Friday, August 26, 2016

SAMATTA ASAIDIA KLABU YAKE KUFUZU MASHINDANO YA EUROPA LEAGUE.

Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

Hii ni baada ya klabu yake KRC Genk ya Ubelgiji kupata ushindi wa jumla 4-2 mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao Lokomotiva Zagreb ya Croatia.

Genk walipata ushindi wa 2-0 mechi iliyochezwa jana jioni.

Klabu hizo mbili zilitoka sare 2-2 mechi ya mkondo wa kwanza.

Samatta alifungia klabu yake bao la kwanza dakika ya pili naye mwenzake Leon Bailey akafunga la pili muda mfupi baada ya mapumziko.

Samatta pia alioneshwa kadi ya njano dakika ya 69.

Droo ya hatua ya makundi itafanywa mjini Monaco baadae leo ijumaa mwendo wa saa tisa za Afrika Mashariki.


No comments: