Monday, November 7, 2016

TP MAZEMBE YATWAA UBINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA.

Tp mazembe
Timu ya TP Mazembe ya Congo imetwaa ubingwa wa kombe la shirikisho barani Africa, baada ya kuichapa Mo Bejaia ya Algeria kwa 4-1 katika mchezo wa fainali ya pili.
Mabao mawili ya kiungo Rainford Kalaba na mengine ya Merveille Bope na Jonathan Bolingi yametosha kuipa TP Mazembe Ubingwa.
Sofiane Khadir aliifungia timu ya Algeria bao la kufutia machozi na kufanya matokeo ya jumla yawe 5-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Blida.
Mazembe sasa watamenyana na washindi wa Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kati ya Februari 17 na 19 mwakani kuwania taji la Super Cup ya CAF.

No comments: