Wednesday, August 24, 2016

TETEMEKO LA ARDHI ITALIA LASABABISHA VIFO VYA WATU 21.

Nyumba zimefukiwa
Kikosi cha waokoaji wakifanya kazi

Watu takribani 21 wafariki baada ya kutokea tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter katikati mwa Italia.

Watu wengine wengi wamefukiwa chini ya vifusi.

Wengi wamefariki katika kijiji cha Pescara del Tronto ambacho kimeharibiwa vibaya na inahofiwa kwamba idadi ya waliofariki inaweza ikaongezeka.

Tetemeko hilo lilitokea mwendo wa saa tisa na dakika thelathini na sita usiku saa za Italia (01:36)GMT, 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia katika kina cha 10km (maili 6) chini ya ardhi.

Taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi imesema USGS.

Mitetemeko ilisikika miji ya mbali kama vile Roma, Venice, Bologna na Naples. Mjini Roma baadhi ya majumba yalitikisika sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la Repubblica.

Mji wa Amatrice nao pia uliharibiwa vibaya. Watu wanne wanahofiwa kufariki katika mji jirani wa Accumoli.

Eneo hilo ambalo linapatikana katikati ya mikoa ya Umbria, Lazio na Marche ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii.

Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika mji wa Norcia karibu na Perugia.

Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia za ulinzi wa nchi hiyo.

Meya wa mji wa Amatrice Sergio Perozzi ameambia kituo cha redio cha serikali cha RAI kwamba mji huo umeharibiwa vibaya.

Barabara za kuingia na kutoka mjini hazipitiki, nusu ya mji imeharibiwa, watu wamefukiwa chini ya vifusi. Kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja moja ambalo huenda likapolomoka.


No comments: