Wabunge wote wa chama cha wananchi (CUF) wametangaza rasmi kutomtambua aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Wamemtaka msajiri wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kutomkumbatia mwanasiasa huyo aliyebobea katika uchumi, akielezwa kwa sasa hana sifa za kuwa mwenyekiti, labda aanze upya mchakato.
Wameeleza msimamo huo jana mjini Dodoma na Mbunge wa viti maalum, Riziki Mngwali ambaye pia ni kiongozi wa wabunge wa CUF katika mkutano baina ya waandishi wa habari za bunge na wabunge wa CUF isipokuwa mbunge wa jimbo la Kaliua, Magreth Sakaya aliyesimamishwa uanachama.
Mngwali alisema Lipumba amekuwa akikiyumbisha chama na hivi karibuni kudai amekaririwa akisema anasubiri barua ya msajili wa vyama vya siasa ya kuthibitishiwa kuendelea na uenyekiti wake.
"Wakati anajiuzuru uenyekiti Agosti 5 mwaka jana alitangazia umma na kudai anakwenda Rwanda kwa kazi aliyodai ya utafiti ili asaidie serikali, lakini inashangaza sasa anataka kujirejeshea uenyekiti, hilo hatukubali kwa kuwa chama kina taratibu zake" alisema.
Friday, September 16, 2016
WABUNGE WA CUF HAWAMTAMBUI LIPUMBA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment