Msanii mkongwe wa bongo flava Juma nature aliendeleza bifu lake na msanii mkongwe mwenzake T.I.D Mnyama baada ya kutuma picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha KR msanii ambaye alikuwa chini ya Nature lakini kwa sasa yupo kwa Mnyama.
KR alichukuliwa na T.I.D kutoka kwa Nature ili aendelezwe kimziki zaidi, huku Mnyama huyo akimuongelea vibaya Juma Nature kwa kusema kundi lao ni wachafu ndio maana wakaamua kumchukua KR ili wamsafishe rasta zake na kumuweka kisanii zaidi.
Nature alisikika akisema kwenye kipindi cha XXL Clouds FM (U heard) akisema kuwa ameamua kutuma picha hiyo ili kumpa funzo KR kuwa hapaswi kufanya vitendo kama hivyo.
"Mimi nilipigiwa simu na kuambiwa kuwa KR kakutwa kalala pembezoni mwa reli na kutumiwa picha, nilishangaa sana kwa sababu boss wake anajitapa, nahisi itakuwa ni bangi na sio pombe iliyomfanya hivyo" alisema nature.
Hiyo picha juu ni post aliyotuma Juma Nature.
Monday, September 5, 2016
BIFU LA JUMA NATURE NA T.I.D LAPAMBA MOTO.
MAJAMBAZI WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM WAKIWA NA SILAHA.
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekamata watu watatu wanaoshutumiwa kuwa ni majambazi na kukamata silaha na vifaa vya aina mbalimbali zikiwemo bunduki, risasi, redio call pamoja na sare za polisi katika msako maalumu wa kukamata waharifu.
Akizungumsha na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao walisema wana nyumba wanaishi eneo la Mbezi chini na kuzikamata silaha hizo kwenye nyumba, ambapo pia ilidaiwa kuwa majambazi hao ni raia wa Kenya.
Sirro amezitaja silaha hizo ni kama SMG 3, bastola 16, shotgun 3 pamoja na risasi zaidi ya 800.
Mbali na silaha hizo pia Sirro amesema pia polisi wamekamata redio call 12, sare za polisi, pingu 45 na darubini 3.
WAYNE ROONEY: MCHEZAJI ALIYEICHEZEA ENGLAND MECHI NYINGI.
Wayne Rooney ameandika historia ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu ya taifa ya England mara nyingi zaidi, kwa wachezaji ndani ya uwanja.
Ulikuwa mchezo wake wa 116 kuiwakilisha England alipocheza na Slovakia katika michuano ya kufuzu Kombe la dunia la 2008.
Rekodi hii inaipita ya David Beckham ambaye aliichezea timu ya taifa ya England mechi 115.
Mlinda mlango Peter Shilton ndiye anaishika rekodi ya jumla kwa kuichezea England mara 125.
LIL WAYNE ATANGAZA KUACHA MZIKI.
Lil Wayne ametangaza kustaafu kutoka kwenye tasnia ya mziki.
Aliandika kwenye Twitter "Sasa sijiwezi tena, hata kiakili na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu".
Hata hivyo hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa au ataacha uimbaji wa mziki wa kufoka.
Mwanamziki huyo mwenye umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki kuonewa huruma.
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari mbalimbali hivi karibuni. Alikuwa na mzozo wa mda mrefu na Cash Money Records kuhusu kucheleweshwa kwa Albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina la The Carter V.
Alishutumu kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
Polisi Miami walifika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji wa risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.
DODOMA- WATOTO WA MITAANI KUONDOLEWA.
Serikali mkoani Dodoma itafanya operesheni ya kuwaondoa watoto wa mitaani, ambao wamekuwa kero kwa wapita njia na wateja wanaokula hotelini, ambao huwanyang'anya chakula na hata vinywaji wateja.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme alisema watawaondoa watoto hao kutokana na kuwa hatari kwa maisha ya watu wengine. Mndeme alisema watoto hao wamekuwa wakikaa makundi na kuvuta dawa za kulevya aina ya gundi na wamekuwa wakiingia kwenye hoteli na kunyang'anya wateja chakula na vinywaji vyao.
"Idara ya maendeleo ya jamii itaanza kuwaondoa watoto wa mtaani wanaovuta bangi na petroli" alisema.
Alisema watoto hao wamekuwa wakikaa kwenye makundi na kuwa tishio kwa wapita njia hasa nyakati za jioni kutokana na kujihusisha na uhalifu.
"Tutazitambua familia za watoto hao wanapotoka, watarudishwa wanapotoka na wengine watapelekwa shuleni" alisema Mndeme.
Alisema wanachukua hatua hiyo kwa umakini ili watoto watakaoondolewa wasirudi tena mitaani, kwani inaonesha miaka ya nyuma lilifanyika lakini baada ya mda watoto hao walirudi tena mtaani.
WANAFUNZI WAMALIZA MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA.
Wahitimu wa kidato cha Sita waliohitimu mwaka huu, wamemaliza mafunzo yao ya JKT ambayo walianza miezi mitatu iliyopita.
Hiyo ilikuwa ni awamu ya kwanza kwa wahitimu hao, majina ya awamu ya pili yatatolewa hivi karibuni.
Moja ya kambi zilizomaliza mafunzo hayo ni Bulombora kikosi cha 821.
Mafunzo hayo yalifungwa Jana.
MTUHUMIWA MWINGINE ALIYEHUSIKA KWENYE MAUAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA APATIKANA.
Idadi ya washtakiwa katika kesi ya mauaji ya Aneth Msuya ambaye alikuwa dada wa Bilionea maarufu mkoani Arusha, Erasto Msuya imeongezeka na kufikia wawili baada ya mwingine kuunganishwa nayo.
Awali Agosti 23, mwaka huu mshitakiwa Miriam Mrita (41) ambaye ni mke wa bilionea huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth aliyekuwa wifi yake.
Hata hivyo juma moja baadae mfanyabiashara wa jiji hilo, Revocatus Evarist (40) alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo na kuunganishwa na Miriam kwenye kesi hiyo.
Evarist alipandishwa kizimbani mahakamani hapo ijumaa iliyopita na kusomewa shtaka la mauaji ya Aneth na Wakili wa serikali, Diana Lukondo.
MADEREVA TAX DODOMA WAPOTEZA IMANI.
Madereva tax mjini Dodoma wameonyesha wasiwasi kuhusu ujio wa makao makuu, wakidai hauna tija kwao.
Katika vituo vya teksi mjini hapo, madereva wamesema hawaoni tija yoyote kwani licha ya kuwepo kwa ongezeko la idadi ya watu hakuna biashara.
Daudi Yona ambaye gari yake huegeshwa katika kituo cha Nyerere Square alisema hali ya biashara siyo nzuri pamoja na kuwapo kwa idadi kubwa ya watu mjini hapa.
Yona alisema katika kipindi hiki hali ni ngumu kuliko ilivyokuwa miezi mitatu ya nyuma.
Alisema siku hizi watu wengi wanatumia usafiri wa bajaji badala ya magari na hata wageni wanaokuja nao wanatumia usafiri wa bajaji badala ya magari.