Friday, January 20, 2017

SHAMSA FORD: WASANII WENGI HAWAOLEWI KWA SABABU WANATAKA WANAUME WENYE HELA.

Image result for SHAMSA FORD
SHAMSA FORD.
Leo katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na radio stesheni ya Clouds FM, msanii wa kike maarufu kama Shamsa Ford alifunguka na kuhusiana na sanaa yake na mahusiano yake.

Shamsa Ford alisema baada ya ndoa heshima kwa mumewe anayefahamika kwa jina la Chiddy Mapenzi iliongezeka na akaanza kumuogopa, kwa sababu kabla hajaolewa alikuwa anamchukulia poa tu.

Pia Shamsa alisema kuwa wasanii wengi wa kike wa bongo hawaolewi kwa sababu wanataka mwanaume ambaye amekamilika kwa kila kitu, wakati mwanaume anatengenezwa na mwanamke mwenyewe.

Shamsa alimaliza kwa kuwataja wasanii wa bongo movie anaowakubali ni Gabo na Rihama.

No comments: