Wednesday, November 16, 2016

SAMIR NASRI:GUARDIORA HUWATAKA WACHEZAJI KUTOFANYA MAPENZI BAADA YA SAA 6 USIKU.

SAMIR NASIR

Mchezaji wa Ufaransa katika safu ya kati Samir Nasri amefichua kwamba mojawapo ya ufanisi mkubwa wa mkufunzi Pep Gurdiola ni kuwaagiza wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya saa sita usiku.

Katika mahojiano na runinga ya Ufaransa,Nasri amesema kuwa Guardiola aliweka sheria hiyo hata iwapo kungekuwa hakuna mechi siku iliofuatia ili wachezaji wapate usingizi mwanana.

Hata Lionel Messi anayetambulika kuwa mchezaji bora duniani hakuwachwa nje wakati wa uongozi wa Guradiola katika timu ya Barcelona.

Nasri amesema kuwa hatua hiyo ilimwezesha Messi kutopata majeraha ya misuli


No comments: