Ukaguzi uliofanyika katika shule za msingi 6,831 zilizokaguliwa 2015/16 umebaini kuwa wanafunzi 10273, katika shule 515 nchini hawajui kusoma wala kuandika.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi uthibiti ubora wa shule katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi Marystella Wasena jana jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia mikakati ya kukagua na kusimamia utekelezaji na ufundishaji wa kusoma, kuandika na kuongea KKK kwenye shule za awali na msingi.
Alisema miongoni mwa wanafunzi hao 10,273 wasichana ni 5,263 na wavulana ni 5,010 huku tathmini ikibainisha kuwa sababu mojawapo ya tatizo hilo ni wanafunzi wenyewe kushindwa kumudu kujifunza. Pia zipo sababu zilizotokana na watekelezaji wa mtaala wakiwemo walimu wenyewe kukosa umahili wa kufundisha KKK.
Kutokana na hali hiyo alisema idara inaendelea na mipango ya kuwajengea uwezo wathibiti ubora wa shule ili wapate umahiri huo shuleni.
Alisema katika awamu ya kwanza idara katika mradi wa kukuza Stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu LANES imeshawewezesha wathibiti ubora wa shule 1,469 kupitia mafunzo elekezi yaliyofanyika Mei mwaka huu katika vyuo vya ualimu vya Patandi (Arusha), Butimba (Mwanza), Mtwara, Morogoro na Kleruu (Iringa).
Alisema kupitia mafunzo hayo yaliyofanyika Mei, idara iliazimia kuanzisha uthibiti ubora wa ndani ya shule kwa kuhakikisha kila kanda na wilaya inateua shule mbili za mfano zikiwemo shule za sekondari na binafsi ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa.
Naye mthibiti ubora wa shule elimu ya awali na msingi Hawa Selemani alisema shule binafsi zinafanikiwa katika eneo hilo kwa sababu zinachukua wanafunzi wachache kwa kila darasa tofauti na za serikali ambazo zinalenga kutoa huduma.
Sunday, August 28, 2016
IDADI KUBWA YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HAWAJUI KUSOMA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment