Weekend iliyopita kulikuwa na tamasha kubwa la Fiesta lililofanyika jijini mwanza siku ya Jumamosi katika viwanja vya CCM Kirumba.
Mwanamziki mashuhuri wa nyimbo za visingeli Manifongo alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza katika tamasha hilo.
Balaa lilikuja pale Manifongo alipokuwa anatumbuiza nyimbo aliyoshirikishwa na msanii Shilole wimbo unaokwenda kwa jina la Mtoto mdogomdogo.
Manifongo alionekana kujiachia na kimshikilia Shilole. Ndipo mke wake alipata wasiwasi kutokana na show hiyo.
Manifongo alikuwa anakiambia kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, kuwa kwa sasa wameelewana kwa sababu ilibidi amueleweshe mke wake kuwa alikuwa kazini na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.
Vilevile Manifongo alitambulisha nyimbo yake mpya inayoitwa Tumtafute Kibaka.
Wednesday, August 24, 2016
FIESTA YASABABISHA MUIMBAJI WA MZIKI WA KISINGELI MANIFONGO KUGOMBANA NA MKEWE.
BRUCE LEE ACHAGULIWA KUWA DIWANI AFRIKA KUSINI.
Baada ya Vasco da Gama kuwa spika wa baraza la mji wa Johannesburg nchini Afrika kusini, sasa Bruce Lee amechukua wadhifa katika baraza la Tshwane mjini humo.
Kwa wale waliokosa somo la historia, Vasco da Gama alikuwa baharia maarufu ambaye amerikodiwa kuwa mtu wa kwanza kusafiri makini kutoka Ulaya hadi India kupitia Cape of good hope.
Na muda mfupi badae orodha ya majina ya madiwani ilitolewa huko Tshwane nchini humo humo yalionesha Bruce Lee akiwa katika wadhifa wa maendeleo ya kiuchumi katika baraza hilo.
Bruce Lee ni mcheza filamu kutoka nchini Marekani.
RAYVANN WA WCB ASHINDWA KUJIZUIA NA KUANGUSHA KILIO CHA FURAHA.
Mwanamziki anayetokea katika lebo ya WCB Rayvan azawadiwa zawadi ya gari aina ya Rav4 katika siku yake ya kuzaliwa.
Raymond alikuwa anatimiza miaka kadhaa siku ya jumatatu na usiku wake kukawa na sherehe ndogo ya kumpongeza iliyofanyika nyumbani kwa Diamond Platnumz pande za Madale.
Lakini kundi la WCB walimfanyia surprise kubwa Raymond kwa kumzawadia gari aina ya Rav4, ndipo Raymond alishindwa kujizuia na kulia machozi ya furaha.
Raymond ni msanii chipukizi anayefanya vizuri katika tasnia ya bongo flava. Kwa sasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Natafuta kiki.
UZINDUZI WA TUZO ZA MTV MAMA 2016.
Tuzo za MTV Mama zitafanyika Octoba 22 kwenye mji mkuu wa Afrika kusini, Johannesburg.
Uzinduzi wa tuzo hizo umefanyika jumanne hii jijini humo mbele ya waandishi wa habari. Tuzo mbili zilizopita zilifanyika jijini Durban nchini humo.
Tuzo hizo zitatolewa katika ukumbi wa Ticket Pro Dome. Tarehe ya hafla ya kutajwa vipengele na washiriki wa tuzo za mwaka huu itatangazwa siku za usoni.
UTAFITI: JE WAJUA KUOSHA MDOMO NI DAWA YA KISONONO.
Kuosha mdomo kunasaidia kupunguza maambukizi ya kisonono, watafiti wanaamini.
Utafiti wa hivi majuzi umeonyesha kwamba binadamu wanaweza kubeba magonjwa ya zinaa katika koo zao kwa muda wa wiki moja au hata miezi bila ya kupata dalili zozote.
Na wanaweza kusambaza kwa wengine kupitia ngono isiyo salama ya mdomoni.
Wachunguzi wanajaribu kuona iwapo kuosha mdomo Mara kwa Mara kunaweza kusaidia kuzuia polepole na wataalamu wanasema kuwa ni wazo ambalo linafaa kutumiwa.
Tuesday, August 23, 2016
MWANZILISHI WA BENDI ZA BACKSTREET BOYS NA NSYNC AFARIKI.
Mwanzilishi wa bendi ya Boy band, Lou Pearlman amefariki akiwa na umri wa miaka 62.
Pearlman pia ni mwanzilishi wa bendi ya backstreet boys maarufu iliyosajili mauzo mengi pamoja na ile ya Nsync.
Alifungwa kwa takribani miaka 25 mwaka 2008 kwa kuhusika na udanganyifu wa mpango wa ponzi uliogharimu dola 300.
Mwimbaji wa Nsync Lance Bass alituma ujumbe katika twitter alisema kuwa Pearlman hakuwa mfanyabiashara mzuri lakini hasingekuwa hapo alipo bila ushawishi wake.
Sababu ya kifo chake bado haijulikani.
KIONGOZI WA BOKO HARAM AJERUHIWA NA JESHI LA NIGERIA.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Abubakar Shekau, amejeruhiwa vibaya kwenye shambulio la angani lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo.
Makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa.
Taarifa kutoka katika jeshi la angani la Nigeria, limesema shambulio hilo lilitekelezwa ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa jeshi, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.
Kiongozi wao, anayefahamika kama Abubakar Shekau anaaminika kujeruhiwa vibaya begani, jeshi limesema kupitia taarifa iliyotolewa na naibu mkuu wa mawasiliano Kanali Sani Kukasheka Usman.
Kundi la Boko Haram hivi karibuni limekabiliwa na mzozo wa viongozi.
Kundi la Islamic State lilitangaza kuwa Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa kundi la Boko Haram.
Lakini muda mfupi badae, Shekau alisema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo na akamshutumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.