Tuesday, January 24, 2017

MWANAMITINDO MWENYE JINSIA MBILI.

Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili.
Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba alizaliwa na jinsia mbili.
Gaby mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa ameamua kutangaza jinsia yake ili kuhamasisha watu kuhusu watu wenye jinsia mbili mbali na kutoa hamasa kwa jamii.
Ni miongoni mwa wanamitindo wa hadhi ya juu kuzungumzia kuhusu jinsia yake.
Watu wenye jinsia mbili hawana viungo vya ndani ama vya nje vinavyowatambulisha moja kwa moja kuwa na jinsia ya kiume ama ile ya kike.
''Nimefikia wakati katika maisha yangu ambapo nimeamua kutangaza jinsia yangu'', alisema Hanne.
''Ni wakati wa watu wenye jinsia mbili kujitokeza, kuondoa uoga na kuzungumzia maswala ambayo yalitukumbuka tukiwa watoto''.
Hanne ameshiriki katika kuuza mitindo ya Chanel na Prada na pia amekuwa katika kampeni za Mulberry na Balenciaga.

WASANII 5 WA KIKE AFRIKA WANAOTENDEA HAKI MASHABIKI ZAO WAKIWA STEJINI WAKITUMBUIZA.

1. YEMI ALADE.
Image result for YEMI ALADE

2. VANESSA MDEE.
Image result for VANESSA MDEE

3. VICTORIA KIMANI.
Image result for VICTORIA KIMANI

4. TIWA SAVAGE.
Image result for TIWA SAVAGE

5. SEYI SHAY.
Image result for SAY SHAY

LIST YA WATANZANIA WALIOINGIA KWENYE TUZO ZA HIPIPO ZA UGANDA.

The Prestigious HiPipo Music Awards |#HMA2017, 4th/Feb/2017 at Serena
WIMBO BORA WA MWAKA TANZANIA.
AIYOLA - HARMONIZE

KAMATIA - NAVY KENZO

AJE - ALIKIBA

SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

KAJIANDAE - OMMY DIMPOZ ft ALIKIBA

ZIGO REMIX - AY ft DIAMOND PLATNUMZ

SU - YA MOTO BAND ft RUBY

NIROGE - VANESSA MDEE

WIMBO BORA AFRIKA MASHARIKI.
KAMATIA - NAVY KENZO

ZIGO REMIX - AY ft DIAMOND PLATNUMZ

SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

VIDEO BORA YA MWAKA AFRIKA MASHARIKI.
SALOME - DIAMOND PLATNUMZ ft RAYVANN

JE UTANIPENDA? - DIAMOND PLATNUMZ

MSANII MWENYE VIEWS WENGI YOUTUBE.
Tanzania kaingia DIAMOND PLATNUMZ peke yake.



MPIGIE KURA JIHAN KWENYE MASHINDANO YA MISS UNIVERSE.


"VOTE! VOTE! VOTE!!The door is open
sasa tunaweza kumpigia kura mrembo wetu @jihandimack
Kwakutumia Applications tulizopakua na kama bado hujapakua basi waweza pakua sasa na umpigie kura @jihandimack
kutoka Tanzania.

Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:


1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
3) MISS U APP: Pakua Miss U app
4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu. 


Upigaji kura utakapoanza kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.

Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa

Saturday, January 21, 2017

ALICHOKIANDIA FARAJA NYARANDU INSTAGRAM KUHUSU MELANIA TRUMP.


Mwaka 1996, Melanija Knavs akiwa na miaka 26 aliingia Marekani akiwa na ndoto ya kuwa mwanamitindo. Jana, akiwa ni Melania Trump, alishika Biblia aliyotumia kuapa Rais wa 45 wa Marekani, Rais Donald Trump.


Ukiniuliza kama alidhani kuna siku angesimama Capitol Hill kwenye uapisho wa Rais kama Mke wa Rais wa Marekani, nitakwambia hapana. Lakini ndivyo Mungu alivyo. Leo hii huhitaji kumheshimu Melania Trump, ila utaheshimu mamlaka yake, na kwakuwa amekalia hicho kiti chenye mamlaka, utajikuta unamheshimu tu.


Unaweza kudhihaki historia yake, lafudhi yake au hata kazi aliyokuwa anafanya. Ila Mungu keshampa kibali cha kuwa hapo. Hata huyo Askari ukute alimpigia kura Hillary ila anajikuta akitii mamlaka ya Melania.


Kiongozi anaweza akatoka sehemu chakavu isiyo na tumaini. Chini, mwisho kabisa. Kumbuka hata Bwana Yesu alizaliwa katika zizi la ng'ombe. Mungu anaweza kumuinua mtu usiyemtarajia na kumfanya mtawala wako. 


Mungu anaweza kukuinua wewe usiyejidhania na kukuweka mahali pa juu. Mipango Yake si kama yetu. Usidharau mtu yeyote na muhimu Usijidharau. Njia Zake si kama zetu.

Friday, January 20, 2017

TAMASHA KUBWA LA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA.

Image result for SALAAM SK
SALLAM SK.

Meneja wa Diamond Platnumz, fundi mitambo Sallam SK ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.

Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000.
.
Sallam alizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Instagram (Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika uwanja wa Taifa.
.

“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” alisema

Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuudhuria.

QUEEN DARLEEN: SIJAWAHI KUTONGOZWA.

Image result for QUEEN DARLEEN
QUEEN DARLEEN.
Msanii kutoka WCB, Queen Darleen amefunguka jana usiku katika kipindi cha Pillow talk kinachorushwa na Times Fm kuwa, hajawahi kutongozwa.

Queen alisema''kusema ukweli mimi sijawahi kutongozwa na mwanaume, kwa asilimia kubwa mimi ndio huwa nawtongoza wanaume.