Saturday, November 12, 2016

SITTA APUMZISHWA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE HUKO TABORA.

Mamia ya wananchi mkoani Tabora wamejitokeza kumuaga Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta aliyefariki usiku wa kuamkia Jumatatu ya wiki hii.
Wananchi hao wamejitokeza katika Uwanja Shule ya Msingi Urambo jirani ya nyumbani kwake Sitta shughuli ya kutoa heshima za mwisho wa wananchi hao imeanza saa moja asubuhi.
Wananchi hao walijipanga katika mstari mrefu kwa ajili ya kupita pembeni ya jeneza lenye mwili wa Sitta, ambapo toka asubuhi maduka mengi wilayani Urambo yalikuwa yamefungwa.

BARAKA DA PRINCE ANAHITAJI MSAADA.

barakah-1-656x800
BARAKA NA NAJ
Mtoto wa miaka miwili badala ya kusema kikombe akatoa tusi, hufai kumpiga wala kumgombeza. Unachotakiwa kufanya ni kumtia nguvu katika juhudi zake za kujifunza na kumwambia kwa usahihi neno kikombe linavyotamkwa. Hivyo ndivyo hata kwa mtu mgeni katika miji mikubwa.
Mshamba akitoa huko mashambani na kukutana na lifti  katika majengo makubwa na kutaka kuvua viatu kisha ndio aingie, ukimcheka utakuwa juha.
Sasa unamcheka nini na hayo mambo kwao hakuna? Unashanga kitu gani yeye kuvua viatu na kutaka kuingia katika lifti wakati huko kwao kafundishwa ni ustaarabu ukikuta maeneo nadhifu uvue viatu?
Nimetoa mifano hiyo nikikumbuka tabia ya msanii Baraka Da Prince. Kwa siku za hivi karibuni bwana mdogo amekuwa na matukio na kauli za ajabu na cha kushangaza watu wanamshangaa na wengine kumtolea maneno makali.
Ni kweli Baraka anafanya mambo ya kijinga, yasiyofaa kufanywa na mtu anayejitambua. Ila mimi sishangai hayo mambo kufanywa na mtu aina ya Baraka.
Yangefanywa na Diamond, Ali Kiba na akina Chegge  ningeshangaa mno. Nishangae vipi Baraka kuposti nyumba ya mama yake Naj na kusema ni yake wakati najua kijana wetu huyu bado hajatokwa matongotongo machoni?
Katu siwezi kushangaa na yeyote atakayemshangaa, nitamshangaa yeye. Ni jambo linalotarajiwa kabisa kwa kijana ambaye miaka mitatu nyuma alikuwa akishindia kababu na mihogo huku akiwa ndani ya kaptura chafu isiyojulikana rangi yake, viatu vilivyotoboka na akiwa anadhihakiwa na kila msichana anayejaribu kumchombeza, kuwafanyia unyama ndugu zake kisa kuwa na msanii Naj katika mapenzi.
Baraka ni kwanini asitokwe na akili kwa Naj wakati miaka mitatu iliyopita alikuwa akimuona bibie katika magazeti na majarida akiwa kakumbatiwa na Mr Blue, msanii ambaye Baraka huyu amekuwa akimuona toka kipindi anaomba Shilingi ishirini akanunue ice cream kwa mama John?
Siwezi kumlaumu Baraka. Kumlaumu Baraka kwa ujinga anaoufanya ni sawa na kulaumu mtoto mdogo anapotukana kipindi akijifunza kuongea.
Siku moja katika mitandao ya kijamii Baraka baada ya kuposti picha ya mpenzi wake, Najma Dustan, msanii mwenzake, mtoto wa mjini Msami akamtania kwa kujifanya anamtamani Naj.
Kilichotokea kiliniacha hoi kwa kicheko. Baraka akatokwa na matusi kwa Msami na kumwambia akamtamani dada yake.
Baraka anatupa maneno haya kwa mtu ambaye amekuwa akionekana katika video na magazeti kwa zaidi ya miaka sita sasa.
Anatokwa povu la kijinga kwa Msami kwa kudhani kuwa eti ni kweli anamtamani mpenzi wake huku akiwa amesahau ni Msami huyu ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na mastaa wengine wakubwa wa Bongo.
Msami ni mtoto wa  mjini sana kuliko Baraka. Msami kaona mengi ya kimjini kuliko yeye. Kutoka  dansa hadi kuwa msanii mwenye kueleweka, Baraka anatakiwa ajue uzito wa Msami.
Yeye bado ni mgeni katika jumba la mastaa, anayofanya ni sehemu ya ulimbukeni wa kawaida kwa mgeni. Kumlaumu au kumkosoa sana ni kumkosea.
Anayofanya Baraka ni sawa na mtu ambaye hajawahi kumiliki au kuendesha gari zuri la thamani. Atatembea kila eneo kutaka kuonesha kuwa anaendesha gari zuri. Huu ni  ulimbukeni.

Friday, November 11, 2016

MKE WA RAIS MAGUFULI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.


Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ameruhusiwa na kurejea nyumbani leo (Ijumaa), baada ya afya yake kuimarika.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa imesema kuwa kabla ya kuondoka katika wodi ya Sewahaji alikokuwa amelazwa Mama Janeth Magufuli amewashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa matibabu mazuri aliyoyapata na pia amewashukuru Watanzania wote kwa kumuombea afya njema.
"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru madaktari na wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara.
"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu" amesema Mama Janeth.
Mama Janeth alilazwa MNH tangu juzi  baada ya kuugua ghafla na kupoteza fahamu.

BONGO FLEVA: THAMANI MAPENZI BY RWEGA DA ONE.

Kutoka kwenye miamba iliyopangana ikapangika, sio pengine tunazungumzia Rock City (Mwanza). Yule kijana machachali RWEGA DA ONE aliyeimba Isabela na Nakudeku anakuja tena na video mpya inayokwenda kwa jina la THAMANI MAPENZI.
Video inatoka siku ya Jumapili 13Nov.
Video directed by Blaki Bryan kutoka ROCK GOLD ENTERTAINMENT.



MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ASHINDWA KUFANYA MTIHANI BAADA YA KUPIGWA NA MWALIMU MKUU.

Image result for beaten students
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ridhwaa Seminary iliyopo wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Yusuph Kivugo, amemshambulia mwanafunzi wake, Mbaraka Mwalimu, kwa kumpiga ngumi usoni na kumsababishia maumivu makali.
Mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha nne katika shule hiyo iliyopo Kinondoni Mkwajuni, alikutwa na mkasa huo Novemba 3, mwaka huu wakati akijiandaa na mtihani wa Historia.
Kwa mujibu wa ratiba ya mitihani ya taifa ya kidato cha nne inayoendelea nchini, mtihani huo ulikuwa unafanyika mchana, lakini hata hivyo hakufanya kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.
“Tulikuwa msikitini na wenzangu tunasoma, ilikuwa ni saa mbili asubuhi kabla ya mtihani wa Historia kuanza, mwalimu alikuja akauliza kwanini tunapiga kelele na kuanza kutupiga.
“Upande wa pili kulikuwa na wanafunzi wa pre-form one ndio waliokuwa wakipiga kelele, nilishangaa kamkunja mwenzangu anaitwa Mohamed akawa anampiga mangumi, mimi nilijua labda kuna kosa amefanya.
“Katika kujitetea akina Mudy walikimbia, mara akaja kwangu akanishika akaanza kunishambulia, amenipiga ngumi nyingi za usoni, kwenye taya na nyingine jichoni kiasi kwamba sikuweza kufanya mtihani kwani jicho lilivimba sana,” alisema.
Mwalimu wa nidhamu shuleni hapo, Omary Ikome, alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Alisema jukumu lake ni kusimamia nidhamu kwa wanafunzi na kwamba suala hilo lipo juu ya uwezo wake.
“Nilimkuta Mbaraka analia na jicho la kushoto limevimba, nilimuuliza akasema amepigwa na mkuu. Mimi nasimamia nidhamu kwa wanafunzi, lakini kwa kuwa kitendo hiki kimefanywa na bosi wangu, siwezi kuzungumzia zaidi kwani lipo juu ya uwezo wangu,” alisema.
Mwalimu mkuu huyo alipoulizwa kiini cha tatizo, hakuweza kutoa ushirikiano na kumfukuza mwandishi ofisini kwake.

TB JOSHUA AREJESHA UJUMBE ALIOFUTA FACEBOOK.

index
TB JOSHUA
Utabiri kutoka kwa mhubiri raia wa Nigeria TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani, umerejeshwa tena baada ujumbe huo kufutwa kutoka mtandao wa Facebook.
Kulingana na barua pepe iliyotumwa kwa BBC na idara ya mitandao ya kanisa la TBJMinistries ilisema kuwa , “ujumbe huo uliondolewa kimakosa na sasa umerejeshwa kwa kuwa hiyo si sera yetu.”
“Siku kumi zilizopita nilimuona rais wa Marekani akishinda kwa kura chache, yule niliyemuona ni mwanamke,” ujumbe huo ulisema.
TB Joshua alikejeliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakati watu walitambua kuwa ujumbe huo ulikuwa umefutwa, licha ya wafuasi wake wengi katika mitandao ya kijamii bado kumtaja kuwa nabii.

BEYONCE NA JAY Z WAMTAKA MICHELLE OBAMA KUGOMBEA URAIS 2020.

beyonce-jay-z
BEYONCE NA MUMEWE JAY Z.
Baada ya Hillary Clinton kushindwa katika uchaguzi mkuu nchini Marekani dhidi ya Donald Trump, nyota wa muziki nchini humo, Jay Z na mke wake, Beyonce, wamemtaka mke wa Barack Obama, Michelle Obama, awanie kiti hicho 2020.
Wasanii hao walikuwa wanamsapoti Hillary katika uchaguzi huo na walikuwa wanaungana baadhi ya sehemu kwa ajili kumnadi, lakini hajafanikiwa kushinda, hivyo wawili hao wameamua kuangukia kwa mke wa Obama, Michelle, kuwa awanie nafasi hiyo mwaka 2020 wataungana pamoja kwenye kampeni.
Michelle na mume wake, Obama, ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wanampigia debe Hillary, lakini hawakufanikiwa.
Novemba 7 mwaka huu, Jay Z aliachia wimbo mpya ambapo ndani yake kuna mistari inasema kuwa anataka mtoto wake akue huku akiwa anaongozwa na rais mwanamke na hivyo walitamani kuona Hillary kupata nafasi hiyo.
“Nilitamani kuona mtoto wangu akiwa anakua chini ya rais mwanamke, Hillary hajapata nafasi hiyo, lakini ninaamini bado kuna nafasi nyingine baada ya miaka minne ijayo, nimekuwa nikiongea na Michelle mara kwa mara na ninaamini atafanya hivyo,” alisema Jay Z.
Wasanii mbalimbali wameonesha kuguswa na uchaguzi huo, huku wengine wakionesha kuwa tofauti na matokeo hayo.
Lady Gaga
Image result for LADY GAGA
LADY GAGA.
Nyota huyo wa muziki nchini Marekani, juzi alionekana mtaani akiwa amevaa T-shirt ambayo inaonesha kumpenda Rais Mteule, Donald Trump.
Msanii huyo alionekana katika mitaa ya jiji la New York akiwa amevaa T-Shirt nyeupe yenye maandishi mekundu ambayo yanasema ‘Nakupenda Trump’.
T.I
Image result for T.I
T.I
Rapa T.I kwa upande wake amempa pole rais ambaye anamaliza muda wake, Barack Obama, kwa mteja wake kushindwa katika uchaguzi huo.
“Pole kwa matokeo ambayo kuna baadhi ya watu hawakuyatarajia, lakini tunafurahi tulikuwa na wewe kwa kipindi chote, lakini sasa tunasubiri kinachofuata,” alisema T.I.
Snoop Dogg
Image result for snoop doggy
SNOOP DOGG.
Rapa huyo ameonekana kumshambulia Hillary kwa kushindwa uchaguzi huo. Snoop amedai kuwa Hillary ameshindwa mbele ya mtu dhaifu.
Hata hivyo, rapa huyo alionekana kutumia maneno makali kwa Hillary na pia amedai kuwa Obama hakuwa na timu nzuri ya kuweza kuwashawishi watu.