Rais John Magufuli ameondoka asubuhi hii kwenye nchini Kenya atakakofanya ziara ya siku mbili.
Mbali na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta, taarifa ya Ikulu imesema Rais Magufuli atafanya mambo yafuatayo:
- Kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
- Kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.
- Kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen, Nairobi, na
- Kuzindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo jijini Nairobi.
No comments:
Post a Comment