Director maarufu hapa nchini Hascana, ametangaza rasmi kuachana na Wanene na kuanza maisha yake mapya. Hanscana alisema hajagombana na uongozi wa wanene entertainment bali ameamua kuondoka ili aanzishe maisha yake mwenyewe, kwasababu amekuwa sasa (23).
Director huyo ameondoka na crew yake nzima ya videos department tangu tarehe 4 mwezi huu wa nane, kwasababu ya kutofautiana kimalengo kati ya Hanscana brand na wanene entertainment. Hanscana alisema ametumia juhudi kubwa sana kuipigania hiyo kampuni kama yake from zero to hero, mpaka kufikia kuwa moja ya kampuni kubwa ya videos hapa Afrika Mashariki.
Hascana alisema kuwa anahitaji kuwa na kampuni yake mwenyewe na hakuna ubaya kati yake na wanene entertainment.
"Kitu ambacho nilikipigania mwenyewe siwezi kukiongelea vibaya, hata kwa bahati mbaya".
Hanscana alimaliza kwa kusema, ameamua kuweka wazi jambo hilo kwasababu amekuwa alipigiwa simu sana na waandishi, bloggers.
Monday, August 15, 2016
DIRECTOR HANSCANA ATANGAZA KUACHANA NA WANENE ENTERTAINMENT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment