Serikali ya Sudani kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya kwa mujibu wa shirika la Associated press.
Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.
Nyaraka zinaonyesha kuwa shughuli za kuwaajiri watoto hao ilifanyika muda mfupi baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudani kusini, kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.
Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Macha ambaye tayari amekimbia nchi hiyo.
Saturday, August 20, 2016
WATOTO WAINGIZWA KWENYE JESHI SUDANI KUSINI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment