BABU TALE.
Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale na ndugu yake Idd Taletale wamekwama tena mahakamani katika harakati zao za kukwepa ulipaji wa fidia ya Sh250 milioni kutokana na makosa ya hakimiliki.
Badala yake hatima yao sasa itajulikana Jumanne juma lijalo wakati Mahakama itakapotoa maelekezo muhimu.
Babu Tale ambaye pia ni meneja wa msanii maarufu nchini wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), Abdul Nassib maarufu kama Diamond Platnum na nduguye leo wamekwama baada ya Mahakama Kuu, Dar es Salaam kuwagomea na kutupilia mbali maombi yao.
Leo walipaswa waieleze Mahakama ni kwa nini wasifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama hiyo iliyowaamuru kulipa fidia hiyo baada ya kupatikana na hatia ya ukiukwaji wa Sheria ya Hakimiliki, au kueleza ni lini na namna gani watalipa fidia hiyo .
http://burudaninaangie.blogspot.com/
http://burudaninaangie.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment