Monday, August 22, 2016

WAZIRI MKUU ATOA TAHADHARI HII KWA WATENDAJI KATAVI.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka watendaji halmashauri mkoani katavi kuwa makini na matumizi ya fedha za maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea zitamuunguza.

"Fedha hii tafadhari ni ya moto, msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta hapa kwa ajili ya wananchi itawaunguza vidole, tunaileta kwa madhumuni tunataka wananchi wahudumiwe". Alisema waziri mkuu.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo jana jioni wakati akihutubia umati mkubwa wa wananchi  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Azimio wilayani Mpanda.

Alisema ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao  kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.


No comments: