JAKAYA KIKWETE. |
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, juzi alisafiri nje ya nchi baada ya baadhi ya watu waliokuwa katika ujumbe wake, kukamilisha taratibu ambazo hapo awali zilishindikana na hivyo kuachwa na ndege.
Kikwete na ujumbe wake ambao walikuwa wakielekea nchini Abu Dhabi (Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu – UAE), walishindwa kusafiri Jumamosi iliyopita kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates, iliyokuwa inaondoka saa 10:30 jioni baada ya baadhi ya wajumbe hao kutokuwa na viza.
Ofisa mmoja wa juu serikalini ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu maalumu, akizungumza na na gazeti hili jana alisema: “Ni kweli Kikwete na ujumbe wake walishindwa kusafiri siku ya Jumamosi kwa Shirika la Ndege la Emirates baada ya baadhi ya wasaidizi wake kuonekana kuwa na shida kwenye viza.”
Kwa mujibu wa ofisa huyo ambaye alisema hata yeye amefuatilia kwa undani suala hilo, pamoja na shida hiyo kutokea, rais huyo mstaafu aliruhusiwa kusafiri kwa ndege hiyo, ila washauri wakasema ni vyema aliweke sawa jambo hilo ili aweze kuondoka.
“Sio kama alizuiwa, hapana, viza za wasaidizi wake zilikuwa hazijasoma kwenye system (mfumo), baadaye aliruhusiwa ila washauri walisema ni vyema ali-clear (aliweke sawa) kwanza jambo hilo ndipo aondoke.
“Halafu jambo jingine, kama imetokea shida, kwa mtu kama Kikwete kwa hadhi yake anaambiwa akiwa nyumbani, mambo kama yapo sawa sawa ndio anakwenda airport (uwanja wa ndege),” alisema ofisa huyo.
No comments:
Post a Comment