Sunday, September 4, 2016

VIJANA 7,170 WALIOPITIA JKT WAAJIRIWA.

Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Ally Mwinyi.

Vijana 7,170 waliojiunga kwa kujitolea katika jeshi la kujenga Taifa (JKT) wameajiriwa katika  vyombo vya ulinzi na usalama kuanzia mwaka 2010 mpaka sasa.

Waziri wa ulinzi na JKT, Dk. Hussein Ally Mwinyi amesema kuanzia mwaka huo JKT huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi na kuwajengea uzalendo.

Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na TBC, Dk. Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri toka uraiani bali vijana  waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa wakiajiriwa kwa mwaka.

Alisema pia kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kampuni binafsi za ulinzi.


No comments: