Thursday, October 27, 2016

MATOKEO YA DARASA LA SABA.

Baraza la Mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi (PSLE) ambayo yameonyesha ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.

Akitangaza matokeo hayo leo (Alhamisi), Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema jumla wa watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

Amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 70.3 ya ufaulu tofauti na ufaulu wa mwaka jana ambao ulikuwa ni asilimia 67.8

"Hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52," amesema Dk Msonde.

Pia amezitaja shule 10 bora kuwa ni  Shule ya Msingi Kwema (Shinyanga), Rocken Hill (Shinyanga), Mugini (Mwanza), Fountain of Joy ( Dar es Salaam), Tusiime (Dar), Mudio Islamic (Kilimanjaro), Atlas (Dar), St Achileus (Kagera), GiftSkillfull (Dar) na Carmel (Morogoro)


No comments: