YAYA TOURE |
Kiungo wa kati wa Manchester City amesalimu amri na kumuomba msamaha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya kutochezeshwa kwa muda na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola.
Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: "Naomba radhi - kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha - wasimamizi wa timu na wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya suitafahamu zilizotokea awali.
"Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii."
Wiki iliyopita, Guardiola aliambia wanahabari kwamba anamuhitaji Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo Dimitry Seluk.
Toure, 33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Baada ya kuachwa nje ya Guardiola kikosi cha wachezaji watakaocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Seluk alisema kuwa kiungo huyo wa kati ''alifedheheshwa'' na kwamba Gurdiola anafaa kumuomba msamaha iwapo City haitashinda kinyang'anyiro hicho.
TOURE AKIWA UWANJANI. |
Ni hapo ambapo Guardiola alijibu na kusema Toure hangecheza tena hadi ajenti huyo aombe msamaha.
''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake hajashirikishwa kwenye kikosi," Guardiola alisema.
Guardiol alikuwa kocha mkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment