Saturday, August 13, 2016

MZEE YUSUPH KUACHA MZIKI NA KUMRUDIA MUNGU.

                                   

Gwiji wa mziki wa taarabu nchini Mzee Yusuph "Mfalme wa taarabu" amethibitisha kuwa ameachana na kazi hiyo takribani miezi miwili iliyopita. Taarifa zilienea kwenye mitandao ya kijamii siku mbili zilizopita kuwa nguli huyo ameachana na mziki huo.

Mzee Yusuph alikubali kuhusiana na taarifa hizo kuwa ni za kweli na akusema "nashangaa hizi taarifa zinasemwa leo, ni suala la muda mrefu takribani miezi miwili iliyopita na kwa sababu nimeamua kurudi kwa Allah".

Alisema familia yake imekubaliana na maamuzi yake, kwa sasa ataanza kuimba kaswida zenye mafundisho ya dini. Alipoulizwa kwanini alichukua uamuzi mkubwa kiasi hicho, alijibu kifupi,
"ndiyo tunavyofundishwa na viongozi wa dini"
Ijumaa hii Mzee Yusuph alikuwa katika Swalat Jumaa ndani ya masjid Taqwa Ilala Bungoni, alipopata fursa ya kuongea na waumini alishindwa kuvumilia na kuanza kulia.
Pia alisema kuwa aataitisha mkutano rasmi kuelezea swala hilo.


HISTORIA FUPI YA MZEE YUSUPH.
Mwimbaji na Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, amezaliwa Zanzibar mwaka 1977 na amemaliza darasa la 10 katika Shule ya Haile Selasie.

Alianza mziki baada ya kumaliza darasa la kumi na  alikuwa anafanya mziki na maigizo, huku anaendelea na shule na ikafika pahali akachukuliwa na bendi ya melody.

Mzee Yusuph ameshinda tuzo nyingi katika tasnia ya mziki wa taarabu zikiwemo Kilimanjaro Music Awards 2014-2015.

No comments: