Monday, October 31, 2016

WANAOSOMEA CHINI YA MWEMBE WAONGOZA KIMKOA.

Shule ya msingi Kashifa katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi licha ya kukabiliwa na uhaba wa madarasa na walimu, imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya na kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2016.
Katika matokeo ya mwaka 2015 shule hiyo, ilishika nafasi ya pili kiwilaya na nafasi ya 18 kimkoa.
Shule hiyo yenye wanafunzi 600 ipo katika kata ya Ikola, mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Kwa miaka mitano mfululizo, wanafunzi wake wanasomea chini ya miti kutokana na kuwa na vyumba viwili vya madarasa na walimu saba tu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) hivi karibuni, yamebainisha kuwa shule hiyo imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya kati ya shule 31 na nafasi ya kwanza kimkoa kati ya shule 92.
Shule hiyo imeshika nafasi ya 176 kitaifa kati ya shule 8,241 zilizofanya mtihani huo.
Ufaulu huo unaonesha kuwa wanafunzi 14 wakiwemo wasichana sita na wavulana wanane wamepata alama B katika somo la Kiingereza.
Katika Hisabati wanafunzi watatu wamepata alama A na 11 wamepata alama B.
Somo la Sayansi wanafunzi wanane wamepata alama A, sita wamepata alama B.
Diwani wa Kata ya Ikola, Philemon Moro amekiri kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na walimu wanafundisha chini ya miembe.

MAMBO ATAKAYOFANYA RAIS MAGUFULI KENYA.

Rais John Magufuli ameondoka asubuhi hii kwenye nchini Kenya atakakofanya ziara ya siku mbili.
Mbali na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta, taarifa ya Ikulu imesema Rais Magufuli atafanya mambo yafuatayo:
  1. Kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
  2. Kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.
  3. Kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen, Nairobi, na
  4. Kuzindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo jijini Nairobi.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA OKTOBA 31, 2016.

NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Man City101523
2Arsenal101323
3Liverpool101123
4Chelsea101222
5Tottenham10920
6Everton10718
7Watford10115
8Man Utd10115
9Southampton10113
10Bournemouth10-212
11Leicester10-412
12Crystal Palace10-211
13Burnley10-511
14Middlesbrough10-210
15West Brom10-410
16West Ham10-910
17Stoke9-79
18Hull10-157
19Swansea9-75
20Sunderland10-132

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUANZA MTIHANI WA NECTA KESHO.

Image result for FORM FOUR NECTA PICTURE
Jumla ya watahiniwa 408,442 wa kidato cha nne wanatarajia kuanza mitihani ya kidato cha nne itakayoanza kesho, ikiwa ni idadi pungufu ya waliofanya mtihani huo mwaka jana.
Akizungumza na wanahabari leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dk Charles Msonde amesema mwaka jana kulikuwa na watahiniwa  448,382 waliofanya mitihani huo.
Dk Msonde amesema maandalizi yote ya mitihani hiyo itakayomalizika Novemba 18, mwaka huu yameshakamilika.
Amewataka wanafunzi, walimu na wasimamizi kujiepusha na udanganyifu wa mitihani kwani baraza hilo halitasita kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kuwafutia matokeo.

TAZAMA PICHA ZA HARUSI YA RAPPER MABESTE.


sv1
sv3

MSAKO WA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WANAOPOKEA MIKOPO KIMAKOSA.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema itawapoka mikopo baadhi ya wanafunzi ambao uhakiki utawabaini kuwa hawakuwa wanastahili kupewa mikopo waliyokopeshwa. Utaratibu huo utawagusa wanafunzi wapya na wale wanaoendelea na masomo baada ya bodi kufanya uhakiki na uchunguzi wa taarifa za wanufaika wote wa mikopo. Uchunguzi huo unaanza kesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru alisema wanafunzi watakaokutwa na hadhi zisizostahili wataondokewa na sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi cha fedha watakachokuwa wamepokea tayari. Alifafanua kuwa kiasi cha fedha ambacho watalazimika kurejesha wanafunzi ambao watakutwa hawana uhitaji ni fedha walizochukua kuanzia Novemba mwaka huu.
“Kwa kweli tukikuta mtu ambaye anapata mkopo na hana uhitaji kwa kweli tutamnyang’anya mkopo ili apate mtu mwingine mwenye uhitaji,” alisema Badru.
Uamuzi huo wa bodi wa kutangaza kuwapoka mikopo baadhi ya wanafunzi ni wa kwanza kufanywa na chombo hicho ambacho mara kwa mara kimekuwa kinatoa mikopo kwa kufuata sera za serikali.
Miaka ya nyuma wanufaika wa mikopo hiyo walikuwa ni wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na la pili bila kujali familia wanazotoka. Lakini mwaka huu, serikali imetangaza kuwa sera ya mikopo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya vipaumbele vya taifa na uyatima, ulemavu, ualimu wa sayansi na hisabati, sayansi ya tiba na afya, sayansi asilia, sayansi ya ardhi, usanifu majengo na miundombinu na uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo na gesi asilia na mabadiliko ya tabianchi.
Badru katika maelezo yake, alifafanua kuwa katika kuhakikisha wanafunzi wote wanahakikiwa, bodi hiyo imeandaa dodoso ambalo litawekwa kwenye tovuti ya bodi hiyo na wanafunzi wote ambao wananufaika na mkopo wa bodi ni lazima wajaze taarifa za kiuchumi za wazazi na walezi wao.
Alipoulizwa kwa nini wanafunzi wanaoendelea na masomo wapokwe mikopo wakati waliomba kwa kutumia masharti yaliyowekwa kwa wakati huo, Badru alisema kwamba bodi yake haileti masharti wala mwongozo mpya, bali umekuwepo miaka yote.
“Mwongozo tunaoutumia ni sawa na ule uliotumika mwaka jana, ila kama bodi ni lazima tufanye uhakiki ili kuboresha taarifa zetu ili iwe rahisi kuwadumia,” alisema mkurugenzi huyo mtendaji na kusititiza kuwa wanafunzi wasio na uhitaji wa mikopo lazima waondolewe mikopo hiyo.
Mikopo ni kwa watoto wa maskini Akizungumzia vigezo ambavyo bodi yao imevifuata mwaka huu katika utoaji wa mikopo, Badru alisema kwamba walengwa zaidi ni watoto wenye uhitaji mkubwa hasa watoto wa wakulima ambao wengi wao ni maskini. Alifafanua kuwa katika kuwabaini hao, bodi hiyo imepitia wanufaika wote wa mikopo na shule za sekondari walizosoma pamoja na ada ya mwisho aliyolipa mwanafunzi huyo wakati akiwa kidato cha sita.
“Tuna orodha ya shule zote na ada zao, sasa ili kubaini wahitaji tunaangalia alikosoma mwanafunzi huyo na ada aliyokuwa analipa, hii inatusaidia kuwapata watoto wa wakulima na maskini ili waweze kunufaika na mikopo hii ya serikali,” alisema Badru.
Alifafanua kuwa kuna wanafunzi ambao walikuwa wanasoma kwa ufadhili wa mashirika ya dini au ya mtu binafsi hao nao watawafikiria katika kuwapatia mikopo kwa kuwa taarifa zao wamezijaza kwenye fomu kuonesha aliyekuwa anamlipia ada.
Alisema pia kwamba watoto yatima ambao wamefiwa na wazazi wao nao ni walengwa wengine katika mikopo waliyoitoa.
Alisema wanufaika wengine ni wale ambao wanasoma masomo ya kipaumbele cha taifa. Waliopangiwa mikopo Badru alisema baada ya uchambuzi wanafunzi 20,183 wamepatiwa mikopo ambao wanasoma mwaka wa kwanza na wanafunzi 93,295 ambao wana sifa mbalimbali.
Alisema wanafunzi wengine wenye sifa ambao maombi yao yana kasoro bado wanaendelea kupokea maombi yao yenye marekebisho na watawapatia mkopo.
Mtendaji huyo wa Bodi alisema wanafunzi ambao hawakuridhika na uamuzi wa bodi wanaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku 90.
Alisema bodi yake itashughulikia rufaa hizo ndani ya muda huo ili mwombaji ajue hatima yake. Badru alisema asilimia 90 ya wanafunzi waliomba mkopo wameshapatiwa mkopo na majina yao yamewekwa kwenye tovuti ya bodi hiyo. Kuhusu kiasi ambacho mwanafunzi amepata, alisema wanafunzi watafahamu asilimia waliyopata baada ya kwenda chuoni na kuletewa stakabadhi ya malipo iliyofanywa na bodi kwa chuo husika.
“Kwenye ile orodha hatujaonesha kiwango cha asilimia, ila kiasi hicho kimeoneshwa kwenye pay list tuliyotuma chuoni. Tunapeleka orodha hiyo kwa awamu,” alisema Badru. Pia alisema kwamba wanafunzi ambao hawakujumuishwa katika uchujaji wa mikopo ni wanafunzi 27,053.
Katika orodha hiyo kuna wadahiliwa 6,581 hawakuomba, wadahiliwa 8,781 ni wahitimu binafsi, wadahiliwa 9,940 wamefuzu kwa vigezo ainishi, wadahiliwa 1,416 ni wale ambao waliomba mkopo wakashindwa kurekebisha taarifa zao licha ya kupewa fursa ya kufanya hivyo.
Kwenye orodha hiyo wamo wadahiliwa walioomba mkopo lakini wamehitimu kidato cha sita miaka mitatu iliyopita idadi yao ni 245 na waliomba mkopo wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 30 ni 27,053.

BASI LA ABIRIA LATEKETEA MOTO NA KUUA.

Basi la abiria kutoka mkoani Dodoma, Safari Njema na lori lenye tela lililokuwa limebeba mifuko ya saruji, yameteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu na msongamano wa magari kwenye Barabara Kuu ya Dar – Morogoro. Magari hayo yameungua baada ya kugongana jana mchana.
Ajali hiyo ilitokea saa nane mchana.baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuligonga basi ambalo lilijaribu kulikwepa, lakini likagongwa ubavuni na kusababisha mlipuko na kuwaka moto magari yote mawili.
Basi hilo lina namba za usajili T 990 AQF wakati lori liliteketea kabisa kichwa chake, lakini tela lake lenye namba za usajili T 534 BYJ limebaki.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Garage, Kimara kati ya Suka na Stop Over wilaya mpya ya Ubungo katika Barabara Kuu ya Dar – Morogoro, na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ameungua moto kiasi cha kutotambulika.
Watoto watano na wadada wanne wameripotiwa kuokolewa dakika 15 baada ya magari hayo kuwaka moto, huku abiria wengine wa basi hilo wakiruka kwa nia ya kuokoa maisha yao katika ajali hiyo mbaya.
Hadi jana saa 12.30 jioni, bado magari hayo yalikuwa eneo la ajali na kulikuwa na msururu mrefu wa magari kutoka eneo la Mbezi kwenda jijini Dar es Salaam pamoja na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nje ya Jiji na mikoani na abiria walikuwa wakitembea kwa miguu.
Wakati huo askari wa trafiki ndio walifika eneo la tukio.
Akizungumza katika eneo la ajali jana saa 12.45 jioni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Suzan Kaganda alithibitisha kifo cha mtu mmoja ambaye anaelezwa kuwa ni mtoto, na amehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa utambuzi zaidi.
Kamanda Kaganda alieleza kuwa ajali hiyo imesababisha majeruhi 16 ambao kati yao, 10 hali zao ni mbaya na wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati sita waliruhusiwa kurejea makwao baada ya kutibiwa kwani walipata mshtuko tu.

TOM CLOSE DAKTARI WA AINA YAKE.

Daktari
Tom ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu. Alizaliwa 28 October 1986. Alianza kuimba kwenye Kwaya ya kanisa. Mwaka 2005 Muyombo aliunda kundi lake la kwanza akiwa na marafiki zake wanne wakijiita Afro-Saints.
Wimbo wake wa kwanza akiwa msanii wa kujitegemea ulikuwa Mbwira aliourekodi mwezi Novemba mwaka 2007 kisha mwaka 2008 akaachia Albamu iliyoitwa Kuki. Baadaye alirekodi albamu nne kati ya mwaka 2008 na 2013 zikiitwa Sibeza, Ntibanyurwa, Komeza Utsinde na Mbabarira Ugaruke.
Anautambua muziki wake kuwa wa mahadhi ya "Afrobeat, Dancehall, Pop na RnB ambayo ina mtindo wa kiafrika.
Tom
Ameshirikiana na wasanii kadhaa akiwamo Radio na Weasel, General Ozzey, Knowles na hata Sean Kingston. Ametumbuiza kote Afrika mashariki n ahata Marekani na miongoni mwa wanaomvutia ni Chris Brown na Usher Raymond.
Tom Close alichaguliwa kuwa mshindi wa tuzo ya kwanza ya mwaka ya Primus Guma Guma Super Star ambayo hutunukiwa mwanamuziki anayependwa zaidi nchini Rwanda.
Tom Close
Pia ameshinda na kuwa msanii bora wa mwaka katika Salax Awards mwaka 2009, 2010 na 2011.
Zaidi ya muziki na udaktari wa kutibu binadamu aliousomea katika Chuo cha taifa cha Rwanda na kuajiriwa na Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyoko Kigali, pia ni mwandishi wa vitabu vya Inka Yanjye, Nkunda u Rwanda, na Isuka Yanjye.

MISS TANZANIA AWEKA WAZI ELIMU NA MAISHA YAKE.

Image result for MISS TANZANIA 2016
Baada tu ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2016, Mrembo Diana Lukumay alianza kupokea msg za taarifa zilizosambazwa mitandaoni kuonyesha kwamba alifeli kidato cha nne lakini pia pamoja na hayo bado CV yake ilionyesha anayo degree.
Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema ‘Jina langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na umri wangu ni miaka 18, nilizaliwa Arusha Mount Meru Hospital na ni mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto wanne’
Nilisoma shule ya msingi ya serikali Levolosi 2005-2011, sekondari ya kutwa ya serikali Arusha 2012 -2015,  matokeo ya kidato cha nne nilipata darala la pili… nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa kwenda shule ya Wasichana Bwiru Mwanza’
‘Kwakuwa nilikua tayari nipo kwenye tasnia ya urembo niliamua kutojiunga na masomo hayo kwakuwa yalishaingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya kitongoji ambapo nilijiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016/2017) – Diana
Baada ya kuahirisha masomo ya kidato cha tano niliomba kujiunga na masomo ya ngazi ya cheti kozi ya maswala ya kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha ambapo mpaka masomo yanaanza mwanzoni mwa October 2016 tayari nilikua kwenye kambi ya Miss Tanzania, mafanikio ambayo niliyapata baada ya kuibuka mshindi na kutangazwa kuwa lete Raha Miss Kinondoni 2016/2017’
‘Juhudi zangu hazikuishia hapo, nilipotangazwa mshindi sikubweteka na taji hilo bali niliendelea na kazi zangu za kijamii katika jamii yangu ya kimasai’