Monday, November 7, 2016

WASHINDI WA TUZO ZA MTV EMA.


Tuzo za MTV Europe Awards 2016 ‘MTV EMA’ zimefanyika usiku wa kuamkia leo November 7 2016, washindi wa tuzo hizo ni;
BEST SONG
Adele – “Hello”
Justin Bieber – “Sorry” — WINNER
Lukas Graham – “7 Years”
Mike Posner – “I Took A Pill In Ibiza (Seeb Remix)”
Rihanna ft. Drake – “Work”
BEST VIDEO
Beyoncé – “Formation”
Coldplay – “Up&Up”
Kanye West – “Famous”
Tame Impala – “The Less I Know the Better”
The Weeknd ft. Daft Punk – “Starboy” — WINNER
BEST FEMALE
Adele
Beyoncé
Lady Gaga — WINNER
Rihanna
Sia
BEST MALE
Calvin Harris
Drake
Justin Bieber
Shawn Mendes — WINNER
The Weeknd
BEST LIVE
Adele
Beyoncé
Coldplay
Green Day
Twenty One Pilots — WINNER
BEST NEW
Bebe Rexha
DNCE
Lukas Graham
The Chainsmokers
Zara Larsson — WINNER
BEST POP
Ariana Grande
Fifth Harmony  — WINNER
Justin Bieber
Rihanna
Selena Gomez
Shawn Mendes
BEST ROCK
Coldplay — WINNER
Green Day
Metallica
Muse
Red Hot Chili Peppers
BEST ALTERNATIVE
Kings of Leon
Radiohead
Tame Impala
The 1975
Twenty One Pilots — WINNER
BEST HIP HOP
Drake — WINNER
Future
G-Eazy
Kanye West
Wiz Khalifa
BEST ELECTRONIC
Afrojack
Calvin Harris
David Guetta
Major Lazer
Martin Garrix — WINNER
BEST PUSH
Alessia Cara
Anne-Marie
Bebe Rexha
Blossoms
Charlie Puth
DNCE — WINNER
Dua Lipa
Elle King
Halsey
Jack Garratt
Jonas Blue
Lukas Graham
BIGGEST FANS
Ariana Grande
Beyoncé
Justin Bieber — WINNER
Lady Gaga
Shawn Mendes
BEST WORLD STAGE
Duran Duran – Piazza Del Duomo, Milan (2015)
Ellie Goulding – Piazza Del Duomo, Milan (2015)
Jess Glynne – Isle of MTV, Malta (2016)
Martin Garrix – Isle of MTV, Malta (2015) — WINNER
One Republic – MTV Evolution, Philippines (2016)
Tinie Tempah  – MTV Crashes, Plymouth (2015)
Tomorrowland – Belgium (2016)
Wiz Khalifa – Isle of MTV, Malta (2016)
WORLDWIDE ACT WINNERS
Troye Sivan – Australia
Shawn Mendes – Canada
Maluma – Columbia
GOT7 – Korea
Wizkid  – Nigeria
Zara Larsson – Sweden
Ariana Grande – U.S.

Saturday, November 5, 2016

HITIMISHO LA BURUDANI FIESTA JIJINI DAR.

Image result for TIGO FIESTA

Lile tamasha la Fiesta lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wakazi wa Dar es salaam limewadia. Ni siku ya leo tarehe 5 Nov, Jumamosi 2016, litafanyika katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa kumi na mbili jioni.

KIINGILIO:
18,000/= Ukilipa kwa TigoPesa
20,000/= Ukilipa kawaida
25,000/= Ukilipa cash mlangoni

tigo-fiesta

WASANII WATAKAO KUWEPO:
TEKNO, YEMI ALADE, JOSE CHAMELEON huku wakisindikizwa na wasanii wa ndani;

  • Vanessa
  • Belle9
  • Benpol
  • Darasa
  • Weusi
  • Juma nature
  • Jux
  • Chege
  • Tunda man
  • Shilole
  • Manfongo
  • Barnaba
  • Alikiba
  • Raymond
  • Hamadai
  • Maua sama
  • Mr. Blue
  • Nandy
  • Young D
  • Baraka da prince
  • Billnass
  • Christian Bella
  • Dogo janja
  • Fid Q
  • Jay Moe
  • Stamina
  • Sholo mwamba
  • Msami
  • Roma
  • Lord Eyes


MBILIKIMO WASHIRIKI MITINDO.

wakipita-jukwaani
MBILIKIMO KATIKA MASHINDANO.
Wanawake wafupi warembo wameweza kuvunja mtazamo wa miaka mingi kuwa urembo na au uanamitindo ni kwa warefu, wenye miguu mirefu na wembamba pekee.
Ni kupitia maonesho ya mitindo ya mavazi yanayopigiwa chapuo na taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo la Onesho la Kimataifa la Mitindo la Mbilikimo.
Taasisi hiyo, inayoitwa Onesho la Taifa la Mitindo la Mbilikimo ilianzishwa mwaka mwaka 2014 mjini New York Marekani baada ya kuona changamoto zinazowakabili mbilikimo.
Tayari imechochea kufanyika kwa mashindano ya mitindo ya mavazi kwa mbilikimo katika miji ya New York, Paris, Berlin na hivi karibuni mjini Tokyo Japan.
Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali hulenga kuinua uelewa na mwamko kuhusu umbilikimo.
Huwashirikisha katika maonesho hayo kufuatia changamoto zinazowakabili kupata mavazi yanayowafiti.
Kubwa zaidi kuliko yote maonesho haya huendesha kampeni za kubadili mtazamo wa jamii kuhusu tasnia nzima ya urembo kwa ujumla wake na vigezo vya aina ya washiriki.
Hivi karibuni mjini Tokyo, Japan wanawake mbilikimo sita waliweza kushiriki onesho la kimataifa la mitindo kwa mbilikimo.
Picha zikionesha warembo hao wakipingana na dhana kuwa urembo ni kwa ajili ya warefu pekee wakiwa wamependeza na mavazi yao wakati wakitembea kwa miondoko ya kipaka huko Ebisu, zilivutia hadhila. Ni onesho la mavazi lililofana mno.
Hivyo, waliweza kuonesha kwamba wanamitindo wanaweza kutokana na maumbo na saizi yoyote ile kuliko inavyofikiriwa sasa.
Kwa kawaida wanamitindo wanafahamika  kuchaguliwa wakiwa na vigezo vya urefu si chini ya mita 1.30.
Na washiriki hawa ‘twiga’ kutoka duniani kote husafirishwa katika madaraja ya juu ya ndege na kuwekwa katika hoteli za kifahari kwa kushiriki maonesho hayo.
Hali kama hizo zinazowafanya wahusudiwe huwafanya wanawake wengine kuhesabiwa hawana sifa na au si warembo.
Kitendo hicho huwaathiri wengine kisaikolojia au hujikuta wakiingia katika mkumbo wa kujitengeneza miili yao kwa kupandikiza plastiki, kitu ambacho kinafahamika ni hatari kwa afya.
Shoo hii ya Japan inafanyika kwa mwaka wa tatu ikiwa tayari imefanyika katika miji ya Paris na New York kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Katika onesho la mwaka jana mjini Paris, ambalo liliandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya serikali kusaidia kuhamasisha viwango mbadala vya urembo katika tasnia hiyo inayopendelea warefu na wembamba.
Lilifanyika baada ya waandaaji kuishutumu vikali tasnia ya urembo nchini humo kwa kubagua wanawake wengine.
Wanawake mbilikimo 15 wenye urefu wa futi nne walishiriki kwa mavazi tofauti tofauti ya kisasa yaliyobuniwa na wabunifu maarufu mjini humo.

CLINTON AMTUHUMU TRUMP KUMTUMIA WAHUNI KUMZOMEA.

MGOMBEA urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton
HILLARY CLINTON.
Mgombea urais kupitia Chama cha Democrat, Hillary Clinton, jana uzalendo ulimshinda na kuwakemea waandamanaji waliokuwa wakimzomea katika mkutano wake wa kampeni, huku akimtuhumu hasimu wake, Donald Trump kuwatuma.
Waandamanaji hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyosomeka ‘Bill Clinton ni mbakaji’ katika jimbo la Florida, walimpa usumbufu mkubwa mgombea huyo wakati akihutubia kutokana na kelele na maneno waliyokuwa wanayatoa.
Akiwa kwenye mkutano huo wa hadhara, Clinton alionyesha waziwazi kukerwa na kitendo cha waandamanaji hao na kumshutumu Trump kufadhili vitendo visivyo vya kiungwana katika kampeni.
“Nimechoshwa na vitendo vya giza na uchokozi vinavyotoa picha mbaya ambavyo vinafanywa na wafuasi wanaomuunga mkono Donald Trump,” alisema Clinton kwa sauti yenye hasira.

MAGUFULI: YANGA NA SIMBA MWIKO KUTUMIA UWANJA WA TAIFA.

Rais John Magufuli akiwa na msanii nguli wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto, Ikulu, Dar es Salaam baada ya Rais kuzungumza na wahariri na waandishi wa habari jana. (Picha na Mroki Mroki).
RAIS MAGUFULI AKIWA NA MRISHO MPOTO, JANA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amepigilia msumari wa mwisho kwa timu za Simba na Yanga na kuzitaka zifute ndoto za kutumia Uwanja wa Taifa.
Rais Magufuli alisema jana Ikulu Dar es Salaam, katika mkutano wake na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari na kudai kuwa anapenda kwenda uwanjani kuangalia mpira, lakini anashindwa kufanya hivyo kutokana na fujo ambazo zimekuwa zikizuka kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
“Natamani kwenda Ndondo Cup kuangalia kuliko kwenda kuangalia timu ambazo wanashindana Uwanja wa Taifa, wakishindwa wanang’oa viti,”alisema Rais Magufuli na kuongeza: “Nimefurahi uamuzi wa Waziri (Nape) kufungia uwanja, ni lazima kujenga nidhamu, uwanja umejengwa kwa gharama kubwa, huwezi kung’oa viti, Ndondo ni bora kuliko hizo timu kubwa,”alisema.
Kauli ya Magufuli imekuja ikiwa ni siku za kadhaa baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuzifungia kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana timu za Simba na Yanga kutokana na mashabiki wa timu hizo kung’oa viti katika mechi ya Ligi iliyofanyika Oktoba mosi na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Hata hivyo, vurugu kubwa ziliibuka kabla na baada ya mchezo huo ambao kabla ya mchezo mashine za tiketi za elektroniki zilishindwa kufanya kazi na kusababisha mlundikano kwenye mageti upande wa lango la Yanga na mashabiki kukosa uvumilivu na kuvunja mageti hayo.
Vurugu nyingine kubwa ilizuka dakika ya 26 ya mchezo baada ya mchezaji wa Yanga, Amis Tambwe kuifungia timu yake bao, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua utata, huku wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele, hata hivyo Mkude alikuja kufutiwa adhabu yake na kamati ya saa 72.
Katika vurugu hizo, serikali iliamuru Simba kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibika, ikiwa ni pamoja na kuzuia mgawo wa Simba hadi walipe gharama za uharibifu, na Yanga ilitakiwa kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake 

TIGO KUJA NA KIFURUSHI KIPYA CHA INTANETI (MEGAMIX).

MKURUGENZI MTENDAJI WA TIGO.
Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Tigo imezindua kirufushi kipya cha intaneti kiitwacho  Megamix ambacho kitakuwa kimeambatana na muda wa maongezi ili kuendelea kuwafanya watanzania kuishi kidijitali.
Mkurugenzi wa biashara wa kampuni hiyo Shavkat Berdiev amesema kifurushi hicho  kitauzwa kuanzia Sh 500 na kitawawezesha wateja wao kupata taarifa za kidunia, kusikiliza muziki na  kupakua  sinema.
"Tumekuja na mpango huu kwa kuwa siku hizi intaneti ni huduma muhimu kwa binadamu ambapo huitumia kutatua changamoto zao za kila siku na kujipatia maarifa,"alisema Berdiev.

BODI YA MIKOPO KUPELEKA FEDHA VYUONI LEO.

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI, PROFESA JOYCE NDALICHAKO.
Wakati ikiendelea na mchakato wa uhakiki wa waombaji wa mikopo, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo zinapelekwa vyuoni leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ametoa agizo hilo baada ya wabunge mbalimbali kuomba miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17.
 Mwongozo kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo.
 Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga ameitaka Serikali kutoa maelezo.
 Akitoa kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako amesema fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita.
 “Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”amesema.
 Kuhusu wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako amesema wanafunzi wote wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa mwaka uliopita.
Hata hivyo, amesema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo.
 Pia, amekiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni.
 Ndalichako amesema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni zimekwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.