Saturday, August 20, 2016

WATOTO WAINGIZWA KWENYE JESHI SUDANI KUSINI.

Serikali ya Sudani kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya kwa mujibu wa shirika la Associated press.

Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.

Nyaraka zinaonyesha kuwa shughuli za kuwaajiri watoto hao ilifanyika muda mfupi baada ya baraza la usalama la  umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudani kusini, kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.

Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Macha ambaye tayari amekimbia nchi hiyo.


PICHA YA MVULANA WA SYRIA ILIYOWASIKITISHA WENGI.

Picha ya mvulana mdogo akiwa ameketi kwenye gari la  kubebe wagonjwa Syria, imeweka wazi madhara wanayopitia raia nchini humo.

Mvulana huyo anaonekana akiwa amejaa damu na vumbi baada ya kutelekezwa kwa shambulio la angani mji wa Aleppo.

Picha hiyo ya Omran mwenye umri wa miaka 4, imesambaa sana mtandaoni sawa na ilivyofanya picha ya mwili wa Aylan Kurdi, uliopatikana ufukweni mwa uturuki mwaka jana.

Omran alitolewa kwwnye vifusi baada ya kutelekezwa kwenye shambulio la angani Jumatano katika eneo la Qaterji, kusini mashariki mwa Aleppo.

Watu 290,000 wameuawa na mamilioni wengine kutoroka makwao katika vita vilivyoanza mwaka 2011 nchini humo.


WEMA AKANUSHA KURUDIANA NA DIAMOND.

Ndani ya wiki hii kumetokea vitu vingi kati ya Wema na Idris kugombana, mpaka kupelekea Idris kufuta akaunti yake ya Instagram.

Sasa siku mbili zilizopita kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya Romeo (Romy Jons) binamu yake Diamond na Wema akahudhuria kwenye sherehe hiyo na kupelekea watu kujua Wema amerudiana na Diamond, kwa sababu alionekana kuwa karibu sana na WCB.

Lakini Wema aliongea kwenye U heard ya Clods FM na kukanusha hizo tetesi kuwa hayupo pamoja na Naseeb.

"Yani watu wakiona naongea na Diamond wanajua tumerudiana, hapana mimi na Naseeb hatuna beef tena nafurahi na nina amani".

Wema alisema hana tatizo na familia ya Diamond na kukanusha kumchukia Tiffa na kukana kumuita Zombie.

"Simchukii Tiffa kwa sababu hajanikosea, yule ni malaika kwa nini nimchukie wakati mimi napenda watoto"

Wema alimalizia kwa kusema kuwa hana shida na Zari kwa sababu ametongozwa na Diamond hana kosa yeye pia ni mwanamke.


BREAKING NEWS: MSANII MKONGWE WA TAARABU BI SHAKILA SAID AFARIKI DUNIA.

Marehemu Bi Shakila amefariki usiku wa jana na sasa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya jeshi lugalo.

Bi Shakira amewahi kutamba na nyimbo hizi macho yanacheka moyo unalia, hujui alacho kuku pamoja na kifo cha mahaba.

Mwili wa marehemu utapumzishwa leo saa saba mchana.

INALILAH WAINAILLAH RAAJIUN