Friday, January 20, 2017

TAMASHA KUBWA LA DIAMOND PLATNUMZ KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA.

Image result for SALAAM SK
SALLAM SK.

Meneja wa Diamond Platnumz, fundi mitambo Sallam SK ametangaza ujio mpya wa tamasha kubwa la Diamonds Are Forever 2017 ambapo safari hii litafanyikia katika uwanja wa Taifa.

Muimbaji huyo alifanya tamasha hilo kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2012 katika ukumbi wa Mlimani City show ambayo ilihudhuriwa na watu wengi kwa kiingilio cha Tsh 50,000.
.
Sallam alizungumza live na mashabiki katika mtandao wa Instagram (Insta Live) alisema show hiyo ipo kwenye maandalizi na itafanyika uwanja wa Taifa.
.

“Mjiandae na Diamonds Are Forever 2017, Diamonds Are Forever 2017 is back,” alisema

Meneja huyo alidai safari hii tamasha hilo litafanyika uwanja wa taifa ili kuwapa fursa watu wengi zaidi ya kuudhuria.

No comments: