MKUU WA WILAYA YA GEITA, HERMAN KAPUFI. |
Kituo cha Afya Katoro kilichopo Wilaya ya Geita mkoani hapa kinakabiliwa na uhaba wa majengo la kulazimu kulaza wagonjwa na maiti kwenye wodi moja.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Peter Janga alisema mgonjwa anapofariki hulazimika kumuacha kitandani hadi ndugu zake wafike kuchukua mwili na kama hana ndugu, huagiza gari kutoka hospitali ya mkoa kwa ajili ya kwenda kuhifadhiwa huko.
“Tunalazimika kuwachanganya kwa sababu hatuna chumba kingine cha kuwalaza, tunachokifanya kama mgonjwa akifariki tunaweka godoro chini na kuulaza mwili hapo,” alisema Dk Janga.
Alisema mbali na ukosefu wa jengo la kuhifadhia maiti na wodi, wanakabiliwa na uhaba wa vitanda.
“Tatizo hilo linatulazimisha kuwalaza wagonjwa wawili wawili kwenye kitanda kimoja.
No comments:
Post a Comment