake bao, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua utata, huku wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele, hata hivyo Mkude alikuja kufutiwa adhabu yake na kamati ya saa 72.
Katika vurugu hizo, serikali iliamuru Simba kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibika, ikiwa ni pamoja na kuzuia mgawo wa Simba hadi walipe gharama za uharibifu, na Yanga ilitakiwa kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake 

TIGO KUJA NA KIFURUSHI KIPYA CHA INTANETI (MEGAMIX).

MKURUGENZI MTENDAJI WA TIGO.
Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Tigo imezindua kirufushi kipya cha intaneti kiitwacho  Megamix ambacho kitakuwa kimeambatana na muda wa maongezi ili kuendelea kuwafanya watanzania kuishi kidijitali.
Mkurugenzi wa biashara wa kampuni hiyo Shavkat Berdiev amesema kifurushi hicho  kitauzwa kuanzia Sh 500 na kitawawezesha wateja wao kupata taarifa za kidunia, kusikiliza muziki na  kupakua  sinema.
"Tumekuja na mpango huu kwa kuwa siku hizi intaneti ni huduma muhimu kwa binadamu ambapo huitumia kutatua changamoto zao za kila siku na kujipatia maarifa,"alisema Berdiev.

BODI YA MIKOPO KUPELEKA FEDHA VYUONI LEO.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI, PROFESA JOYCE NDALICHAKO.
Wakati ikiendelea na mchakato wa uhakiki wa waombaji wa mikopo, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo zinapelekwa vyuoni leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa agizo hilo baada ya wabunge mbalimbali kuomba miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17.
 Mwongozo kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo.
 Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga ameitaka Serikali kutoa maelezo.
 Akitoa kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako amesema fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita.
 “Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”amesema.
 Kuhusu wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako amesema wanafunzi wote wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Hata hivyo, amesema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo.
 Pia, amekiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni.
 Ndalichako amesema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni zimekwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.

DAKIKA 160 ZA MAGUFULI.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.
Rais John Magufuli amekutana na vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam katika tukio ambalo limehusisha wahariri  na kutumia dakika 160 kuelezea mambo yaliyojitokeza katika mwaka mmoja wa utawala wake.
Katika mkutano huo ulioanza saa 3:58 asubuhi mpaka saa 6.40 mchana, Magufuli aliyekuwa akizungumza kwa upole na masihara mara kadhaa, mbali na suala la muswada wa Sheria ya habari, mambo mengine yaliyoulizwa na kupata ufafanuzi ni mchakato wa Katiba Mpya, Tanzania ya viwanda, mgawanyo wa madaraka, ubora wa elimu, ugumu wa maisha na mgogoro wa Zanzibar.
Akijibu swali la muswada wa sheria ya habari hilo, Rais Magufuli amesema sheria hiyo kama zilivyo nyingine zimefuata utaratibu wa kupelekwa bungeni na kuwa ukipitishwa na kuwa sheria atausaini haraka.
“Sheria ya habari imeanza nafikiri kuanzia mwaka 2011, baadaye ukatolewa kwamba tujiandae zaidi. Sasa kama ndiyo hivyo kuanzia mwaka 2011 watu hawakujiandaa, mpaka leo 2016 hawakujiandaa maana yake hata wakipewa miezi mitatu hawawezi kujiandaa.
“…Mimi nakwambia bila unafiki, siku ukiletwa kwangu nitaisaini, ili kusudi kama mnataka kuibadilisha mkaibadilishe. Sitaki ku-frustrate (kupinga) maamuzi ya Bunge.Mnaweza kujikuta mnazungumza kwa sababu ya wamiliki wa vyombo fulani fulani, mtakuwa mmepotea. Kwa sababu katika rasimu niliyoiona, sifahamu wabunge watakachoamua, lakini pia ni ya kulinda masilahi ya waandishi wa habari na mnakuwa na vyombo vyenu,” amesema.
Kuhusu madai ya kuwapo kwa rushwa kwa wabunge ili muswada huo upitishwe, Rais Magufuli amesema kuna vyombo vya kupambana na rushwa vitashughulikia.
Wakati kukiwa na manung’uniko miongoni mwa wananchi kuhusu hali ngumu ya maisha, Rais Magufuli amesisitiza wanaolalamika hivyo ni watu waliozoea ‘kupiga dili’ kwa njia chafu.
“Mifuko imekauka, imekaukaje? Maana yake ulikuwa unapata fedha za ajabu ajabu. Sasa tumia mbinu nyingine ya kupata hela. Ndiyo maana nimetoa mfano wa ndugu zetu wa Lindi kule, mwaka jana waliuza korosho kwa kilo Sh600 hadi 700 mpaka 1,000. Leo kilo moja ya korosho wanauza kwa Sh4,000, four times (mara nne). Sasa huyo ukisema hela hamna atakushangaa,” amesema.
Hata hivyo, hotuba ya Rais Magufuli haikupita bila wadau kutoa maoni yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema Rais Magufuli kusitisha mchakato wa Katiba ni kulitia Taifa hasara.
“Inasikitisha sana kusikia Rais hana mpango na mchakato wa Katiba wakati ulitugharimu pesa nyingi kama Taifa kuufikisha mahali ulipofikia na ukweli ni kwamba nchi inahitaji Katiba Mpya,” amesema.
Profesa Abdallah Safari amesema, “Magufuli anairudisha nyuma Tanzania badala ya kuipeleka mbele, pesa nyingi zilitumika mchakato wa kuandika Katiba, iweje asitishe kwa urahisi namna hii.”
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana amesema ni vyema Watanzania wakatambua kuwa Katiba inatakiwa kuandikwa kwa utulivu na usahihi, hivyo ni vyema wakajipa muda.

MOURINHO AKASILISHWA NA UCHEZAJI WA MAN U.

Manchester United
WACHEZAJI WA MAN UNITED.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema wachezaji wa Manchester United walichukulia mechi dhidi ya Fenerbahce katika Europa League kana kwamba ilikuwa mechi ya kirafiki ya kujiandaa kwa msimu.
Red Devils walishuka hadi nambari tatu kwenye Kundi A ligi hiyo ndogo ya Ulaya baada ya kulazwa 2-1 na klabu hiyo ya Uturuki mjini Istanbul.
Manchester United sasa wameshinda mechi mbili pekee kati ya saba walizocheza mashindano yote karibuni.
"Timu inayofunga baada ya dakika mbili pekee ni timu ambayo haiko tayari, haijajiandaa kiakili, haina mwelekeo na haina umakinifu," amesema Mourinho.
United wamefunga mabao mawili pekee mechi zao nne walizocheza karibuni zaidi.
Aidha, walifungwa baada ya sekunde 30 pekee na Chelsea na sekunde 65 na Fenerbahce.
Mshambuliaji Moussa Sow alifunga kwa kombora la kushangaza la kupitishia mpira juu ya kichwa, naye Jeremain Lens akaongeza jingine kupitia frikiki kabla ya Wayne Rooney kufunga bao la kufutia machozi mechi ikikaribia kumalizika.
Bado lake hilo la dakika ya 89 limemuwezesha kufikia magoli 38 Ulaya na kufikia rekodi ya Ruud van Nistelrooy.
Hata hivyo, amefunga mabao mawili pekee katika mechi 17 alizocheza msimu wote.
Group A
Mourinho amesema: "Matatizo yetu yalianza na mtazamo wetu wa kiulimwengu. Walikuwa wanacheza fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, tulikuwa tunacheza mechi ya kirafiki ya majira ya joto. Huo ndio uhalisia wa jinsi mechi ilianza.
"Walistahili kushinda, soka haihusu tu ubora, kuna kutia juhudi pia, kujitolea, kujituma na kujitolea kabisa. Lazima ucheze dakika zote 90 kwa hamu na umakinifu.
"Katika mazingira kama haya, kuwapa nafuu wapinzani wako (kwa kufungwa mapema), hapo ndipo wanataka kuwa. Kisha, tulituliza kasi ya uchezaji na kuanza kumshinikiza refa, kuigiza kwamba tumechezewa vibaya na hayo ndiyo makosa yetu."
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea hata hivyo alikiri kuwa "moja ya mambo mazuri leo ni kwamba Rooney hatimaye amefunga bao."
Henrikh Mkhitaryan
Kati ya wachezaji walionunuliwa na Mourinho majira ya joto - Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly - ni Mfaransa Pogba pekee aliyeanza mechi.
Hata hivyo, aliondoka kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika akionekana kuumia.
Ibrahimovic aliiingia nafasi yake.
Mkhitaryan naye alichezeshwa mara ya kwanza tangu 10 Septemba. Aliingia dakika ya 61 nafasi ya Marcus Rashford. Beki wao Bailly anatarajiwa kukaa nje miezi miwili kutokana na jeraha la goti.
Haijabainika jeraha la Pogba ni mbaya kiasi gani na iwapo ataweza kucheza dhidi ya Swansea Ligi ya Premia Jumapili.
Sow akifunga bao la kwanza

Majeruhi United

Pogba, aliyetoka Juventus, amejiunga na orodha ya majeruhi wengi United amba wanajumuisha mabeki:
  • Eric Bailly (kano za goti) - hatacheza hadi Desemba
  • Antonio Valencia (mkono) - haijulikani atarejea lini
  • Chris Smalling (mguu) - haijulikani atarejea lini
  • Paul Pogba
    POGBA ALIUMIA.

    Magazeti Uingereza yalivyoandika baada ya United kuchapwa:

    Telegraph
    Independent
    Daily Mail



YAYA TOURE AOMBA MSAMAHA MAN CITY.

Yaya Toure
YAYA TOURE
Kiungo wa kati wa Manchester City amesalimu amri na kumuomba msamaha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya kutochezeshwa kwa muda na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola.
Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: "Naomba radhi - kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha - wasimamizi wa timu na wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya suitafahamu zilizotokea awali.
"Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii."
Wiki iliyopita, Guardiola aliambia wanahabari kwamba anamuhitaji Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo Dimitry Seluk.
Toure, 33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Baada ya kuachwa nje ya Guardiola kikosi cha wachezaji watakaocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Seluk alisema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang'anyiro hicho.
Yaya Toure
TOURE AKIWA UWANJANI.
Ni hapo ambapo Guardiola alijibu na kusema Toure hangecheza tena hadi ajenti huyo aombe msamaha.
''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kwenye kikosi," Guardiola alisema.
Guardiol alikuwa kocha mkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.

MWANAMKE ALIYEMZUIA TRUMP KUJENGA INDIA.

Smita Panvalkar
SMITA PANVALKAR.
Miaka mitano iliyopita mwanamke mwenye umri wa zaiid ya miaka 50 aliyekuwa akiishi kwenye jengo moja la miaka 87 mjini Mumbai alipata umaarufu mjini humo kwa kupinga mradi wa tajiri Donald Trump.
Taarifa zilimuelezea Smita Panvalkar ambaye alikuwa akiishi na mmewe , mtoto wake wa kiume na nduguye katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, kama kizuizi kikubwa cha Trump alipokuwa na mpango wa kuanza mradi wake wa kwanza nchini India.
Zaidi ya familia 20 ziliishi kwenye jengo ambalo lingebomolewa kujengwa kwa Trump Tower
JENGO ALILOTAKA KUMILIKI TRUMP.
Mwaka 2011 Trump, mfanyibiashara tajiri aliungana na mfanyibiashara mwingine raia wa India kujenga jumba la ghorofa 65 la Trump Tower lenye vyumba 50 vya kifahari.
Mji wa Mumbai unakumbwa na ubaha mkubwa wa ardhi, na mijengo yoyote mipya hujengwa baada ya majengo ya zamani kubomolewa kwa kuwalipa fidia au kuwapa makao mapya wakaazi wa zamani.
Hatma ya jengo la ghrofa la Pathare Prabhu ambapo Panvalkars alikuwa akiishi tangu mwaka 1990 ilikuwa hatarini.
Aliandikwa kwenye magazeti ya India
TRUMP ALIANDIKWA KWENYE MAGAZETI HUKO INDIA.
" Tuliishi masha ya kawaida hadi mwaka 2011, alisema Prasad Panvalkar ambapo alikuwa akilipa kodi ya dola 2.7.
Haikuchukua muda mrefu kabla ya Trump na mfanyibiasahara wa India kuafikia makubaliano ya kujenga jumba la Kwanza la Trump Tower nchini India.

Hata hivyo Smita Panvalkar alikataa kuondoka kabisa.
Familia hiyo iliendelea kuishi kwenye jengo hilo licha ya umeme kukosa kwa siku 45
FAMILIA HIYO ILIENDELEA KUISHI KWENYE NYUMBA HIYO.
Matajiri hao walitoa fidia. Lakini Smita akasema kuwa hataondoka kamwe hadi apewe chumba ndani ya jengo jipya.

Kwa miaka sita iliyofuata hadi mwezi Juni mwaka huu, familia ya Panvalkars ilikataa kuondoka na kutatiza jitihada za kubomolewa kwa jengo hilo.
Familia ya Panvalkars iliishi kwenye jengo hilo kwa miaka 27
Mradi huo mpya ulikumbwa na changamoto zaidi na hata kushindwa kufuata sheria za ujenzi.
Mwaka 2013 aliachana na mradi huo.

WAZIMBAMBWE WALALA NJE YA MABENKI KUSUBIRI FEDHA.

Zimbabwe iliacha kutumia sarafu yake mwaka 2009
Wazimbabwe si watu wa kutaka pesa zao kuchezewa hasa baada ya kuzinduliwa kwa noti ,mpya ambazo zina lengo la kusuluhisha tatizo la uhaba wa pesa nchini humo.
Picha za watu wakiwa wamelala nje ya mabenki wakisubiri yafunguliwe ili watoe pesa zao zimekuwa zikichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Gavana wa benki kuu Jonathan Moyo, alisema mwezi Mei kuwa noti hizo zitadhaminiwa na mkopo wa dola milioni 200 kutoka benki ya Africa Export-Import
Noti hizo za dola 5, 10, 20 zitakuwa na thamani sawa na zile wanazotumia za Marekani.
Zimbabwe ilianza kutumia dola za Marekani ilipoacha kutumia sarafu yake mwaka 2009.
Tangu wakati huo wazimbabwe wamekuwa wakitumia dola pamoja na sarafu za nchi zingine ikiwemo ya Afrika kusini ya rand na ya China ya yuan.

WAWADUNGA WATOTO SINDANO ZA MADAWA YA KULEVYA ILI WALALE.

Ashlee Hutt mwenye umri wa miaka 24 ana watoto watatu
Familia moja katika jimbo la Washington nchini Marekania inalaumiwa kwa kuwadunga watoto wadogo sindano zenye madawa ya kulevya ya heroin ili kuwafanya walale.
Polisi wanasema kuwa Ashlee Hutt na Mac Leroy McIver walipatikana wakiishi na watoto watatu wenye umiri wa miaka 6, 4 na 2 ambapo pia zilikuwepo sindano na madawa ya heroin.
Bi Hutt alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu ambapo anakabiliwa na kesi ya kuhatarisha maisha ya watoto.
Sindano na dawa ya heroin vilipatikana kwenye nyumba ya washukiwa
Bwana Mclver naye anakabiliwa na mashtaka kama hayo.
Kulinga na taarifa za mahakama, mtoto wa umri wa miaka sita aliwaambia wachunguzi kuwa watu hao waliwapa dawa ya kuhisi vizuri ambazo alizielezea kuwa poda nyeupe ambayo inachanganywa na maji na kudungwa kwa sindano.
Wawili kati ya watoto hao walipatikana na dawa hiyo mwilini baada ya uchunguzi pamoja na alama za kudungwa sindano.

HUAWEI YAZINDUA SIMU MPYA MATE 9.

Huawei Mate 9Huawei imezindua simu mpya yenye skrini kubwa wakati huu ambapo simu ya Samsung Galaxy Note 7 inakumbwa na changamoto.
Simu hiyo kwa jina Mate 9, ni kati ya simu za kwanza zinazotumia teknolojia ya Android 7 na inakuja ikiwa katika aina mbili za kamera.
Kampuni hiyo ya China inasema kuwa imeshughulikia tatizo la simu hizo kupoteza mauzo baadaye.
Lakini mtaalamu mmoja anasema kuwa wateja bado wanazitilia shaka simu za kampuni hiyo.
Simu za Huawei hazijafikia viwango vya simu za Samsung na ndiyo sababu huwa inafanya ushirikiano na kampuni zingine kama Leica na Porsche kuboresha teknolojia yake ya Kamera.
Samsung ilitizisha uundaji wa simu ya Note 7 mwezi uliopita baada ya simu kadha kuwaka moto.