Inawezekana likawa ni tukio baya lililoacha simanzi na majonzi baada ya mfanyabiashara maarufu jijini moshi Romani Shirima (74) kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli kwa kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.
Ingawa hakuna taarifa ya nini kilichosababisha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walisema ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.
Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la marangu alijilipua kwa petroli katika gari lake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:25 asubuhi maeneo ya mjohotoni.
Alisema mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha na kujilipua na kibiriti.
Kamanda Mutafungwa alisema chanzo bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.
Taarifa za tukio hilo la aina yake limekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Moshi na vitongoji vyake.
Sunday, August 21, 2016
MFANYABIASHARA AJILIPUA NYUMBANI KWAKE JIJINI MOSHI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment