Friday, August 26, 2016

MUOGELEAJI WA MAREKANI RYAN LOTCHE ASHITAKIWA.

Polisi nchini Brazil wamemshtaki muogeleaji wa olmpiki wa Marekani Ryan Lotche kwa kutoa madai ya uongo kuwa yeye na wenzake watatu waliibiwa kwa kushikiwa bunduki wakati wa michuano ya Rio, kitu ambacho ni upotoshaji.

Uhalifu huo hukumu yake ni miezi nane jela.

Msemaji wa polisi ameeleza kuwa kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lotche atatakiwa kujibu mashtaka hayo. Idara ya Marekani  imesema inatambua ombi hilo.

Lotche ameondoka Brazil kabla hajaojiwa na polisi. Ameomba msamaha kwa kusema uongo juu ya kuibiwa. Lotche amepoteza wadhamini wake wakubwa wanne kufuatia tukio hilo na hivyo kuweka hatarini kazi yake ya uogeleaji.


No comments: