Saturday, August 27, 2016

POLISI WAANZA MSAKO MAALUMU WA MAJAMBAZI.

Kamanda Sirro

Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam imetuma askari zaidi ya 80 kwenda katika misitu ya vikindu, Mkuranga na maeneo ya jirani kufanya operesheni maalumu ya kuwasaka majambazi.

Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro amesema kikosi cha askari hao kimeondoka mchana huu kwenda kwenye operesheni hiyo.

Kuhusu mapambano ya jana katika eneo la vikindu mashariki, wilayani mkuranga alisema kuna watu kadhaa waliuawa  na wengine kadhaa wamekamatwa bila kutaja idadi kwa kile alichoeleza kuwa kinaweza kuvuruga upelelezi.

Wakati huo huo kamishna Sirro amesema bado jeshi hilo linaendelea kusisitiza kutokufanya maandamano Septemba 1 na tayari limepata taarifa kuwa kuna vijana wamelipwa fedha kufanya hivyo.

"Kuna vijana tunajua wamelipwa fedha kufanya maandamano Septemba 1 sisi tumekataza ila kama wao wanaona ni vyema kuandamana tunawakaribisha" alisema kamanda Sirro.


No comments: