Friday, August 12, 2016
KESI YA TYGA NA MWENYE NYUMBA WAKE KUFIKIA MUAFAKA.
Rapper Tyga week iliyopita alishitakiwa na mwenye nyumba wake kuwa alikaa miezi mitatu bila kulipa kodi, kisha akaondoka akaiacha nyumba ikiwa imeharibiwa na kumpa gharama mwenye nyumba kutengeneza, lakini Tyga hakwenda mahakamani kuhudhuria kesi yake. Ndipo alipoamuliwa kukamatwa Tuesday, 9 august.
Lakini Tyga na kambi yake ya kisheria wameweza kufikia muafaka na mshitaki ambaye ni mwenye nyumba katika mahakama ya Santa Monica.
CHRIS BROWN AMTETEA MALIA OBAMA.
ALIKIBA ATOA MILIONI 21 GSM FOUNDATION.
King of Bongo fleva Alikiba, amechangia kiasi cha milioni 21 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia watoto wanaosumbuliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi. Katika ukurasa wake wa Instagram Alikiba aliandika haya;
NAJ AMSAVE MR.BLUE KWA JINA LA ZAI.
Msanii wa kizazi kipya Naj ambaye ni mpenzi wa sasa wa Baraka Da Prince akanusha tetesi zinazomshutumu kuwasiliana na Blue aliyekuwa mpenzi wake wa zamani na kugombana na Baraka. inasemekana Blue alimpigia Naj usiku wa manane. Baraka baada ya kushika simu ya mpenzi wake akakuta namba imeseviwa kwa jina la Zai, sasa baada ya kuipiga akapokea mkaka ambaye ni Blue.
Katika kipindi cha XXL kwenye segment ya Uheard na Soudy brown mwanadada Naj alikanusha tetesi hizo na kukiri kuwa ilikuwa ni makosa kumsave blue kwa jina la kike.
"zamani kabla sijawa na Baraka, nilipata nilipata namba hiyo sasa nikasave haraka kwa jina hilo la Zai ili niingie whatsaap nijue nani" Alisema Naj
"kwanza mimi siwasiliani na Blue, yani nikishaachana na mtu siwezi kuwa na mawasiliano naye, kwanza tunaongea nini?" Alisema NajNingekuwa sijihamini nisingempa Baraka simu yangu ashike, najiamini ndio maana anashika simu yangu. pia mimi na Baraka hatujagombana.
AIKA WA NAVY KENZO AFUNGUKA KUHUSU HARUSI YAO.
Mwanadada maarufu wa kundi la Navy Kenzo Aika afunguka na kusema harusi yao itafungwa tu Mungu akipenda, hiyo imetokana na mashabiki kutaka kujua lini ndoa yao maana wamekuwa wakisema watafunga na miaka inakwenda tu. Aika aliulizwa katika 255 ya XXL Clouds FM kati ya ndoa na mtoto kipi kitatangulia?
"chochote kinaweza tangulia itategemea tu coz siwezi sema nataka ndoa kwanza kabla ya mtoto ya Mungu mengi, chochote kitakachotangulia sawa tu nipo tayari" Alisema Aika.
BONGO STAR SEARCH KUANZA HIVI KARIBUNI.
Week hii Madam Ritha amepost instagram post ambayo ameelezea ujio wa msimu mpya wa Bongo star search. Watu wengi wanafikiri bongo star search haitokuwepo mwaka huu kama miaka iliyopita, lakini Ms.Paulsen amerithibitisha hilo ingawa BSS imechelewa mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)