Friday, January 20, 2017

WASANII WATAKAO TUMBUIZA KWENYE SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA TRUMP SIKU YA LEO.

Jackie Evancho
JACKIE EVANCHO.
Heshima ya kuongoza wimbo wa taifa imepewa msichana wa umri wa miaka 16, Jackie Evancho, ambaye alimaliza wa pili katika shindano la America's Got Talent mwaka 2010.
Sam Moore
SAM NA DAVE.
Sam Moore, wa bendi ya watu wawili ya Sam and Dave, ataongoza wakati wa dansi rasmi ya Liberty and Freedom (Uhuru).
The Rockettes
RADIO CITY ROCKETTES.
Radio City Rockettes pia watatumbuiza katika dansi hizo rasmi, ingawa hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya wanachama wa bendi hiyo.
Wengine watakaotumbuiza katika dansi hizo ni Tim Rushlow na bendi yake ya Big Band, Silhouettes, Pelican212, The Piano Guys, Circus 1903, Cache Olson, Lexi Walker na Erin Boheme.
PIA KUTAKUWA NA DANSI ZA WANAOMPINGA TRUMP. Kutakuwa na dansi mbadala - ambazo zinaitwa Dansi za Amani - ambazo zimeandaliwa na wanaharakati watetezi wa uhuru. Miongoni mwa watakaotumbuiza huko ni dadake Beyonce, Solange Knowles.
Solange Knowles
SOLANGE KNOWLES.
Mwanamuziki wa jazz mshindi wa tuzo ya Esperanza Spalding pia atatumbuiza katika Dansi ya Amani mjini Washington.
Esperanza Spalding

No comments: